Kiongozi wa dini usihubiri amani ya kisiasa bali hubiri amani ya Mungu

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,082
Ndugu zangu kuna tofauti kubwa kati ya amani ya kisiasa na amani ya Mungu.

Amani ya kisiasa inapatikana kwa kufuata sheria zilizomo ndani ya katiba ya nchi.

Wakati Amani ya Mungu inapatikana kwa kutii sheria za Mungu na kuyafuata na kuyatii maandiko ya Neno la Mungu.

Amani ya Mungu inauwezo wa kuleta amani ya kisiasa.

Amani ya kisiasa haina uwezo wa kuleta amani ya Mungu.

Nashangazwa sana na baadhi watumishi wa Mungu hasa maaskofu badala ya kuhubiria watu wapate Amani ya Mungu wao wanatumia nguvu nyingi kuhubiria watu wapate amani ya kisiasa.

Maasikofu wamesahau wajibu wao, sasa wanatumia nguvu nyingi. Wanahubiria watu ili waingie kwenye ufalme wa ikulu badala ya kuhubiria watu waingie kwenye ufalme Mbinguni.

Mungu tusaidie sana, Yesu alipokuja duniani hakuhangaika na amani za kisiasa hakuhangaika na ufalme wa dunia hii kama jinsi ambavyo tunawaona baadhi ya maasikofu wanahangaika na kujitutumuakuhubiri hadharani kabisa na kuzungumzia amani ya kisiasa.

Askofu inatakiwa uitafute amani ya Mungu, kwa kuwahubiri watu waokoke sio kunga'ng'ana kudai katiba mara tume huru.

Askofu katiba yako ni biblia hubiri watu waokoke amani ya kisiasa na tume unayoitaka iko ndani ya biblia humo. Hubiri watu waokoke wote watakua na amani.

Acha uvivu na kuanza kutumia nguvu ya akili. Rahasha hiyo sio njia sahihi. wewe inatakiwa utumie nguvu ya imani na kuomba tena ukiwa peke yako sio kutangaza hadharani.

Rejea
 
Maaskofu wa makanisa ya KKKT, Anglikan,Moravian,na RC,Wengi wao ukisikiliza mahubiri yao utazani hotuba ya wakuu wa mikoa.Mahubiri yao hayana upako kabisa. Shida ilianza baada ya kukubali kutumika kisiasa.Biblia wanaigusa gusa tu juu juu. Ndio maana hata kuombea wagonjwa hawawezi. Kitu wanachoweza ni kuunga juhudi.
 
Maaskofu wa makanisa ya KKKT, Anglikan,Moravian,na RC,Wengi wao ukisikiliza mahubiri yao utazani hotuba ya wakuu wa mikoa.Mahubiri yao hayana upako kabisa. Shida ilianza baada ya kukubali kutumika kisiasa.Biblia wanaigusa gusa tu juu juu. Ndio maana hata kuombea wagonjwa hawawezi. Kitu wanachoweza ni kuunga juhudi.
Siku hizi imekua ngumu sana kuwatofautisha hawa jamaa na wanasiasa.
 
Kwahiyo wewe na ukoo wako hamtaki hata kusikia ukweli hata ule uwakumbushao kuacha uovu hata ule unaohusiana na sii hasa.
 
Yuko jamaa anazunguka makanisa ya dom na dar jpili nakujifanya anamjua mungu,kumbe ni shetani anaependa kuua wanaomkosoa
[/QUOTE
Xmass kwake Ingekuwa na maana Kama angewasamehe wote waliomuudhi kwa kuwatoa gerezani na utakatifu sio kupiga picha kanisani Ili kuwarishisha wanadamu bali ni kuishi imani
 
Kwani hao maaskofu wanaishi kwenye sayari tofauti hadi wasihubiri amani ya dunia, hebu toa ufafanuzi amani ya Mungu inahubiriwaje, na kwa jinsi gani hao viongozi wa dini hawaihubiri...
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom