Kiongozi tunayemhitaji

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tunahitaji kiongozi ambaye sio mwenye makuu na mwenye kutaka sifa, Sio muonevu na asiyependa haki, bali atakayetawala kwa haki na usawa. Lakini pia asiye na tamaa ya kujilimbikizia mali. Kwasababu kiongozi anapokuwa na tamaa ya kujilimbikizia mali, ndio mwanzo wa kukandamiza haki za raia na kuwafanya raia watwana badala ya raia huru.

Na uhuru wa kweli watu wanaupata watakapoweza kujitawala wenyewe binafsi na kutenda matendo yaliyosahihi kwa kujizuia wasiibe, wasizini, wasifanye ufisadi na kutenda uovu mwingine wowote, ambao kwakweli ndio mambo haya yanayoleta disorder na kufanya jamii isifanye kazi inavyotakiwa, ama sivyo uhuru huo utaminywa kwa sheria na nguvu kutoka ndani na nje. Nguvu kutoka ndani adhabu dhidi ya nafsi yake kutoka kwa Mungu lakini nguvu kutoka nje adhabu kutoka katika taasisi ambayo imeundwa kutawala binadamu yaani serikali.

Tunajua fika bila kuzingatia misingi ya maadili na haki hakuna jamii itakayobaki.

Jamii za binadamu husimama na kuendelea pale misingi ya haki na ya kimaadili inaposimamiwa vyema. Na nguvu hii ya nje ni muhimu ili kurekebisha tabia za watu ziendane kama watu wanaofikiri sawa sawa na kuendana na jamii kwa kutendeana haki, na haki ndio huleta utengamavu.

Ndio maana tuna jela na polisi. Na vyombo hivi vinatakiwa kuwa vyenye maadili. Kwasababu watu wanaopaswa kuwafanya wengine wafuate sheria, wao wanapaswa kwanza kufuata sheria.

Na viongozi wanapaswa kutumia vyombo hivi kwa haki na busara na sio kuvitumia kama vyombo vya ukandamizaji.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa kiafrika wamejawa saana na ulafi,uroho,ubinafsi,uchu wa madaraka hata kujifanya wako juu ya sheria,.hawataki kukosolewa zaidi ya kuabudiwa na kutukuzwa,vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vya kuwalinda wao na sio Taifa na watu wake...kuna wakati nafikiri bora tungekuwa chini ya mtu mweupe tuu tukajua moja,.
 
Back
Top Bottom