Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe apata ajali Mkoani Kigoma, asafirishwa kwa ndege kwenda Dar

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,907
25,180
Kiongozi wa chama ndugu Zitto Kabwe amepata ajali mida hii huko Kigoma kusini akiwa na watu wengine wanne jumla watu 5 wote wazima japo kiongozi ana majeraha anapelekwa hospitali habari zaidi kufuata baadaye.

======

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Zitto Zuberi Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini leo Jumanne Oktoba 6, 2020.

Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.

Wamepata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye wamepelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Imetolewa na:

Arodia Peter

Afisa Habari ACT-Wazalendo

Oktoba 6, 2020

UPDATES;

Updates Juu ya Ajali ya Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe pamoja na Viongozi wengine wa ACT Wazalendo Kigoma

Muda huu Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe pamoja na Majeruhi wenzake wanavushwa kwenye Mto Malagarasi ili kufika Ilagala, ambako ni Kilometa 50 kufika Kigoma Mjini. Tayari ndege ya Kuwasafirisha kuwaleta Dar es Salaam kwaajili ya Matibabu zaidi imeshafika Uwanja wa Ndege wa Kigoma.

Majeruhi wote hali zao zinaendelea vizuri

Janeth Rithe
Naibu Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, ACT Wazalendo
Oktoba 6, 2020

=====

UPDATES;

TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe pamoja na majeruhi wengine 4 waliopata ajali ya gari jana Oktoba 6, 2020 katika Jimbo la Kigoma Kusini wanatarajia kuwasili Dar es Salaam majira ya saa 5:00 asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa zamani terminal 1.

Baadaye majeruhi wote watapokelewa na gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Mbali na Zitto, majeruhi wengine ni pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Said Rashid Bakema., Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Soily Simon Matete pamoja na Boaz Chuma, (mwanachama).

Tutaendelea kuwajulisha kadri taarifa zinavyopatikana.

Imetolewa na
Janeth Joel Rithe
Naibu/ Katibu Uenezi, Habari na Mahusiano ya Umma.
Oktoba 7,2020

======

UPDATES 08/10/2020

Updates Juu ya Ajali ya Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe pamoja na Viongozi wengine wa ACT Wazalendo Kigoma

Majeruhi watatu kati ya wanne walioletwa Dar es Salaam kwa vipimo na matibabu zaidi baada ya ajali ya Kigoma wamepata ruhusa. Walioruhusiwa kurudi nyumbani baada ya vipimo mbalimbali na matibabu ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, Ndugu Said Rashid Bakema, Katibu wa Jimbo la Kigoma Kusini, Ndugu Soily Simon Matete, pamoja na Mwanachama Mwandamizi, Ndugu Boaz ‘Chuma’ Ndaha.

Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe yeye bado anaendelea na matibabu, hajapata ruhusa kutoka hospitalini, lakini afya yake imeimarika zaidi.

Janeth Rithe
Naibu Katibu wa Uenezi,Habari na Mawasiliano kwa Umma, ACT Wazalendo
Oktoba 8, 2020

Pichani ni gari mbili zilizopata ajali kwenye msafara wa Kiongozi wa chama ndugu Zitto Zuber Kabwe nawenzake wanne 4.

Gari moja ilikuwa niyamgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ndugu SAID RASHID BAKEMA na nyingine ilikuwa niya kiongozi wa chama ndugu Zitto
IMG-20201006-WA0028.jpg
IMG-20201006-WA0029.jpg
IMG-20201006-WA0027.jpg
IMG-20201006-WA0030.jpg
 
Kipindi cha nyuma,ilikuwa ikifikia kipindi cha uchaguzi ilikuwa ni kawaida kusikia jirani kapotelewa na mtoto na hasa wenye ulemavu wa ngozi,

Mwaka huu, ni ajali, ajali, ajali,

Duu! Inaogopesha aisee!!

I wish you a speedy recovery Mr. Zitto
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom