kiongozi wa eneo la Guendi nchini Chad na vipi amesilimu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kiongozi wa eneo la Guendi nchini Chad na vipi amesilimu.

Discussion in 'International Forum' started by Mandago, May 5, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mandago JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2008
  Messages: 238
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kiongozi wa eneo la Guendi nchini Chad na vipi amesilimu.

  Kisa hiki ni cha ajabu na ni cha kuvutia kwa msomaji. Kwani ni kisa cha mkristo mwenye msimamo mkali wa dini yake,lakini Mwenyeezi Mungu akamuhidi na kuwa ni mtowaji daawa maarufu sana katika bara la Africa.

  Jina lake kiukamilifu ni Ramadhani Najili.

  Yeye alikuwa akiwachukia sana waislamu kiasi cha kwamba alikuwa anatamani kama angekuwa na uwezo angewachoma moto.

  Anaanza kuelezea hitoria yake kwa kusema nilikuwa ni mtu aliyepotea mpaka niliposilimu mnamo mwaka 1977,chini ya shekh mmoja wa Nigeria ambaye anafanya kazi katika maktaba moja ya daawa.

  Ambaye aliweza kunikinaisha kwa ujuzi wake wa kuzungumza na kutowa mifano na hadithi za Mtume SWALA LWAHU ALAYHI WASALAM, pamoja na aya katika Quran.

  Zamani mimi nilikuwa nikiona watoaji daawa wa masufi(usufi)walikuwa wakija kuwalingania watu wa eneo letu kuingia katika dini ya kiislamu, kwa kuwapa zawadi kama matunda, ng`ombe na nguo.

  Jambo ambalo wengi walilikataa kwani waliona kwamba dini yao ni ya maslahi.

  Lakini baada ya kuja shekhe huyu wa Nigeria na kutuelezea na kutufafanulia dini ya kiislamu kwa uwazi kabisa,na kusema kwamba si kama wanavyo ielezea wale masufi.

  Akatuelezea vipi washirikina walivyo mwambia Mtume SWALA LWAHU ALAYHI WASALAM kwamba watampa ufalme na mali, basi aache kutangaza dini ya kiislamu na Mtume SWALA LWAHU ALAYHI WASALMU akakataa.

  Na jinsi gani washirikina wa Makkah walivyompinga Mtume SWALA LWAHU ALAYHI WASALAM na jinsi alivyo pigana na washirikina,jinsi alivyo pata mateso mpaka mwisho akashinda kuitangaza dini na ikaendelea kuenea kila pembe.

  Baada yA kutuelezea na kutukinaisha yote hayo na alifanya hivyo kwa miezi kadhaa,tuliingiwa na imani na tukasilimu kwa kukinai na kuitikadi.

  Tumesilimu hali ya kuwa tumetulia nyoyo zetu,kwa kumuabudu Mwenyeezi Mungu mmoja na siyo ibada ya kuabudu masanamu,ili watukuribishe na Mwenyeezi Mungu. Wala si ibada ya mashetani au uchawi.

  Mimi nilisilimu pamoja na watu wengi wa kabila yangu akiwemo baba yangu mkuu wa kijiji cha Mahiim tuki Guend.

  Baba yangu baada ya kusilimu alisema atakuwa kuanzia sasa kiongozi wa kiislamu.

  Na atamuhudumia shekh ambaye aliye tulingania katika uislamu na kutufundisha uislamu.

  Baba yangu alikwenda kukaa nyumbani kwa shekh huyu miaka sita,akimuhudumia kwa mkabala wa kumfundisha uislamu.

  Baada ya hapo akaenda kusoma zaidi kuhusu dini nchini Nigeria ,kisha akawa mtowaji daawa maarufu sana.

  Kisha akaniambia nifanye nae kazi nikamwambia nimesoma katika Quran kwamba Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.

  Baada ya baba yangu kufa mimi nikawa kiongozi wa eneo letu,na katika miaka miwili tokea kuwa mkuu wa eneo hili nilikuwa nikiwa lingania watu katka uislamu na wamesilimu watu 4722 wa kabila la Sara kulayi,miongoni mwao 14 ni mapadre.

  Na katika hao mapdre miongoni mwao wameshaanza kutangaza dini na kufanya majadiliano na watu wanao tangaza dini ya kikristo wa kusini mwa Chadi.

  Ambao wanajaribu kuiharibu dini ya kiislamu,na kuna watu ambao wameritadi kwa hiyo kuwepo watu wa kutowa daawa kusini mwa chad ni muhimu sana.

  Kwani wataweza kuzuwia au kupambana na wakristo hao ambao hujaribu kuwapotosha watu kwa kuwapa pesa,wanawake,kuwapa nyumba za kifahari au mashamba.

  Na kwa kufanya hivi wamewapoteza wengi na kutimiza lengo lao,jambo ambalo limefanya serikali ya chad,kumuweka mjumbe kutoka baraza la kiislamu la chad.

  Mimi walijaribu kunitumia kwa njia hiyo lakini walishindwa na ijapokuwa wanatumia mali na pesa nyingi ili kuivuruga dini ya kiislamu lakini hawakupata lengo lao kama walivyo tegemea kwani wana poteza pesa nyingi kwa mkabala wa baadhi ya watu kidogo tu kuritadi.

  Na walipoona wanashindwa kuwavutia waislamu katika dini yao,wakaanza kuwachochea wapagani ili wawe dhidi ya waislamu. Lakini jaribio lao hilo pia lilishindwa.

  Jumuiya ya kiislamu ilinipatia mwaliko wa kwenda kufanya ibada ya Haji,nilipo kwenda Makkah nikaona waislamu wote wako pamoja hakuna tofauti kati ya mweusi na mweupe, wala masikini wala tajiri wote wamevaa nguo sawa nyeupe na wote wapo katika nyumba moja.

  Sikuweza kujizuwia nikaanza kulia. Na huko sikuenda na ndugu yangu yeyote lakini nilihisi kuwa watu wote ni ndugu zangu. Jambo hili ndio lililo nifanya nizidi kuitangaza dini hii ya kiislamu kwa kadri ya uwezo wangu. Ili niwaokowe ndugu zangu waliyo baki na moto wa jahanamu,nikaamuwa mara tu nitakapo maliza ibada yangu ya haji nitaanza daawa katika nchi ya chad.

  Nilipo rudi kutoka Hajj nikaamuwa kuanzisha kituo cha daawah cha kiislamu katika misikiti na mashule. Na nina mshukuru Mwenyeezi Mungu nimeweza kujenga misikiti 12,na shule moja ya vijana wa kiislamu,pia nimechimba visima 12 katika eneo la Guendi.

  Pia nimeungana ili kuunda jumuiya ya kutowa zoezi kwa waongofu,ili wawezi kutowa daawa ya kiislamu.

  Kwani lengo langu tokea mwanzo lilikuwa ni kuitangaza dini ya kiislamu,kuifundisha adabu zake, na nilitilia mkazo kujifundisha lugha ya kiarabu na dini ya kiislamu ili nifungue chuo cha kufundisha Qurani tukufu na sunna za Mtume SWALA LWAHU ALAYHI WASALAM.

  Na nina mshukuru Mwenyeezi Mungu nimeshafunguwa chuo hiko.

  Jambo ambalo linanitatiza hivi sasa ni vikwazo ambavyo ninawekewa na wakristo, na hii si kwa mimi tu bali kwa watoaji wote wa daawa wa chadi ya kusini,na sana katika maeneo ya Maadi, kwani watu wengi ni masikini huko.

  Kwani wengi wanaosilimu katik aeneo hilo hawana hata nguo ya kuwasitiri hata kwa kuswali swala zao. Si hivyo tu bali katika eneo hilo hakuna hata njia ya kupita kwa gari.

  Jambo ambalo limefanya kuwa n awapagani wengi na ni fursa ya wakristo kwa kuwatolea wito au kuwalingani katika dini yao.

  Pia sisi katika maeneo yetu tumepungukiwa na walimu wa kufundisha dini kwani waislamu wengi hawajuwi isipokuwa shahada tu.

  Na kwa hali hii mimi nina hisi kuwa sisi ni sawa na wakristo ambao wanawalingania watu kwa kujitahidi kuwapa vitu vya lazima ili dini yao ishinde,na kwa msingi huu katik aeneo hilo wakristo ni wengi sana.

  Na father Vatican alipozuru eneo hilo la Guendi katika ziara yake ya mwisho katika Bara la Africa,alikutana na walinganiaji wa kikristo wa eneo hilo,akapanga mpango wa hali ya juu wa kufanya eneo hilo liwe la wakristo. Ambapo aliwaletea walinganiaji wengi kutoka Europe.

  Si hivyo tu bali aliwaletea na pesa nyingi na akawaambia kuwa atawajengea kanisa kubwa katika eneo hilo. Na mlinganiaji mmoja kutoka Italy aliniambia utakapo fika mwaka 2002 eneo hili lote litakuwa ni la wakristo tu.

  Na kila mwezi wanafanya maonyesho ya kitaifa na kuwapa wapagani wa eneo lile chakula,vinywaji na mahitaji yote. Si hivyo tu bali hutembelea vituo vya mayatima na sehemu mbali mbali za mafakiri na kuwalingania ili wawa batize watoto wao na yote hayo kwa mkabla wa pesa.

  Hawa watu ni wabaya sana wanafanya kazi zao kwa jina la msalaba mwekundu,pia nimegunduwa kwamba wanawapa dawa wanawake bila ya wao kujuwa ili wasizae tena.

  Na hii ndio njia wanayo tumia ili kuuondosha uislamu katika Chad.

  Mwisho anamalizia kusema lakini mimi nimeonja utamu wa dini ya kiislamu.

  Na hakuna mtu yeyote atakaye pinga kuwa dini ya kiislamu ni dini ya usawa na uadilifu.

  Katika usilamu hakuna tofauti kati ya masikini na tajiri isipokuwa kwa ucha Mungu,waislamu wote huelekea kwa Mwenyeezi Mungu na wote ni waja wa Mwenyeezi Mungu.
   
 2. g

  gepema Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tafuta kitabu kinachoitwa the Torn Veil,uende ukapumzike kwa amani
   
 3. K

  Kivia JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nimekupata mkuu, asante kwa kutulingania- jazakallah kheir.
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...asubiri akifa akamuliwe ma.i!!
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Dini walete Waarabu na Wazungu.. sisi Waaafirika bado tunashabikia? Kwa nini Imani zetu za Jadi tuliziacha? Only in Africa .. Wajapan, India wameshika dini zao.. Je leo wapo wapi?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...