Kiongozi gani amewahi kutembelea maktaba na je Serikali inazijali?

Mzee Mwanakijii,

Mimi hapa, tena nna maktaba yangu nyumbani na kwenye kompyuta zangu, nna maktaba zilizosheheni vitabu, picha na vijarida vya kila aina. Na nnazitembelea kila siku kutwa kutwa X 10 +.

Au wewe sio kiongozi? na kwanini sio kiongozi?
 
Huko hawana habari nako mkuu!!! Achana na maktaba ya taifa au za mikioa;


MMM tunaomba uombe attendance ya Wabunge kwenye maktaba ya bunge!!! nadhani tutaangusha kilio hapa!
 
Nakumbuka kila Jumamosi walikuwa wanaonesha Cinema Nazokumbuka ni ile ya Watoto Saba na Mfalme Kima ilikuwa raha si Mchezo...

Palikuwa na Huduma ya Maji ya Kunywa Baridi Bure kutoka kwenye Water Dispeser Vitabu vilikuwa Vingi unakuwa na kadi zako tatu na J hizo kadi ni za kuazimia vitabu...
 
Ni kweli ni hulka na tabia ambayo unaijenga mwishoni inakuwa hobby!!kila mmoja wetu aweke lengo dogo tu kusoma vitabu 3 kila mwezi itasaidia sana kuongeza maarifa
 
Mi nimewahi kujisomea katika makitaba za mikoa ya Morogoro, Tabora na Shinyanga na ya wilaya ya Masasi. Katika hizi maktaba kidogo maktaba za Moro na Tabora zinahuduma bora na vitabu current na vinasaidia sana watumiaji hasa wanafunzi. Lakini Shinyanga nilitumia karibu miezi miwili ninaulizia maktaba watu hawajui kama kuna kitu hicho mpaka nikafanikiwa nilipojiunga na kuanza kuitumia ni kwamba madhari sio nzuri mahudhurio ya watu ni ndogo mno sana sana utakuta watoto tu. Nilijaribu kumuuliza mhudumu akaniambia uwepo wa wanachama wachache unawapunguzia kazi, nikaomba kitabu chenye historia ya Tanganyika sikupata na ukienda kutafuta vitabu kwenye mashelf jiandae kupata mafua na jengo ni la zamani mno hali inasikitisha. Vitabu vya waandishi wakitanzania ndo hamna kabisa unakuta vichache vya miaka ya 70s &80s inaonesha labda hatuna mwamko wa kuandika na kununua vitabu vyetu wenyewe. Ila kama tutakuwa na miradi ya kukuza utamaduni wa kujisomea tunaweza tukawa wasomaji wazuri kwa kuwa na maktaba kila kata, na kukuza soko la vitabu vya waandishi wakitanzania.
 
MZEE MWANAKIJIJI ACHA UCHOKOZI KWA VIONGOZI WETU KWENDA KUJISOMEA MAKTABA, UNATAKA WAONEKANE WATU WA KAWAIDA MKUU?

Huo sasa ni uchokozi dhahiri na wewe Mzee Mwanakijiji kwa viongozi wetu waliowengi nchini.

Kweli kabisa unadiriki kuuliza swali kama hilo wakati unajua hata kule ofisini hawawezi kusoma japo kurasa moja tu ya mafaili matatu kwa siku mpaka mtu anayetoka huko Shinyanga kuja kufuatilia jambo dogo tu Dar es Salaam anafika mahali anaanza kugombana na ndugu kwa kugeuza nyumba zao makazi yake ya kudumu kwa kusubiri tu faili isomwe kisha tutiwa sahihi sehemu ndogo tu!!

Kwa kweli uchokozi wa aina hii sijaipenda. Wafanyakazi wetu kazi hufanya tu kwa mazoea na hata wale walioingia kazini miaka kumi wakiwa na digri zao mpaka sasa ni weupe tu kama wanafunzi wa shule za msingi; kazi kunyunyizia tu viingereza viwili vitatu na ukali debe kuonyesha wamesoma kumbe hamna kitu.

Maktaba zenyewe unazozisemea, nani mwenye akili zake aende huko kwenda kutafuta ugonjwa wa TB kwenye vitabu kuu kuu vilivyojaa vumbi tele. Waulize wanafunzi wa shule za msingi amba ndio siku hizi wanajazana huko kwenda kushangaa mi-picha na eleo pekee lenye ukimya kote katika miji mbali mbali nchini; watakuthibitishia kwamba vitabu ambvyo ni vipya zaidi za mwaka 2000 kurudi nyuma, sasa hapo bado kuna hai tena hapo?

Labda Makamu wa Rais Dr Bilal atuambie kwamba bajeti za Maktaba zeti (si bajeti kwa ajili ya utawala, posho na kongamano) nchini kwa ajili ya kazi moja tu kununulia vitabu vipya imekua ni shilingi ngapi kila mwaka wa fedha? Sana sana, japo inasikitisha sana lakini ndio ukweli wa mambo yalivyo, maktaba zetu kote nchi yamebakia tu na uzuri wa majengo ya enzi za Mwalimu Nyerere bila kukarabatiwa ila mle ndani nakuambia KUMEGEUZWA DEMPO taka taka za miaka kadhaa iliopita ambayo wenzetu huko Ulaya hawahitaji tena kwenye maktaba zao ndio tunakingia bakuli kama msaada!!

Bure kabisa na wala hakuna kitu pale kwenye hiyo orodha ndefu ya maktaba zetu. Mzee Mwanakijiji na wana JF wote, kherini hivo hivo ya Krismasi na mwaka mpya hata kama wengine mnadai kukopwa sehemu ya mishahara yenu bila ruksa!!
 
Kila anaekuja hapa anasema kuwa yeye alizoeshwa alipokuwa mdogo na sasa hivi ni mzuri wa kusoma vitabu. Kwa nini huo utamaduni hamkuwarithisha watoto na wadogo zenu?

Wangapi leo hii wanawapeleka watoto wao maktaba wikiendi? Ni kweli kuwa jumla kuu ya Watanzania hawana uwezo wa kununua vitabu vingi kwa watoto wao au vijana wao majumbani, lakini hata hao wenye uwezo hawafanyi hivyo. Tumejiuliza kwa nini?
 
Tunapozungumzia tatizo kubwa la kutokuwa na library au kujali umuhimu wa library tz lazima tuanze kwanza kwa kweli kukubali kuwa utamaduni wa kujisomea tz umekufa au kupungua kwa kiasi kikubwa na hii inajitokeza (kama dalili) pale tunapoona hata viongozi hawajali tena umuhimu wa library.....si tu kwenye mashule na vyuo vyetu bali hata kwenye mikoa na wilaya zetu.Tatizo hili kwa kweli ni la kijamii zaidi.......yaani jamii ya mtanzania kuanzia manyumbani....................hamna utamaduni wa family kujisomea.......ambapo watoto kwa kujifunza kwa wazazi wanaweza kujisomea......tunachoona ni kukua kwa utamaduni wa kuangalia tv tena kwa programme za kijingajinga zisizojenga...e.g comedies etc..........watoto wanasoma wakati wanapotakiwa kujiandaa na mitihani tu (kama ambavyo wazazi nao walitumia library za vyuo kusomea mitihani tu).....yaani hili ni tatizo kubwa la kijamii tz..............nina uhakika hata kama kungekuwa na library nchi nzima ktk kila halmashauri....hakutajaa watu library.....watu wasio na utamaduni wa kujisomea........hata kama kuna library hawatasoma..............wanafunzi nchi hii wanaenda library pale wanapokuwa na mitihani tu.........hizi internet hata kama zingekuwepo everywhere........matumizi yake katika jamii ya mtanzania si kujitaftia maarifa bali ni sehemu ya intertainment......watu wanachat tu....na kucheza games (wanafunzi wanatumia pale tu inapowabidi kitaaluma)hamna kitu kingine.......na haijalishi umri....watoto kwa watu wazima nchi hii wamepoteza utamaduni wa kujitaftia maarifa kwa njia ya kujisomea viwe vitabu au electronic media(e.g internet).......tatizo hili ni pana kuliko tunavyoliona.....wameathirika watanzania wooote .....hata viongozi....ndio sababu taifa linajikuta lina watu wanaopenda short cuts tu.......mfano....watu wanasaini mikataba hovyohovyo tu..bila kuwa na in depth knowledge ya subject matter......mitihani inaibwa hovyohovyo(vile watoto hawasomi)....mifano iko mingi.........sijui nisemeje.....mtu mweusi(mwafrika)anaonekana kuathirika sana na tatizo la kutokujitaftia maarifa kwa njia ya kujisomea......kwa wale mliokaa nje ya nchi(i hope Mzee Mwanakijiji pia)....ebu jiulizeni kwenye hizo library zilizopo kila kona ya nchi kwa wenzetu......je ni watu weusi wangapi mnawaona wakijisomea.?(i mean kwa kuwalinganisha na watu weupe)......nadhani mtagundua ni weusi wachache saaana wanaosoma at free will and time.........
 
Hili suala la maktaba tuliangalie kwa jicho la tatu kama Watanzania na tofauti za kisiasa tuziweke kando. Naomba serikali iongeze nguvu kwenye library za mikoa na wilaya ikiwezekana kila shule iwe na maktaba yake. Tumeweza maabara na madawati hata maktaba tunaweza kama tukiamua.
 
Swali la msingi ni kwa nini watu wanasoma vitabu au majarida? Kama ni kupata habari au information, ni kwa nini wanahitaji hizo taarifa na habari? Je, hakuna njia nyingine za kupata hizo taarifa na habari? Kama zipo, je sio kuwa hizo njia nyingine zinapewa priority wakati mhusika anataka kupata hizo habari na taarifa? Je, kuna njia bora ya kupata habari au taarifa ile ile kulinganisha na nyingine?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom