Kiongozi wa ACT-Wazalendo atoa waraka mzito kwa Serikali ya Magufuli juu ya sakata la Uchaguzi

Faridi

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
672
274
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.

Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa Zanzibar, ACT-Wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine walioshiriki kwenye uchaguzi.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa vyama vya CCM na CUF kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.

Suluhisho la hali hii ni vyama vingine vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya Wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo viwili.

Kwa ujumla hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya siasa za Zanzibar.

ACT-Wazalendo kinapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa subira na uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali ya sintofahamu.

Imetolewa leo, Desemba 20, 2015.

Mji Mkongwe, Zanzibar

Kabwe Z Ruyagwa Zitto, Mb

Kiongozi wa Chama
 
Kwa hiyo tunampangia rais aina ya ulinzi.vita ya kutumbua majibu si mchezo lazima utumie mbinu mpya za ulinzi wa nchi
 
Shein achiachiye tuu mpka anaona aibu ccm wanamlazimisha jamaa mcha Mungu anaenda tuu ila ukweli anaujua
 
ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

ACT wazalendo Mambo ya ulinzi wawaachie wataalam wa mambo ya ulinzi wao waendelee na siasa.Ukiona mwananchi anaogopa askari huyo lazima awe mhalifu
 
mosi, mshindi wa uchaguzi mkuu wa zanzibar uliofanyika oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde serikali ya umoja wa kitaifa na kuwaunganisha wazanzibari.

Pili, act-wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda bandari, uwanja wa ndege, vituo vya redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa zanzibar, act-wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine walioshiriki kwenye uchaguzi.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa vyama vya ccm na cuf kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.

Suluhisho la hali hii ni vyama vingine vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo viwili.

Kwa ujumla hali ya kisiasa zanzibar ni mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya siasa za zanzibar.

Act-wazalendo kinapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa zanzibar kwa subira na uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali ya sintofahamu.

Imetolewa leo, desemba 20, 2015.

Mji mkongwe, zanzibar

kabwe z ruyagwa zitto, mb

kiongozi wa chama

hayo anayo ongea kabwe ametumwa na ccm kufanya hivyo kwa kuwa vikao vyao vimefikia hapo.
(1)kabwe ni mpinzani ndani ya ccm
(2)kabwe ana pambana na ukawa
 
zitto demokrasia hakuna daini haki ya kukutana vinginevyo mtaenda mwendo wa hapa kazi.zitto ulibaki bungeni umekwisha bara na pwani
 
Kwa hiyo tunampangia rais aina ya ulinzi.vita ya kutumbua majibu si mchezo lazima utumie mbinu mpya za ulinzi wa nchi

majipu ya zanzibar ni ccm kung'ang'ania madaraka wakati wameshindwa uchaguzi wanajaza wanajeshi ili kulinda jipu lao lisitumbuliwe
 
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.

Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa Zanzibar, ACT-Wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine walioshiriki kwenye uchaguzi.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa vyama vya CCM na CUF kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.

Suluhisho la hali hii ni vyama vingine vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya Wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo viwili.

Kwa ujumla hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya siasa za Zanzibar.

ACT-Wazalendo kinapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa subira na uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali ya sintofahamu.

Imetolewa leo, Desemba 20, 2015.

Mji Mkongwe, Zanzibar

Kabwe Z Ruyagwa Zitto, Mb

Kiongozi wa Chama

shein ni mstarabu ameonyesha kila dalili ya kukubali kushindwa ,ila kuna madudumizi yako nyuma yake yalizoe vya kunyonga ndio yanayompelekesha
 
Huyu jamaa ni mtu hatari...Waliungana Deo [RIP] ( CCM) kupinga vibaya Muhongo,Leo anamkubali.Anaungana na Jussa ( CUF) -UKAWA sasa kumpinga Shein (CCM) zanzibar, Huku Tanganyika anakubali Ccm ili kuipinga UKAWAHuyu ni hatari kwa Usalama....HAFAI!!!!
 
ACT wazalendo Mambo ya ulinzi wawaachie wataalam wa mambo ya ulinzi wao waendelee na siasa.Ukiona mwananchi anaogopa askari huyo lazima awe mhalifu

...vipi ukiona serikali inajaza askari wengi penye amani?!
 
Mosi, Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu atangazwe haraka ili hali ya utulivu wa kawaida irejee. Mshindi ale kiapo, aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kuwaunganisha Wazanzibari.

Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

Tatu, kwa ajili ya mustakabali mwema wa Zanzibar, ACT-Wazalendo kinataka mazungumzo yoyote kuhusu uchaguzi uliofutwa yahusishe wadau wa vyama vyote na taasisi nyingine walioshiriki kwenye uchaguzi.

Hii si mara ya kwanza kwa viongozi wa vyama vya CCM na CUF kukutana na kufanya mazungumzo baada ya kutokea matatizo. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba suluhisho huwa si la kudumu na badala yake matatizo yaleyale hujirudia baada ya muda.

Suluhisho la hali hii ni vyama vingine vyote, kujumuishwa katika aina hii ya mazungumzo ili kupata mawazo jumuishi na yatakayowakilisha sehemu kubwa zaidi ya Wazanzibari ambao wengi wao, hasa kizazi kipya, hawana uhusiano wowote na vyama hivyo viwili.

Kwa ujumla hali ya kisiasa Zanzibar ni mbaya sana na inatisha kwani wananchi wanaishi kwa hofu kubwa na hawaelewi kinachoendelea, ukimya uliotamalaki hauashirii hatima njema ya siasa za Zanzibar.

ACT-Wazalendo kinapenda kutumia nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa subira na uvumilivu wa kiwango cha juu waliouonyesha katika kipindi hiki cha hali ya sintofahamu.

Imetolewa leo, Desemba 20, 2015.

Mji Mkongwe, Zanzibar

Kabwe Z Ruyagwa Zitto, Mb

Kiongozi wa Chama
Wana uhusiano na vyama gani?! Hao kizazi kipya ni zaidi ya 50% ya wapigakura, na kwa matokeo ya uchaguzi yanayojulikana hadi sasa hakuna chama tofauti na ccm na cuf kilichofurukuta huko, hao kizazi kipya hawakupiga kura?!
 
Pili, ACT-Wazalendo imebaini kuwapo kwa idadi kubwa isivyo kawaida ya wanajeshi wanaolinda Bandari, Uwanja wa Ndege, Vituo vya Redio na maeneo mengine muhimu. Chama chetu kinataka askari hao warejee makambini kwao kwani uwepo wao katika maeneo ya kiraia unasababisha hali ya shaka na hofu miongoni mwa wananchi.

1. Katika historia ya Tanzania, wanajeshi wamekuwa wakiishi makazi ya raia kwa miaka nenda rudi, na sio wanajeshi tu hata vyombo vingine vya ulinzi na usalama......tunakula nao, tunakunywa nao na tunataniana nao bila ya kujali kazi zao......hivyo, sio jambo baya kama serikali imeona busara kuwatumia wao mahali wanapoona kuna haja ya kufanya hivyo......na wala haijawahi wakwaza raia! Kwakuongezea ni kuwa, wananchi wapo more comfortable na wajeda kulikoni na police.

2. Hata maeneo anayoyataja Zitto, kama viwanja vya ndege, bandari na vituo vya redio, hakika siyo makazi ya watu ili isemwe kuwa inawanyima wananchi usingizi! Kwahiyo ni hoja mfu!

3. Kauli zako zinajichanganya, mosi yako unataka tume imtangaze mshindi haraka.....jambo ambalo ni sahihi, lakini pia unataka vyama vingine vihusishwe kwenye mazungumzo! Kama matokeo yakitangzwa "mazungumzo unayoyataka ni yanini'? Hivyo wito wako wa kuhitajika mazungumzo una maana kwa hali ilivyo sasa ambapo matokeo hayajatangazwa!

- Wito wa kuhusisha vyama vingine, ni kuzidi kulitia ugumu jambo husika na kutia chokochoko zisizo na maana, pia kuna binadamu wengine wataona hiyo ni sehemu yakujitafutia umaarufu badala ya umoja unaotarajiwa! Na hata ikiwa kuna haja ya kujumuisha vyama vingine, basi ACT hakifai maana katika kura za ngazi zote nchini sidhani kama kimepata hata 5% ya kra zote!

- Ni bora mazungumzo yaendelee kwa hali iliyopo sasa, kwani bado hali ya Amani ni shwari na hakuna chokochoko zisizo za msingi!

- Vyama vya upinzani, vimsaidie Rais kwa sasa kuainisha maeneo yenye udhaifu na ubadhilifu, na mpendekeze solution siyo kusubiri kosa ili mkosoe, maana rais huyu anaonyesha nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi!
 
Hujaelewa tamko LA Zitto au imeongozwa na msukumo wa ki demagogue
 
Katumwa na CCM huyu anatafuta pa kuingilia akipewa nafasi ahujumu.Huyu alifurahi Kafulila kushindwa,mapenzi kayatoa wapi?
 
Mueshimiwa unahoja nzuri lakini mazungumzo ya nini wakati wananchi walishapiga kura maana yake atangazwe mshindi na sio mazungumzo ya kumsaidia raisi huwezi lazimisha jana iwe leo haiwezekani weka wazi tu ili tuone na maelewano ya upande wa pili ambao tunauhofia lakini naamnini woga wetu ndo unatunyima ruhusa ya kuiweka haki bayana eti itakuwaje? Lakini ni hofu tu.
 
haya yote aliyaanzisha nyerere, zanzibar cuf haiwezi kupata urais hata kama wazanzibar wote wataipigia cuf.
 
Anakulipa shilingi ngapi hadi unapofuka akili kiasi hicho?

Soma maandiko yangu kuhusu Zitto kwenye hili jukwaa ndio utajua msimamo wangu kuhusu siasa za Zitto, sihitaji kulipwa ili nitumie akili Zangu vizuri Mimi sio political demagogue
 
Back
Top Bottom