Kiongozi Mbio za Mwenge kitaifa.

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
7,587
12,114
Wadau heshima kwenu wote.
Nilipokuwa mdogo na hata wakati nasoma sekondari,nilipata kusikia kuwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa huwa hawaishi muda mrefu,mara baada ya kumaliza kukimbiza mwenge,niliambiwa huishi si zaidi ya miaka mitano tokea awe kiongozi wa mbio za mwenge.

Wakaendelea kudai ile kazi ni ya kuchosha mwili na akili,japokuwa malipo yake huwa ni makubwa.
Leo nikasema ngoja niwaulize wajuzi wa mambo walioko JF,je hiyo dhana nilihadithiwa zamani ina ukweli wowote?
Ningefurahi pia kupata listi ya wakimbiza mwenge wa uhuru tokea 2005-2015 ambao bado wako hai kama reference.

Ramadhani Kareem!
 
Nadhani mkuu wa mkoa wa dodoma bwana Rugimbana nae alishawahi kukimbiza mwenge,ckumbuki mwaka aliokimbiza mwenge
 
Lengo langu ni kujua wale viongozi wakimbiza mwenge kitaifa,sio kiwilaya au kimkoa.
Bado nasubiri wajuzi wa historia tafadhali.
 
Na ndio maana nikakwambia wapo wengi sana waliokimbiza mwenge na bado wapo hai hadi leo,mmojawapo mheshimiwa rugimbana,na kuna mmoja namkumbuka alikuwaga askari magereza nae yupo hai hadi leo mbona
 
Wadau heshima kwenu wote.
Nilipokuwa mdogo na hata wakati nasoma sekondari,nilipata kusikia kuwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa huwa hawaishi muda mrefu,mara baada ya kumaliza kukimbiza mwenge,niliambiwa huishi si zaidi ya miaka mitano tokea awe kiongozi wa mbio za mwenge.

Wakaendelea kudai ile kazi ni ya kuchosha mwili na akili,japokuwa malipo yake huwa ni makubwa.
Leo nikasema ngoja niwaulize wajuzi wa mambo walioko JF,je hiyo dhana nilihadithiwa zamani ina ukweli wowote?
Ningefurahi pia kupata listi ya wakimbiza mwenge wa uhuru tokea 2005-2015 ambao bado wako hai kama reference.

Ramadhani Kareem!
Jordan Rugimbana ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa dodoma alikuwa ni kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa kati ya mwaka 2000 au 2002 kama sijakosea sababu nakumbuka nilikuwa mdogo na ninakumbuka moja ya nyimbo ambazo walikuwa wakimuimbia.... ukipiga hesabu hata hiyo 2002 tu hadi leo ni miaka 15 na jamaa bado anadunda... Hivyo sidhani kama hicho kina ukweli wowote japo hata mm nimewahi kukisikia
 
Capt mwanosya alikuwa kiongozi wa mbio za mwenge 2010 - 2015 sina uhakika wa mwaka bado yupo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom