Hatimaye kile kilichokuwa kumejificha sasa kimewekwa wazi kwamba Kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa Baraza la vijana-CHADEMA BAVICHA ndiye yuko katika harakati za kumchafua Kiongozi wa upinzani nchini Dr Wilbroad Slaa na ameapa kumuangamiza kisiasa kiongozi huyo kipenzi cha watanzania.
Taarifa za uhakika zilizoibuliwa na gazeti la Tanzania Daima Jumapili zinadai mkakati huo uliopangwa kwa ustadi mkubwa ulianza na Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nauye kuhoji sababu za Dr Slaa kumiliki kadi ya CCM huku akiwa kiongozi wa upinzani.
Baada ya tamko la Nape kundi hilo linaloongozwa na kiongozi huyo wa BAVICHA lilipokea mamilioni ya fedha kutoka kwa wanamkakati hao na kutakiwa kutembea nchi nzima kushinikiza Dr Slaa afukuzwe CHADEMA.
Mkakati wa kwanza ulianza juzi kwa mtu anayejiita mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA Eddo Mwamalala kuitisha mkutano na waandishi Dar na kutaka Dr Slaa atimuliwe mara moja kwa kumiliki kadi ya CCM.Kundi hilo litaendelea na ziara hizo wiki ijayo katika mikoa kadhaa.
Taarifa zinadai Dr Slaa amekuwa mwiba mchungu kwa chama tawala na chama hicho kiko hatarini kuondolewa madarakani.Inadaiwa mipango mbalimbali imepangwa kuhujumu CHADEMA na mkakati wa kwanza ni kumdhoofisha Dr Slaa.
Ingawa gazeti hilo halijamtaja kiongozi huyo wa BAVICHA lakini ni kwa muda mrefu sasa Makamu Mkiti wa BAVICHA Juliana Shonza amekuwa akihusishwa na makundi yanayomhujumu Mkiti wa BAVICHA John Heche.
Source: Tanzania Daima

Mkuu Pasco na Wanajamvi, kwanza kabisa niweke wazi kuwa hili suala la usaliti ndani ya CHADEMA limeshwahi kuzungumziwa hapa jamvini kwa nyuzi kadha wa kadha. Wengine tulitoa ushauri wa bure kabisa kuhusu hali inayoinyemelea CHADEMA.
Mtakumbuka kuwa kumekuwa na nyuzi kutoka kwa Tuntemeke zikishadidia sana uhasama kati ya wanachama.
Sisi tusiochukua upande tulisema wazi kuwa lipo tatizo kwasababu huyu Tuntemeke ingawa anafinyanga taarifa zake lakini ni insider ndani ya CHADEMA na anaweza kufanya spinning hatari zaidi.
Kulitokea mtafaruku ndani ya CHADEMA ukimhusisha Shibuda. Hilo halikuwa tatizo, hatari kubwa ni pale Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Juliana Shonza ambaye bila kujali itifaki, adabu wala utaratibu alikwenda katika vyombo vya habari na kumdhalilisha Mwenyekiti wa BAVICHA katika uso wa dunia.
Suala la Juliana Shonza lilileta mtafaruku mkubwa sana kuliko la Shibuda. Si kwamba lilionyesha mpasauko ndani ya chama bali lilieleza jinsi gani kuna uhasama na kuhasimiana ndani ya chama.
Tulisimama tukaonya kuwa ni lazima hatua zichukuliwe kuleta nidhamu ndani ya chama.
Juliana kwa umri, ufahamu wa kisiasa na mengineyo si tishio kwa uhai wa chama.
Kwa bahati mbaya nguvu hiyo si yake ina vigogo wazito sana na yeye anatumika kama Conduit.
Wakati tunaonya, wakatoke watu ndani ya CHADEMA na hapa ni Dr Kitila Mkumbo na kushauri kuwa vijana wafundwe.
Katika makala yake Dr Kitila haukonekana kusimama kati na kati na kueleza ukweli wa kilichotokea.
Alipindua issue yote na kuifanya kama Ugomvi wa Heche na Juliana. Tulisimama tena na kuonye kuwa hakukuwa na tatizo BAVICHA bali tatizo ni Juliana anayetumika kukiharibu chama.
CHADEMA wakapuuzia ushauri pengine kwa kuchukua ushauri wa mshauri wa chama. It's ok!
Tunafahamu miezi michache iliyopita kulikuw na kauli zilizoonyesha mtafaruku ndani ya chama huku kila mmoja akienda kivyake. Wengine wakiiimarisha chama huko matawini, wengine M4C na wengine wakienda solo wakitangaza nia zao za uongozi. Kilichotokea ni kuchanganya mambo.
Tukaonya pia kuwa kuna dalili za mgawanyiko ndani ya CHADEMA, hilo nalo likapuuzwa.
Kwa taarifa kama iliyopo hapao juu, ni dhahiri kuwa ule mtandao unaotumika ndani ya BAVICHA na baadhi ya vigogo kutaka kusalitiana sasa ni dhahiri.
Nafahamu fika wengi wasingependa kusikia haya, ninachoweza kusema ni kuwa tahadhari imetolewa sana bila kufikiriwa na tunaandika kusaidia vyama kama tulivyowahi kuonya CCM, CUF au TLP.
Hapa ilipofikia ni too late kumwajibisha Juliana hata kama itathibitika. Kinachotakiwa kifanyike sasa ni kushirikiana na Juliana ili kujua wahujumu wa chama na mtandao mzima unaovuruga chama kwa kasi ya juu sana.
Unapokuwa na wasaliti hilo tu linatosha kuwa kiingilio cha maandui. Ni kwa mantiki hiyo Nape anachomeka hoja zake kwa kutambua kuwa kuna udhaifu tayari. Hata kama hoja zake ni dhaifu na za kitoto katika mazingira ambayo ni volatile kama yalivyo ndani ya CHADEMA hilo tu linatosha kuleta sintofaham.
Kuna watu na si CCM ndani ya CHADEMA wanaoona Dr Slaa ni kikwazo cha kufikia ndoto zao. Hawa ndio wanatumia damu changa ya akina Juliana kuleta udhaifu ndani ya chama. Ukisoma maandishi yao na hoja zao wanaonekana kuwa waumini wa demokrasia, wasichokubali nyuma ya mlango ni demokrasia kuchukua mkondo wake.
Nadhani Dr Slaa kama kiongozi mwingine yoyote anapaswa kuwa scrutinized, questioned etc. Na wala sidhani kama ana kinga ya aina yoyote as political leader. He is as vulnerable as any other politician.
Kitu cha muhimu ni kupambana ndani ya chama kwa hoja na mantiki. Kinachotokea sasa hivi ni usaliti unaoweza kuua chama kabisa. Usaliti unafanywa na viongozi wawili au watatu kwa kutumia vijana wasio na ufahamu kama Juliana.
Wanajamvi tatizo sio Nape, ni viongozi wenye matamanio na wanaotumia nafasi zao na uzoefu wao ndani ya chama kutaka kufikia malengo yao kwa kuwatumia akina Juliana Shonza.
Hawa ndio tatizo na wanapaswa kushughulikiwa mapema, ingawa imechelewa sana.
CHADEMA mnabahati ya kupewa ushauri bure, kwa bahati mbaya siku hizi mumeweka pamba masikioni na kufunga vitambaa machoni. Mnafanya kazi kimakao makuu na hamna contact na Political base yenu, hamna contact wala discussion na forum gharama zake ni kubwa sana.