Kiongozi UVCCM akamatwa na bastola eneo la kupigia kura - Serengeti

Dec 11, 2010
3,321
6,327
Kiongozi wa uv-ccm amekamatwa akiwa na bastola kwenye kuto cha kupigia kura cha Butengi huko serengeti, amekamatwa na kina John Heche na amepelekwa kituo cha polisi.

Wakati huo huo vijana kadhaa wa chadema wamekamatwa na mkuu wa wilaya wa Bunda anaye kaimu wilaya ya serengeti na kupelekwa kusiko julikana, wamekamatwa na kupakiwa kwenye gari namba STK 3048 na gari nyingine toyota land cruiser namba T622BFJ.

Nitaendelea kuwajuza kadri ninavyo pokea updates kutoka kwa John Heche.

More updates kutoka kwa John Heche..

• "Vijana zaidi ya 30 wa chadema wametekwa na wamefungiwa kwenye ya ccm"

• "Pikipiki zetu 5 zimechukuliwa kinguvu na vijana wa green guard na wamezifungia pia kwenye moja ya vyumba kwenye ofisi ya ccm"

• Miongoni mwa majina ya vijana walio tekwa.

1. Barena Maro- Bwitengi
2. Samson Ogao- Rwamchanga
3. ADAM Samson- Bwitengi
4. Emanuel Eliya-Bwitengi
5. Onyango Otaro- Miseke
6. MAnginare Samson- Miseke
7. ELIJA Wilson-miseke
Mengine yanakuja.
8. Banage Nanai- Rwamchanga
9. Matororo Saina-Rwamchanga
10. Pikipiki simba- Rwamchanga
11. JOHN ONINGA-RWAMCHANGA
12. Richard christopher
13. Baraka nestory
14. Mwl makima
Peter john odao

• "Miongoni kuna kijana mmoja alifanikiwa kuwatoroka, wamechania nguo na kumnyang'anya kitambulisho chake cha kupigia kura"

• "Tumeenda kuwaomba Polisi wakatoe msaada ili vijana wetu watoke na kuja kushiriki kwenye zoezi la kupiga kura Polisi wamekataa"

•"Hizi ndio namba za magari yaliyo kuwa yanawateka vijana wa CHADEMA T 286 BFB, T545 BFE, zote Landcruiser za Ccm, na T.352 HAD.

• Zilikuwa zinaendesha Operation kukamata wafuasi wetu na kuwaficha kusikojulikana".

• " Nimeongea na kamanda Andengeye amekubali kupeleka vijana wake kwa ajili ya kwenda kuwa- rescue
vijana wetu wanao shikiliwa kwenye ofisi za ccm"

• "Polisi wamesha wachukua vijana wetu wapatao 100 walio kuwa wameshikiliwa kwenye ofisi ya ccm na sasa wanaandikiisha maelezo kwenye kituo cha polisi".

• "Cha kusikitisha hawa vijana hawezi kupiga kura tena maana muda wa kupiga kura umekwisha, hizi ni hujuma za wazi ili kuhakikisha hatushindi"

• "Vijana waliokuwa wametekwa na kupigwa baada ya kuhojiwa na Polis wamenyimwa PF3 na simu zao walizo nyang'anywa"

» Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
hivi ccm walizani watawala mpaka mwisho wa dunia hii nchi ni ya watanzania wote si ccm pekee kama wao wanavyo zani
 
Hapa tulipofika ni pabaya sana.

Ninaamini kabisa ya kuwa huyo aliyekamatwa na bastola akifikishwa polisi hatachukuliwa hatua yoyote. Hizi ni njama chafu na za kimafia za watawala kulazimisha wabaki madarakani kwa hali yoyote ile.

Wakati umefika kwa watanzania kwa jumla yetu tuanzishe mkakati wa nguvu wa kuwaondoa madarakani ccm. Tusingoje 2015, watatumia mpaka silaha ya sumu kuhakikisha wanaendelea kutawala!
 
Hali ya ccm ni mbaya sana kiasi kwamba wanalazimika kutumia vyombo vya dola kuhujumu zoezi la upigaji kura. Kimsingi hakuna matarajio ya ccm kushinda Machira pamoja na kutoa rushwa kwa kiwango kikubwa sana.

Huyo kiongozi wa UVCCM atakuwa ni mwenyekiti wao wa wilaya ndiye amekuwa akituhumiwa kuendesha vitendo vya kiharamia huko Serengeti.
 
mohamedi mtoi Kura zinalindwa? ama mkiwakamata hao wanaoruhusiwa kwenda na bastola maeneo ya uchaguzi mnawasindikiza mpk kituoni kisha kurejea lindoni? ama mnajigawa?
 
Watu siku hizi wameelimika wanakula ccm wanalala chadema,chadema watapeta sana kipindi hiki,haya ndio matunda ya mtu kujua ukweli wake
 
Ndio tabia za viongozi wa kiCCM. Mawazo yao yako kutoa uhai wa Watu tu.

Huo mchezo wa kutembea na bastola alianza Ole Sendeka, Kisha marehemu Ditopile, Aden Rage, Hilary Aeshi, Adam Malima, Ridhwan nk.
 
CCM hawana tofauti na Interahamwe, sasa nimegundua kwa nini Kikwete na Membe wanawatetea FDLR, kumbe lao moja. Wakati umefika kuanzisha move ya kwenda The Hague kushtaki huu uhalifu dhidi ya binadamu unaofanywa na CCM. Walikubali vipi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kama hawataki kushindwa??
 
kama alikuwa anaitumia kutishia wapiga kura atakuwa amejipa matatizo
 
Hayo ni matunda ya M4C watu wameamka na sasa hawataki kusikia CCM!!!
 
Kiongozi wa uv-ccm amekamatwa akiwa na bastola kwenye kuto cha kupigia kura cha Butengi huko serengeti, amekamatwa na kina John Heche na amepelekwa kituo cha polisi.

Wakati huo huo vijana kadhaa wa chadema wamekamatwa na mkuu wa wilaya wa Bunda anaye kaimu wilaya ya serengeti na kupelekwa kusiko julikana, wamekamatwa na kupakiwa kwenye gari namba STK 3048 na gari nyingine toyota land cruiser namba T622BFJ.

Nitaendelea kuwajuza kadri ninavyo pokea updates kutoka kwa John Heche.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.

mbona hutupi updates za Nassari na yeye kuwa Pistol hapo makuyuni, na kutishia kuua mwananchi mmoja hapo??? au pistol zinaruhusiwa kuwa na wanachadema peke yao?? be realistic my brro
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom