Kiongozi wa chama amuandikia barua Rais Samia

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
602
1,526
Mapendekezo ya ACT Wazalendo Kwa Rais Samia Suluh Hassan ili kuzifanya chaguzi kuwa za ushindani, huru na zenye uwanja sawa kwa vyama vyote vinavyoshiriki, tunaleta kwako mapendekezo yafuatayo;

1. Uanzishe mchakato wa kuifanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya shughuli zake kwa Uhuru. Tunapendekeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe na Watumishi wake wanaowajibika kwa Tume tena wasiwe ni makada wa chama kimoja cha siasa.

2. Uanzishe mchakato shirikishi wa kupitia upya Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuondoa vifungu vyote vinavyojinaisha siasa na kubana uhuru wa vyama vya siasa kutekeleza majukumu yake. Tunaomba Vyama vya Siasa virejeshewe haki yake ya kisheria ya kufanya mikutano yake bila bugudha. Haki hiyo iliondolewa kwa amri ya Rais wa awamu ya tano.

3. Kupitia Taasisi zinazomilikiwa na Vyama vya Siasa nchini kama vile Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), uanzishe majadiliano miongoni mwa vyama ili kujenga kuaminiana na kutatua migogoro kwa njia za amani pale inapotokea.

4. Unasihi vyombo vya ulinzi na usalama kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kulingana na viapo vyake, kutojiingiza katika itikadi za kisiasa, kutenda haki kwa wote na kuachia mara moja wanachama wetu na wa vyama vingine vya siasa waliokamatwa na kuwekwa magerezani nyakati za chaguzi kwa makosa ya kubambikiza.

75dky3.jpg
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom