Kiongozi wa CHADEMA tawi la Magadirisho avaa gamba la CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi wa CHADEMA tawi la Magadirisho avaa gamba la CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Emashilla, Jul 22, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo Tawi la Magadirisho, Mji mdogo wa Usa-River kimeridhia uamuzi wa mwenyekiti wake wa Tawi Bwana Nuru Maeda kuvua gwanda na kuvaa gamba la CCM.

  Tukio hili liltokea siku ya Jumamosi jioni, tarehe 21 Julai, 2012 katika mkutano wa CCM wakati Bwana huyu alipojipitisha katika mkutano huo na kujikuta akitekwa nyara na kukubali kujiunga na CCM.

  Muda mfupi leo asubuhi nimezungumza na mama Furaha ambaye alikuwa miongoni mwa vigogo wa CCM waliomteka mwenyekiti wa CHADEMA,ambaye alinihakikishia kwamba yeye alimbeba mgongoni wakati walipomteka na kukubali kujiunga nao. Na aliongeza kwamba bado wanamuwinda kigogo mwingine wa Chadema hapa Magadirisho.Jina halikutajwa. Huenda ni katibu wa Mwenyekiti wa Tawi Bwana Peter Mkambi au ni yeyote mwingine ila hakutaka kumtaja. Siri wanayo CCM wateka nyara.Tusubiri matokeo yake.

  Mtakumbuka mwenyekiti huyu ndiye yule aliyetekwa na kuteswa na viongozi wa CCM kipindi cha kampeni ya ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki. Nuru Maeda alipata umaharufu mkubwa na habari zake kutawala vyombo vya habari na vikao vya bunge, lakini sasa amekuwa mateka kama vile mbwa alyerudia kulamba matapishi yake. Mama Furaha aliniambia kuwa hawampi cheo chochote kwani yeye anamfahamu tangu walipokuwa shule ya msingi. Alisema kuwa ni mtu wa fujo na vurugu tangu zamani.


  Mazingira ya kutekwa kwa Mwenyekiti huyu wa Tawi CHADEMA yalikuwa kama ifuatavyo:  1. Ahadi ya fedha nono. Hana kazi ya kumpa kipato. Siku hiyo alipotekwa alipewa mchango wa fedha zilizojaa kofia kama pongezi kwa uzembe wake wa kuhama CHADEMA
  2. Kuanzishwa serikali ya mseto wa CCM na CHADEMA. Hapa alipewa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya kitongoji mnamo tarehe 29 Juni, 2012. Cheo ambacho alitakiwa kujiuzulu mara moja na wanachama wa CHADEMA magadirisho katika kikao cha 13 Julai,2012
  3. Kujengewa hofu juu ya tuhuma zake za kutekwa kipindi cha kampeni ya uchaguzi mdogo wa mbunge Meru Mashariki ambapo Mh.Joshua Nassari(CHADEMA)alichaguliwa kuwa mbunge. Huenda wazee walimfuata ili asipeleke kesi mahakamani kulinda maovu ya CCM
  4. Kushindwa kutapeli kadi za CHADEMA kutoka ofisi ya kata ambazo alitaka kuwapa watu wake wazirudishe CCM ili kushawishi watu kuwa alikuwa kigogo wa ukweli. Alidai katika kikao cha CHADEMA siku chache kabla ya kutekwa kuwa viongozi wa kata CHADEMA ni matapeli.
  5. Tuhuma dhidi ya kiongozi mmoja wa CHADEMA alizotakiwa kuzidhitisha katika kikao cha tarehe 18 Julai 2012 na kushindwa. Kisha kikao cha kumjadili kilipangwa kufanyika katika ngazi ya tawi tarehe 21 Jualai, 2012. siku hiyo ambayo kikao kilikuwa kinamjadili ili kumvua uongozi ndipo taarifa zikawafikia wajumbe kuwa tayari Nuru Maeda yuko mgongoni mwa mama Furaha na anatukana na kukashifu CHADEMA hadharani huku akishangiliwa na kupepewa kanga za kijani.
  6. Jaribio la kutaka uhusiano fulani na mke wa mwanachama wa CHADEMA na kulipuliwa kwenye kikao. Jambo ambalo amelithibitisha kwenye kadamnasi baada ya kutekwa hiyo jumamosi. Siku hiyo(Jana)alisema kuwa amehama kutoka CHADEMA kwa sababu ya Mke na Mume.Hakuwataja majina.
  7. Kukataliwa na wanachama kugombea katika chaguzi zijazo baada ya kuonekana ni mtu wa tamaa na lugha chafu kwa wananchi. Huenda CCM walimuahidi uongozi kwani alitangaza kuwa atavuta fomu ya kugombea uenyekiti wa serikali ya mtaa utakao fanyika siku zijazo kwa tiketi ya chama kilichomteka nyara.
  8. Jaribo la kusambaratisha Kikundi Cha Maendeleo Ya Wanawake Magadirisho(KIMAWAMA)kushindikana. Alijaribu kuwatapeli wanakikundi kwa kuwataka wachange kila mmoja Shilingi Elfu Tano(5,000/=)ili apewe kwa ajili ya kukifanyia mipango ya maendeleo. Wanachama walikataa, Ndipo aliapa na aliadai kuwa watamtambua kuwa yeye ni nani kwani atakifuta na kuanzisha kipya.
  9. Alikataa kufanya kazi na Katibu wa KIMAWAMA kwa madai kuwa anamzuilia na kumkwamisha katika mipango yake.Yeye sio mwanamke lakini alikuwa akijipenyeza kwenye kikundi na kutawala vikao.

   Hali ya CHADEMA Magadirisho baada ya mwenyekiti wao kutekwa ni hii:

  1. CHADEMA ni chama imara na inaendeleza vuguvugu la mabadiliko kwa kauli ya nguvu ya umma.
  2. Wanachama wamefurahi sana kuondokewa na mtu ambaye alilewa sifa za kuwa mateka kipindi cha uchaguzi
  3. Ndoa yake na mwenyekiti wa tawi CCM Magadirisho ni matunda ya tamaa ya zawadi za uchumba. Ataitwa mwenyekiti wa CCM wa Nidhamu Magadirisho
  4. CHADEMA inaendelea kuelimisha umma juu ya haki na wajibu wao katika kuwaletea wananchi mabadiliko na maendeleo
  5. Nguvu ya CHADEMA imeongezeka kwani wanachama wa CCM wanataka kumkimbia huko kwa kujiunga na CHADEMA.


  SOURCE: Mimi mwenyewe kutoka eneo la tukio Magadirisho, Usa-River, Arusha.
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Hakuwa kamanda wa ukweli!

  I think he was unsound doing such thing!

  Kweli mtu mwenye utimamu na muelewa wa mambo ana hamia ccmwabepande! Siamini
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,792
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  Vipi mzee mangungu yupo magadirisho??
   
 4. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #4
  Jul 22, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yupo. Ni jirani yangu
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Watarudi tu CCM mmoja baada ya mwingine. Let's wait!
   
 6. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Njaa ndio zinamsumbua,siku akijua bwana aliyemkubalia hana mapenzi ya dhati atarudi kwenye ukombozi.
   
 7. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Huyo akapimwe!
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mwache aende ni haki yake...
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kumbe alikuwa mzigo/ gamba ndani ya CDM! Bora amerudi gambani.
   
 10. h

  hans79 JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Hadithi za fisi,eti amfuamta mtu nyuma nyuma akisubiri mkono ondoke lakini wapi hadi jamaa kaingia kwake bila ya mkono kudondoka.
   
 11. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #11
  Jul 22, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waroho wa hizo kodi zetu mnazowahonga ni kweli watarudi mabwepande kama wewe unavyoendelea kubaki ccm kwasababu iyo hiyo ya kuzifaidi kodi zetu. Lakini Mungu mkubwa, iko siku haki yetu itapatikana.
   
 12. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,925
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  nenda rudi nenda rudi .............anastahili ahurumiwe
   
 13. F

  FUNGO jr JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rejao, nape,mkigoma,mpesapesa,ritz,mamaporojo. Fanyeni sherehe
   
 14. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,269
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa alitekwaga akaminywa nyeti zake na mengine mengi ya aibu.

  Kwa uoga amesalimu amri jana.
   
Loading...