Kiongozi Msafi wa Africa na Aseme - Mugabe

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
195
Kulinga na taharifa ya habari ya BBC leo asubuhi, kiongozi wa alijitangazia ushindi katika kura ambayo imekuwa ni aibu kwa africa Robert Mugabe amesema kiongozi yeyote aliye msafi africa na amwambie kuwa hajashinda kihalali ili na yeye amuulize kwake yeye alishinda kihalali au alishinda kwa njia gani.

Alisema maneno hayo jana baada ya kuapishwa kuwa raisi wa zimbabwe kwa kipindi kingine kwa madai ya ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa upande mmoja baada ya mpinzani wake Morgan shivangarai kujitoa kwa madai ya serikali na vikundi vya siri vya raisi Mugabe kushambulia watu wanaosuport upinzani.
 
huyu babu dikteta anaelewa anachokizungumza. miaka 50 baada ya uhuru bara la Afrika bado linasuasua kimaendeleo.tatizo kubwa uongozi mbovu! hapa kunahitajika mjadala na waafrika waache unafiki wa kuzungumza mambo yasiyo na maslahi na nchi. mbona wazee wetu walituonyesha njia? akina mwl Nyerere.Kwame,Sekotoure na wengineo. ubinafsi wa viongozi na ukondoo wa wananchi unaiua Africa.
 
Babu kawabana...Wanayajua ya KIKWETE NA WENZAO!
KIKWETE...SASA KAMATA MAFISADI KABLA HATA MUGABE HAJAKUTOA NISHAI!
 
huyu babu dikteta anaelewa anachokizungumza. miaka 50 baada ya uhuru bara la Afrika bado linasuasua kimaendeleo.tatizo kubwa uongozi mbovu! hapa kunahitajika mjadala na waafrika waache unafiki wa kuzungumza mambo yasiyo na maslahi na nchi. mbona wazee wetu walituonyesha njia? akina mwl Nyerere.Kwame,Sekotoure na wengineo. ubinafsi wa viongozi na ukondoo wa wananchi unaiua Africa.

.....soon case yake against Ndebele 1982 itasomwa The Hague na arrest warrant itakuwa issued.
 
penye ukweli na pasemeke.tumemsema Mugabe mno no kiweli njia aliyojipatia ushindi siyo ya kihalali lakini ni nani Afrika ameingia fairly?Umwagaji damu mwingi na wizi wa kupindukia.Penye ukweli uongo hujitenga.
 
Ukweli Utajitenga huko BONGO!
STARTING WITH DODOMA KESHO!
MSIKATE MATANGAZO ya hotuba TAFADHALI!
 
Mwacheni mzee wa watu afanye kazi zake kwa amani. Bado anaonyesha ujasiri wa kweli, hana unafiki kama akina kikwete vibaraka wakubwa wa us na uk. Tunawataka Bush na Brown wamkome babu yetu kipenzi cha waafirika halisi.

Tunamuomba mwenyezi Mungu amjalie afya njema babu yetu ili awape fundisho akina kikwete!
 
penye ukweli na pasemeke.tumemsema Mugabe mno no kiweli njia aliyojipatia ushindi siyo ya kihalali lakini ni nani Afrika ameingia fairly?Umwagaji damu mwingi na wizi wa kupindukia.Penye ukweli uongo hujitenga.

Watapiga makelele watachoka kwani Mungu yuko upande wa mzee wetu Mugabe.
 
Maths Yukwapi?
Maana Naona Formula Ya Afrika Ya Mahesabu Ya Wembe Mkali Na Nasaba Za Kunguru Mweupe Na Jmushi!
 
Huyu mzee anajua viongozi wote wa Africa hakuna aliyeingia kwa ridhaa ya wananchi ndo maana anawambia msafi na aseme, ndo maana nimesema kama waliandaa agenda inayohusu zimbabwe hawataiongea kwani wote wanajua hakuna hata mmoja atayeweza kusimama mbele ya mzee na kumweleza kuwa amefanya makosa wakati yeye yakwakwe bado yanalindima.
 
Yanalindima Na Kuyamaliza Hawataki!
Wao Wamekalia Zimbabwe...na Sasa Ni Wangwe Na Mbowe.
 
Huyu mzee anajua viongozi wote wa Africa hakuna aliyeingia kwa ridhaa ya wananchi ndo maana anawambia msafi na aseme, ndo maana nimesema kama waliandaa agenda inayohusu zimbabwe hawataiongea kwani wote wanajua hakuna hata mmoja atayeweza kusimama mbele ya mzee na kumweleza kuwa amefanya makosa wakati yeye yakwakwe bado yanalindima.[/QUOTE]


Na kama hii ni kweli its sad for our continet.
 
Na ndo mana wanajizungusha kumbana maana wanajua atawatoa nishai, tena kuanzia na huyo mkuu wao wa umoja wa africa hana tofauti na Mugabe mwnyw kabsaaa..
 
Huko nyuma alimwambia Bush kuwa naye asiseme chochote,akamwambia kama anataka kusema kwanza naye aseme kama kweli alimshinda Gore kihalali.
 
Mnajua vyombo vya magharibi vikishupalia kitu basii unaonekana hufai kabisa.
Mbona Mseven dikteta hawamsemi?Na kila mtu analijua hilo kwa vile anakula wamagharibi basi shwali.
Kwa vile Mugabe amekataa kuwanyenyekea wazungu leo hii anaonekana hafai.
Mwenye akili timamu na anayejua maana ya Ukoloni atajua ni nini Mugabe anapigania na anaelewa vizuri vile mataifa ya hulo Ulaya kwa nini yanamshambulia Mugabe.
Mimi sishangai kwani walisha sema kuwa SADDAM anamiliki nuclear kwenda kule hola lakini kuna kitu walicho kuwa wanakitafuta ndo wanacho neemeka nacho sasa hivi.
Mugabe kwa kweli si mnafiki kama viongozi wetu wa hapa BONGO na kungineko Afrika.
 
Huyu Mzee kaisha wapiga bao la kisigino. Nafikiri mwenyekiti wa AU akiinua mdomo tu Mugabe atakuja na hoja ya Zanzibar, halafu tuone majibu yatakuwa vipi!

Kama ni kupeleka jeshi kwa wanaoingia kwa nguvu naona ni wengi tu.
 
Mugabe tatizo sio kuingia madarakani kihalali, tatizo ni wewe hauko tayari kutoa tax holiday kwa 'wawekezaji', tatizo lako hauko tayari kuingia mikataba ya Buzwagi, tatizo lako hauko tayari kutengenezewa marafiki wa dizaini ya Sinclair, tatizo lako hauko tayari kuruhsu mapesa ya EPA kuwekezwa kwenye mabenki ya 'wafadhili', tatizo lako hauko tayari kumwakikishia mkoloni access ya ulaji kama madikteta wenzio wanavyofanya. Rudi nyuma anza kugawa ardhi, machimbo ya madini na mashirika kwa 'wawekezaji' harafu usikie kama kutakuwa na kelele za human rights au democracy.
 
Back
Top Bottom