Kiongozi hapaswi kuwa mtu wa kulialia—Lowassa

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumapili, Septemba 02, 2012 07:46 Na Eliya Mbonea, Monduli

lowassa%20edward.jpg
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

MBUNGE WA Jimbo la Monduli, Edward Lowassa amesema kiongozi anayeaminiwa na wananchi wake hapaswi kuwa mtu wa kulialia na kuomba msaada badala yake anatakiwa kufikiri na kutoa uamuzi wa maisha ya watu wake. Lowassa ambaye pia ni Laigwanani Mkuu wa Wamaasai alisema hayo jana kwenye mkutano wa siku mbili uliowakutanisha Malaigwanani kutoka nchi nzima kujadili tatizo la ardhi, Katiba Mpya na suala la elimu kwa jamii hiyo.

“Malaigwanani si viongozi wa kulialia, kuombaomba msaada ni watu wa kufikiri na kusema tumechoka na hali na sasa tunaamua kufanya jambo moja, mbili na tatu hatuwezi kuvumilia kuona watu wetu wakiendelea kuumia kila siku wakati sisi ndio viongozi wao, sisi siyo watu wa kulialia,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Lazima leo tuseme kauli ya kuwasaidia wenzetu wa Ngorongoro hakuna kiongozi wa Kimasaai aliyeaminiwa kufanya kazi kisha akawa analialia na kuomba msaada. Ardhi kwa Ngorongoro imekuwa tatizo kubwa nataka leo hapa tulizungumze kwa dhati.

“Tumechoka kusikia migogoro ya ardhi, leo naomba tusaidiane tuseme wenyewe hapa tufanye nini,” alisema Lowassa.

Akieleza maeneo mengine yenye migogoro kwa wafugaji hao, Lowassa aliutaja Mkoa wa Morogoro na kuwataka viongozi wa kimila waliotoka mkoani humo kubainisha wazi nini cha kufanya ili kumaliza migogoro hiyo ya mara kwa mara.

“Tutampata pia mtu atakayezungumza habari ya Morogoro kwa vile napo kuna migogoro mingi ya ardhi nataka leo tuzungumze kwa mapana kuhusu ardhi ya Morogoro kuna tatizo gani na tufanya nini siyo kulialia.

“Wananchi wametuahidi, wametuamini, wametuchagua, wametuteua, wanatuheshimu na wanatupa mifugo yao ili tufanye kazi zao, sasa lazima tufanye kazi tusilalamike,” alisema Lowassa.

Akizungumza kuhusu kutoa maoni mbele ya Tume ya Katiba Mpya iliyopo chini ya Jaji Joseph Warioba, Lowassa aliwataka Malaigwanani hao kuwa msatari wa mbele katika kutoa maoni yatakayokuwa na msaada kwao na kizazi cha baadaye cha wafugaji.

Alisema katika mchakato wa kutoa maoni unaoendelea hivi sasa Malaigwanani wanapaswa kuangalia wanatakiwa kufanya nini ili wawe kwenye Katiba na watambulike kama viongozi halali wa kimila.
 
Hilo dongo linaenda kwa nani. Maana sidhani kama linaishia hapo hapo kwa malagwanani
 
yaani huyu kamchoka swaiba wake anapiga vijembe vilivyotulia sasa subiri swaiba wake alivyo navilipizi kama hata fanya cha ajabu juu yake
 
haha na mie na pita tu sasa na wale jamaa zangu wa ukanda wa pwani na wanao tegemea maisha yao kwa uvuvi katika ukanda huo ambako maeneo yao ya dago yameuzwa kwa wawekezaji inabidi waombe katiba mpya iwalinde ,ila nataka kusema tu viongozi wetu tupendekeze katiba ituweke pamoja na sio kututenganisha .masuala ya ardhi ni vyema yakazingatiwa na serikali kwa sheria za nchi kama hazipo ziwekwe. mabishano ya matumizi ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima ndio hadi leo darfur kuna matatizo sasa suala kubwa ni kuwa ardhi ni ya nchi (serikali )au inataka kupendekezwa iwe ya kabila fulani kwani sasa vijiji ndio vyenye sehemu kubwa ya ardhi .nnogopa kweli hili ni vyema likazungumzwa kwa kuangalia maendeleo ya kisasa ya uchhumi
 
Inawezekana anamlenga Mzee 6 maana na yeye alishawahi kulia Bungeni live..
 
...Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaa kulia lia, omba omba na U VDG yaani kathibitisha Dhaifu na jamaa yakePM wote viazi.... lol

Hilo dongo linaenda kwa nani. Maana sidhani kama linaishia hapo hapo kwa malagwanani
 
Hilo dongo linaenda kwa nani. Maana sidhani kama linaishia hapo hapo kwa malagwanani

Hilo ni indirect dongo kwa swahiba wake kwenye issue ya ziwa nyasa. Amezidi kulialia mno harafu utendaji ni 0, tena kwenye issue ya ziwa nyasa analizwa na mwanamke. Lol
 
Ni kweli nchi hii,wanachi wanalalamika,wabunge wanalalamika,mawaziri wanalalamika,watu muhimu kama Madaktari wanalalamika, wanataka mshahara na posho kwapamoja iwe 7500,000 yani Dr.wa mwaka wakwanza,watumishi wengi zaidi ya wote yani Waalimu wanalamika,Rais wakati mungine analalamika,inatubidi tumpate mtu wa kutupelekeleka mchakamchaka.LOWASA TULIONA MZIKI WAKE WA UWAZIRI MKUU.
 
linaenda kwa kikwete, hatutakiwi kuwa waoga, kauli hii ilitakiwa itoke kwa rais wa malawi na si kikwete.
 
Amesema kweli hata km ukweli unauma dhaifu kazi yake ni kulialia tu ,mifano ipo mingi huwa anawakimbia wahusika na kwenda kulialia kwa wengine ili wamsaidie kutatua matatizo,refer mgogoro wa madaktari na tucta alienda kulia kwa wazee wa dar
 
Back
Top Bottom