Kiongozi vs Mtawala

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tofauti kati ya mtawala na kiongozi iko katika malengo yao ya kutafuta, kuchukua na kuyatumia madaraka.

Hiki ndio kiini cha uongozi na utawala. Kila kitu tunachokiona katika dunia kiwe kizuri au kibaya, kimetokana na malengo na dhamira. Kwahiyo kuna dhamira mbaya na nzuri. Inategemea jinsi gani tunaongoza akili na mawazo yetu na huko ndipo matokeo yatakapokuwepo. Dunia tuliyonayo ni matokeo ya actions na thoughts za binadamu. Without thoughts and without actions binadamu asingekuwa advanced kiasi hiki tunachomuona. Kwahiyo thoughts and actions ni vitu ambavyo lazima viendane pamoja ili vitoe matokeo. Na vitu hivi viwili always lazima vitoe matokeo chanya au hasi.

Mtawala hutumia watu na rasilimali zake ili kufikia malengo yake binafsi. Watu si mali kitu kwake ni objects & subjects. Kwakuwa watu walio wengi ni maskini na wengine uwezo wao wa kufikiri sio mzuri sana huwatumia ili kufikia malengo yake binafsi kwa kuhonga, kudanganya, kwa hila na wakati mwingine vitisho. Kinacho msukuma kuingia kwenye siasa ni mali ili aitumie mali hiyo kuishi maisha ya anasa na starehe. Ni agharabu kwake kuwa na maono ya kitaifa. Maono yake ni ya kibinafsi ya kujenga his own empire'. Na anapochukua hatua katika jambo lolote lile anafanya ili kupata kiki ya kisiasa.

Kwahiyo mtawala yuko kwaajili ya manufaa yake, manufaa ya jamii kwa ujumla si ya msingi sana kuliko manufaa binafsi. Unaweza kuwaona katika maisha wanayoishi ambayo yamejitenga na maisha ya kawaida ya raia wao, wakitopea kwenye starehe na anasa huku raia waliowengi wakiishi maisha ya umaskini wa kutupwa. Na kwa unafiki hujumuika nao nyakati za uchaguzi na kujifanya ni miongoni mwao wakila wali na maharage pamoja nao kwenye hadhara na kucheza nao ngoma. Wakipita huku na huko wakigawa tisheti na chumvi.

Kwao uadilifu sio kitu kuliko mali na madaraka. Watafanya kila wawezalo wabaki madarakani kwa njia chafu au njema. Kutokana na aina ya maisha wanayoishi vijana wengi huingia kwenye siasa si kwaajili ya utumishi na maadili waliyonayo ya kutumikia umma, bali sababu ya mali. Na hapo ndipo mtafaruku na migawanyiko inapoanza . Ikiwa siasa sehemu ya kutafutia mali na si utumishi hapo ndipo mitafaruku huanza. Na kila uchaguzi huleta madhara na migawanyiko pamoja na maumivu kwa jamii. Hakuna rationality inayoongoza ni tamaa ya mali na madaraka na sio uongozi.

Hakuna malumbano ya kimsingi ya hoja wala mtu mwenye maono anayesimama na kuzungumza mikakati gani na njia gani tunazoweza kufanya kuondokana udhaifu tulionao wa ujinga, maradhi na umaskini. Nimeshuhudia matusi, uongo, ulaghai , kushushiana heshima na hadhi chuki zikisambaa siku za uchaguzi. Watu wakipambana kwaajili ya mlo. Kama force inayotudrive kuingia kwenye siasa ni mali si utumishi maumivu na migawanyiko hatutaiepuka.

Na hatutapata viongozi wazuri watakaotutoa hapa tulipo. Watajitoa kwenye siasa ambazo zitawashushia heshima na hadhi yao au kushusha chini busara zao na maono yao. Watakaa pembeni wakiangalia taifa likiangamia kwa kukosa maarifa. Kinacholinda taifa sio polisi na wanajeshi wenye mabunduki ni maadili ya taifa na yanapobomonyoka ulinzi wa taifa hilo unakuwa bure. kwahiyo vijana wa taifa hili wanatakiwa kuangaliwa kwa karibu future ya taifa hili inategemea wana discipline kiasi gani. Bila discipline hakuna maono ya kitaifa yatakayofikiwa.

Kwa kiongozi mahusiano yake na jamii ni kitu muhimu sana kwake. Ni mtu mwenye maono si kwa ajili yake binafsi bali kwa jamii na taifa kwa ujumla. anatamani taifa lifikie level ya juu ya ukuaji wake. Lakini anatambua hawezi kufikia maono hayo bila watu.

Kwahiyo anatakiwa auze maono yake kwa watu. Yeye anaamini kwa watu. Anaamini watu ndio force kubwa sana ya maendeleo ya taifa. Na hata nguvu yake iko kwa watu. Bila kuaminiwa na watu, yeye na maono yake hawezi fanikiwa. Ni mtu mwenye mission sio yake bali ya taifa. kwahiyo hawezi kujitenga na watu au kujiweka juu yao. Anaua matabaka na kujenga umoja kwakuwa anajua hakuna mission ya any great value itakayofanikiwa pasipo umoja wa watu.

Na umaskini wa taifa hili utaondolewa na watu wenye dhamira moja na sio watu waliogawanyika katika ubinafsi ambao ni zao la ufisadi, choyo, wivu na kila aina ya takataka. Na haya yote na mengineyo hupelekea kutokuheshimiana na hata kuto kushirikiana kitu ambacho ni muhimu kwa maendeleo ya taifa '' mashirikiano'' Katika mazingira ambayo mmoja anataka kuwa juu ya mwingine tusitegemee mashirikiano. Taifa hili litaendelea ikiwa watu wakijitambua wao ni wamoja.
 
Back
Top Bottom