SoC01 Kiongozi ni vema kuchunga Ulimi wake

Stories of Change - 2021 Competition

Noel Shao

Member
Jan 19, 2017
89
185
Utimamu wa kiongozi bora ni kuwa na kichwa chenye ubongo wa hekima, unaowaza, unoainisha, unaochambua, na kuweza kufanya tathimini. Vile vile ukamilifu wa kiongozi ni awe na kinywa chenye ulimi wa ufasaha, unaonena maneno ya staha, unaosema maneno ya uhakika, weledi na wenye kutoa nasaha bora.

Aghalabu vitu hivyo vikichagizwa na kifua kilicho na moyo wa wema, utu na busara, pasipo na shaka haki, umoja, upendo, amani vitatamalaki katika taifa.

Natanguliza haya ili kutoa rai kwa viongozi walio na nyazifa mbalimbali kutathimini lugha zinazotoka katika ndimi zao wawapo katika kutimiza wajibu na majukumu ya kila siku kwenye nafasi wanazo hudumu.

Kiongozi ni kiungo
Kiongozi ni mtu anayepaswa kuwa kiungo cha kuwaunganisha watu wa rika zote, katika umoja, urafiki, utu, upendo bila kujali itikadi ya vyama vya siasa, ukabila, tofauti ya uchumi, jinsia, na ukanda. Kwa hatua hii ndipo utulivu, na amani hujengwa na watu kuwa na wasaa wa kujikita katika shughuli za kujiletea maendeleo.

Kiongozi mwenye ulimi wa kusema lugha zinazo kusudia kuleta chuki, dhihaka, uadui, uchonganishi, uchochezi, uhasama wa kisiasa, kidini, kiuchumi, au kikabila ni kiongozi asiye tambua nafasi yake katika jamii anayepaswa kushauriwa namna ya kuutumia ulimi vema na si kazi jepesi kwa namna viongozi hasa walio hudumu katika nafasi za juu wanavyo pata ulinzi wa kikatiba .

Hazina bora na tunu ya Tanzania ni amani, hiki ndicho kilicho bora kuliko uchumi, na siasa zetu. Mengine yote yanabaki kama ziada ya haya.

Nazungumzia viongozi kwa kuwa ndio wenye wajibu wa mambo mengi nchini. Lugha za kutugawa hatutegemei zitolewe na kiongozi mwenye amana ya kuongoza umma. Maneno ya dhihaka, chuki au yasiyo tangaza umoja wetu tulioridhi yataligawa taifa vipande vipande.

Urithi wetu
Tangu enzi za muasisi wa taifa, Hayati Julius Nyerere aliweka juhudi za dhati kuhakikisha umoja wa kitaifa unakuwepo, ndio urithi wa kukumbukwa. Ikatokea siku ama kwa sababu yoyote kushindwa kuilinda na kuitunza amani tuliyo nayo basi hakika historia ya taifa hili itapotea.

Historia ni mwalimu mzuri wa kurejelea, mataifa mengi yaliyo chezea amani, yalijikuta yakiingia katika machafuko, ambayo hayakuwa suluhu ya matatizo yao bali yalivimbisha mioyo ya raia chuki na uhasama.

Hivyo, vipawa na karama za uongozi walizo pewa viongozi hawana budi kuvitawala kwa ufasaha, busara, utashi, hekima na weledi mkubwa. Wajikite kuheshimu utumishi kwa umma, utawala wa sheria na utawala bora.

Ubabe na matendo mabaya yapingwe, kwani kutoyakemea na kuyaacha yataja sababisha taharuki. Lazima viongozi wakumbushwe mipaka yao, wale wanaowazunguka viongozi wawe ndio msaada wa kutoa ushauri.

Tusibebe dhana kuwa siasa ni uadui. Kutofautiana kifikira, kimawazo ni sehemu ya demokrasia, na kutofautiana huko kusisababishe wengine wabebeshe gharama za demokrasia.

Wito wangu
Wito wangu ni viongozi kutambua wajibu wa kulinda amani, uhai na umoja wa taifa. Wakubali ushauri, na kukosolewa kwa lengo la kuboresha. Adui mkubwa wa amani ni pale tunapo ona viongozi hawatendi sawa na kuchagua kukaa kimya”

Nimeandika haya kwa kutopendezwa na kauli za viongozi wa taifa hili kwani iliwahi tokea huko nyumba Rais mmoja aliwaita wapinzani kuwa ni Wapumbavu na Malofa. Kamusi sanifu inatoa tasfiri kuwa mpumbavu ni sawa na juha, fala, mbumbu, na bwege. Huku neno “Lofa” Likiwa na maana ya mtu anaye zururazurura asiye na kitu wala kazi”.
Kiongozi mwingine aliwahi wadhihaki wananchi kuwa yeye ndiye kiongozi anayekula raha kuliko viongozi wote.

Na hivi karibuni wakati watanzania wengi wakilia juu ya makali ya tozo mpya za miamala ya simu, alinukuliwa waziri wa uchumi akisema wale wanaohoji kuhusu makato kuwa makubwa basi wahamie Burundi kwenye unafuu.

Kauli kama hii si ya kutia faraja, au kuleta suluhu bali kusiliba chumvi kwenye kidonda na haipaswi kutolewa na kiongozi wa umma tena waziri. Nachelea kusema ni dhihaka kwa umma ambalo wana haki ya kutoa maoni yao kwa viongozi walio wachagua tena kwenye mambo yanayo wahusu wao moja kwa moja kwa sababu ukweli ni kuwa tozo mpya za miamala ni mzigo wa msumari kwenye vichwa vyenye upara vya wananchi.

Kadhalika, kabla ya kumaliza siwezi acha kugusia tabia ya viongozi wa hasa wa jeshi la polisi jinsi wanavyo dili na viongozi wa vyama vingine vya upinzani kwa kauli za kutisha, kuwabakizia kesi nk.

Tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe
Binafsi sijapendezwa na ukamatwaji wa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe na viongozi wengi huku Mbowe akipewa kesi ya ugaidi, na kupanga njama za mauaji. Hii ni habari mbaya kwenye jicho la kidiplomasia na katika uongozi wa Rais SSH.

Aidha, wajibu ulio mbele ya viongozi ni kujenga utaifa, na kudumisha umoja. Ndimi za viongozi ziwe chemchem ya maneno yenye hekima na busara, ndani ya vifua vya viongozi ikae mioyo ya kupenda haki na amani, isiwe mioyo ya chuki, uadui, uhasama, na kuminya haki za wengine, mambo hayo hayajawahi kuwa chachu ya amani bali mbegu ya uharibifu.
 
Sio staha tu, kuna baadhi ya maneno huweza kuhadaa watu.

Leo hii tuko kwenye mkanganyiko wa chanjo nadhani ni sababu ya kauli za utawala uliopita.
 
Nilivyosoma na kuelewa nimeona kuwa kesi ya mbowe siyo ya juzi bali ni ya tangu mwaka jana hata kabla ya uchaguzi. Alipogundua kuwa alikuwa anatafutwa kwa kesi hiyo, mara tu baada ya uchaguzi akakimbilia Dubai hadi pale Magufuli alipofariki akiamini kesi nayo itakuwa imekufa na Magufuli ndipo akarudi Tanzania.
Siyo kweli.. Mbowe alikuwa na kesi ya kuitisha maandamano yeye pamoja ba watu wengine ikiwemo aliyekuwa Mayor wa Ubungo Boniface Jacob, kilichofanyika ni kuwa walipewa ruhusa na jeshi la polisi kusafiri huku wengine wakiendelea kuripot polisi . Hivyo watu waache siasa
 
Tuhuma za ugaidi dhidi ya Mbowe
Binafsi sijapendezwa na ukamatwaji wa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe na viongozi wengi huku Mbowe akipewa kesi ya ugaidi, na kupanga njama za mauaji. Hii ni habari mbaya kwenye jicho la kidiplomasia na katika uongozi wa Rais SSH.
Mada yako ni mzuri Sana Ila ulipofika hapa umeenda katika ushabiki wa upande wako wa unaoupenda ,hii dhana kuwa ukiwa upinzani ni Malaika ,fanya yote lakini usiguswe katika dhambi zako,kisa siasa
 
Mkuu hoja zako zina logic.. ila chanzo cha ubadhirifu siyo kwenye halimashauri na mikoani, hapana izi hela zina pigwa juu na mapapa hawa wengine wanakula kiasi kdogo sana....
Futulia bajeti na matumizi ya ndani utakuta kinachosemwa na kilichopo hazina, uhusiano wala uhalisia yoyote ...
sitaki kuamini kwamba hawa wakurugezi wanakula hela kwenye halimashauri zetu.. kwa kiwango hicho ..
Namna bora ya kufanya hapa ni kila mkoa iwe na bajeti yake na vya mapato kwa ufasaha then serikali kuu isimamie miradi mikubwa za kitaifa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, ila nimesoma summary iliyotolewa na vyombo vya habari tu. Hata hivyo jambo ninaloongelea ni kwamba "hakubambikizwa"kesi na SSH, bali ni kesi ya tangu mwaka jana.

Wale masheikh wa UAMSHO aliowaachia kesi yao ilikuwa ya lini? Je alipotoa amri ya kuachiwa kwao alikuwa anaingilia uhuru wa mahakama?
 
Back
Top Bottom