Kiongozi mwenye balaa na mikosi anapoongoza balaa na mikosi!

Aug 18, 2010
65
22
...Uongozi ni uoni wenye muelekeo wa utendaji wenye saada na si kuona kibubusa! Kiongozi ni yule anayeona shida, taabu na dhiki za watu wake kisha akatumia falsafa ya tatizo-tatuzi-tatuo na kupata suluhu ya matatizo ya watu wake na si kujilaumu. Kiongozi mwenye mikosi na balaa huzusha shida na balaa kwa watu wake na yeye (kiongozi) hajijui kama ana balaa! Hii ni hatari ya kiongozi mwenye balaa na mikosi kwa kuwa wanaoongozwa hubeba balaa na mikosi ya kiongozi na kuiingiza kwenye mfumo wa maisha yao kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Uongozi si laana; ni neema kwa mtu mweledi anayejuwa hali za watu wake na shida zao. Uongozi ni kuonyesha njia yenye saada, tija na ufanisi wa utumizi mzuri wa rasilimali kwa maendeleo ya watu kwa uwiano sawiya. Kiongozi shujaa ni yule anayekubali kufa kwa haki juu ya kuwatumikia watu ilhali yeye (kiongozi) akitaabika. Kiongozi mwema ni yule asiyependa utajiri wa watu wengine na kuwakaribisha kwenye uwekezaji wa kiwendawazimu na au wa kijambazi. Kiongozi mwema hawezi kuwa tapeli wa kisiasa; na zaidi kiongozi mwema hawezi kuwa mnafiki - anayeahidi maisha bora huku watu wake wakitaabika na msoto wa kupigika na maisha.

Balaa la kiongozi, mikosi yake na jinsi anavyoogopa hata kivuli na au giza la usiku ndiye anayeongoza mikosi na balaa kwa watu na kuongoza kwa nguvu za kishirikina na au kichawi - analindwa na "majini." Kiongozi mwenye kuamini nguvu za kishirikina kwenye kuongoza hawezi kuleta saada ya maendeleo ya watu. Hii ni balaa na ni mikosi kwa taifa....tafakari chukua hatua!
 
Back
Top Bottom