Kiongozi gani amewahi kutembelea maktaba na je Serikali inazijali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi gani amewahi kutembelea maktaba na je Serikali inazijali?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 1, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nafikiria fikiria hapa kuona ni kiongozi gani amewahi kuonesha umuhimu wa maktaba kwa watoto wetu vijana na hata watu wazima. NI watu wazima wangapi ambao wanatembelea maktaba? Ukiondoa maktaba za balozi mbalimbali je jiji la Dar lina maktaba za kutosha na zenye hadhi ya kutosha?

  Kwanini kila halmashauri nchini isitakiwe kwa lazima kuwa na maktaba yake ambayo inawekewa kiwango cha chini cha uwepo wa vitabu, kompyuta, nafasi n.k?

  Hili wazo limenijia baada ya kufikiria ahadi ya Rais kujenga maabara katika kila shule na kila mwanafunzi wa sekondari kupata kompyuta shuleni hapo - nadhani hili la pili alikosea ulimi tu maana sidhani hata nchi zilizoendelea zimewahi kufanikiwa katika hilo.

  HIZI NDIZO MAKTABA ZA MIKOA (Mikoa 18 ina maktaba kati ya 27)

  National Central Library, Dar es salaam

  Head Quarter
  National Central Library, Dar es salaam
  Bibi Titi Mohamed Road,
  P. O. Box 9283, Dar es Salaam
  Tel.: (255) 022-2150048/9
  E-mail: (JavaScript…
  Arusha

  Arusha
  Uhuru / Sokoine street,
  P.O. Box 1273 Arusha,
  Tel: (255) 027-252642
  E-mail: (JavaScript must be enabled to view this email address)
  Dodoma

  Dodoma
  Dar es salaam road,
  P.O. Box 1900, Dodoma
  Tel.:

  Iringa
  Uhuru Street,
  P.O. Box 172, Iringa
  Tel.: (255) 026-2702421

  Kigoma
  Lumumba Road,
  P.O. Box 933, Kigoma
  Tel.: (255) 028-2803168
  Kagera

  Kagera
  P.O. Box 321, Kagera,
  Tel.:(255) 028-2220460
  Lindi

  Lindi
  P.O. Box 443, Lindi
  Tel.: (255) 023-2202156

  Mara
  Jamat Khana Street,
  P.O. Box 874, Musoma
  Tel.: (255) 028-2622183
  Kilimanjaro

  Kilimanjaro
  Kibo Road,
  P.O. Box 863, Moshi
  Tel.: (255) 027-275432
  Morogoro

  Morogoro
  Old Dar es salaam Road,
  P.O. Box 858, Morogoro
  Tel.: (255) 023-2602160
  Mtwara

  Mtwara
  Uhuru Street,
  P.O. Box 37, Mtwara
  Tel.: (255) 023-2333352
  Mbeya

  Mbeya
  Maktaba Street, P.O. Box 842, Mbeya
  Tel.: (255) 025-2502589

  Mwanza
  Station Road,
  P.O. Box 1363, Mwanza
  Tel.: (255) 028-41895
  Rukwa

  Rukwa
  Msakila Road
  P.O. Box , Sumbawanga
  Tel.: (255) 025-282259
  Ruvuma

  Ruvuma
  Sokoine Road,
  P. O. Box 929, Songea
  Tel.: (255) 025-2602041
  Shinyanga

  Shinyanga
  P.O. Box 804, Shinyanga
  Tabora

  Tabora
  Lumumba Street,
  P.O. Box 432, Tabora
  Tel.: (255) 026-6099
  Tanga

  Tanga
  Uhuru Street,
  P.O. Box 5000, Tanga
  Tel.: (255) 027-2643127

  Na hizi ni MAKTABA ZA WILAYA (11 kati ya wilaya 127)

  Biharamuro

  Biharamuro
  P.O. Box 146,
  Tel.: (255) 023-2623047
  Bagamoyo

  Bagamoyo
  P.O. Box 287, Bagamoyo
  Tel.: (255) 02440427
  Kilosa

  Kilosa
  P.O. Box 146, Kilosa
  Tel.: (255) 023-2623047

  Kwimba
  P.O. Box 25, Ngudu
  Lushoto

  Lushoto
  P.O. Box 240, Lushoto
  Makete

  Makete
  P.O. Box 10, Makete
  Mbozi

  Mbozi
  P.O. Box 227, Mbozi
  Tel.:(255) 025 2580088
  Mufindi

  Mufindi
  P.O. Box 223, Mufindi
  Njombe

  Njombe
  P.O. Box 179,
  Tel.: (255) 026 2782135
  Pangani

  Pangani
  P. O. Box 31, Pangani
  Tunduru

  Tunduru
  P. O. Box 40, Tunduru


  Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu Maktaba zenu: http://www.tlsb.co.tz
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mwanakijiji hebu pumzika na habari za siasa kwanza.......
  ukiendelea hivi utadhurika afya.......
  unachokifanya sometimes ni kama kuwapigia mbuzi gitaa.....
  viongozi,viongozi.......viongozi wepi???????
  hivi tunaweza sema tuna viongozi?????????
   
 3. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Dar es salaam yenye wakazi wanaofikia milioni 5 ina maktaba moja tu...tena ni ya mwaka 47 tangu tunasoma vidudu mpaka sasa hivi! Huu ni utani kwa kweli!
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj sijui umekumbukaje hii na kuilink na hiyo mipango mipya ya serikali ya ujenzi wa maabaraz? Bongo kweli tuna matatizo tena ya kujitakia!!!!!!!!!

  Well I am not sure kama maktaba zinahusiana na serikali za mitaa. Lakini jengo la maktaba Mbeya ni dogo kuliko Mkapa hall iliyojengwa juzi juzi na ambayo mainly hutumika siku za wikiendi. Jengo lile ni dogo kuliko Nyumba mpya ya mkuu wa mkoa. Have I just said it? Yes ni dogo kuliko hata nyumba yangu!!!!

  And yet tunaona gavana kukaa nyumba ya 1.2 million USD ni jambo la kawaida.
   
 5. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Maktaba kuu ya Dar inaboa,still wana old systems za kutafuta vitabu(yaani vitabu vinatafutwa manually),maktaba haina hata database ya vitabu vyao!,ni ngumu sana kukuta latest versions za vitabu pale.Yaani ile maktaba imesuswa.Sasa za mikoani ndo utachoka
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hata kwenye miradi mikubwa ya uwekezaji kama mlimani city nilitegemea kuwe na kipengele cha kuwekeza kwenye maktaba ya kisasa, ikichukuliwa kuwa eneo lenyewe lipo ndani ya chuo kikuu cha dar...

  Tuna tatizo zaidi ya tunavyofikiriii..
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sijui nini Vipaumbele vyetu?
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hatuna culture ya kusoma, tunasoma for a purpose kutafuta kazi, kwa ajili ya kufanya mitihani na au habari za udaku. Ni mara chache utaona mtu anatoa gazeti, jarida au kitabu kijisomea kama hana kazi ya kufanya. Ni afadhali aongelee arsenal na chelsea kuliko kusoma kitabu au Gazeti. Majumbani mwetu TV tumezipokea bila orientation zimefuta kabisa culture ya kusoma na kusikiliza vipindi vya kielimu redioni.

  Matokeo yake umbumbumbu kwenye knowledge na ujuaji kwenye mambo yasio muhimu.

  Sio Maktaba tuu hata kwenye majumba yetu ya makumbusho viongozi wetu hawaendi kabisa, nenda amboni caves, kimondo mbozi, makumbusho ya ujiji ( walipokutana livingstone na stanley) soma kitabu cha wageni ukiona jina la Waziri walahi itakuwa ajabu. Sasa hivi ujiko ni kupeleka watoto wet and wild na south beach ambako hagain chochote.
   
 9. b

  buckreef JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lakini wenye makosa ni viongozi tu au pamoja na sisi wote ambao hatuna culture ya kusoma?

  Nafikiri kwa hili tujilaumu wote kwa kuwa sio wasomaji labda mpaka kuwe na mtihani.
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  haya...proposal yako inakuwaje? How do u train kids to read? Pesa ya kununua vitabu utaambiwa haipo. Books are actually quite expensive and i dont see many parents who would be willing to buy books!
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  jamani kitabu cha mwanao unaona expensive kununua, hebu nitajia majina ya hivyo vitabu and i will direct you toa bookshop selling books at reasonable prices. Secondly watoto wasiwe addicted to TV wakiwa na Tv hakika hawapenda kusoma.

  Wazazi nasi tunachangia, kwa siku bia tatu bia moja say 1500 X 3= 4500/= X 30 days =135,000/=. Ina maana ukisacrifice kugida kwa mwezi unapata vitabu kadhaa vya mtoto. Na mtoto akisoma atapata knowledge na hatapata hangover wewe ukigida unaamka kichwa kinauma na knowledge hujapata.

  Tafakari chukua hatua.
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji nimeshtuka kuona kati ya wilaya 127 ni wilaya 11 tu zenye maabara. Hii inadhihirisha ni aina gani ya watawala wamekuwa madarakani. Kama ulivyosema mtu anajiuliza Kikwete alipata wapi ujasiri wa kusema ktk miaka 5 ijayo kila mwanafunzi kwenye shule za sekondari atakuwa na kompyuta yake ili hali hata wilaya hazina maktaba ya watu kujisomea?

  Binafsi sishangai hali hii kwa sababu wengi ya wakuu wa wilaya ni mbumbumbu na wengi ya wakurugenzi ni wezi wa mali ya umma.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu unalosema ni sahihi kwamba kiasi fulani watanzania/waafrika kwa ujumla tunatumia pesa zaidi kwenye mambo mengine badala ya kutilia mkazo kwenye elimu ya watoto wetu. Lakini serikali bado inawajibu wa kuweka miundombinu muhimu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii.
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Very true. Africans especially Tanzanians wengi wetu ni wavivu wa kusoma.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kuwa na mashule ni kitu kimoja na nakubali kuwa hilo ni jukumu la serikali, lakini kwenda kwenye public library ni kitu kingine na kuwa na Home Library ni kitu kingine. Tukubali kuwa culture ya kusoma tanzania imekwisha na ndio maana tu wajinga kiasi hiki. Zamani nyumba za wazazi wetu zikuwa zinapambwa sebuleni na bookshelfs, home library was a must by then. Ona leo sisi tunashindana kununua DVDs na kuunganisha DSTV, Easy Tv, etc mambo ya elimu tumesahau kabisa.

  Pamoja na uchache wa Maktaba kiongozi gani amewahi kuingia maktaba angalau kuona pakoje na kuhamasisha watu wasome na au wajiunge na huduma hiyo? Maktaba ni kama mtoto yatima Tanzania inaishi kwa donations ya outdated book from abroad . Ombi maalumu hata wewe ukiwa na kitabu cha zamani ukanunua new edition donatecha zamani to the nearest Library watashukuru na kukuandikia barua kuacknowledge.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Culture ya kusoma jamani inajengwa. Mimi milele nashukuru wazazi kuniintroduce na maktaba kila jumamosi, walikuwa wanaleta magazeti ya Uhuru Mzalendo na DAily news kila siku (japo yalikuwa ndiyo ya jana yake). Nashukuru niliposoma SEC - o level sijui wamarekani gani walitupatia vitabu tukatengeneza maktaba yetu pale. Mimi naamini utamaduni huu unajengwa na watu wenyewe.

  Wangapi hapa sisi wenyewe tunaleta vitabu nyumbani na kusoma na watoto wetu? Wangapi tunaweza kwenda hata kwa kupita karibu na library tu. Hapa nilipo nimezungukwa na maktaba kubwa tatu - ya Mji, ya Chuo Kikuu na ya Mji mwingine mkubwa ambako pote nina uanachama. Juzi nimeenda kwenye maktaba ya Southfiled na kuweza kupata kitabu juu ya Nyerere "We must Run while they Walk" ambacho kingejibu maswali ya watu wengi sana humu. Sijui kama kinapatikana hata kwenye library zetu.

  Sijui kwenye vyuo vikuu vinavyoanzishwa nchini ni kwa kiasi gani vimejenga maktaba. Siwezi kushangaa hata Ikulu haina maktaba!
   
 17. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Mtanzania,maktaba,kusoma ni maneno ambayo ni aghalabu kuyapata kwenye sentensi moja.
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji, tujuze mambo ya muhimu kwenye hicho kitabu, nakumbuka mzee wetu alikuwa ametunga vitabu vingi sana wakati huo vikipatikana Tanzania Publishing House sijui vinapatikana wapi kwa sasa. Wizara ya Elimu wakaweka kwenye mtaala, duh ! wakaja wajanja wakaona watanzania wakisoma busara zake watawashtukia sasa hivi havisomwi tena mashuleni.  Busara iliyomo ndani ya vitabu vile ni valid mpaka leo.
   
 19. p

  pareto 8020 Member

  #19
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wazo lako la kuwa na maktaba katika kila halmashauri ni zuri sana.... It is much easier kwa halmashauri kujenga na kuendesha maktaba kwasababu wao wana vyanzo vya kupata resources za kuendesha maktaba hizo.

  Mimi nadhani kinachotakiwa ni kutafuta njia ya kufikisha wazo hili kunakohusika ili lifanyiwe kazi...tutakuwa hatutendi haki kuacha wazo la aina hii liishie kwenye mjadala tu tena ambao naona wengi wetu badala ya ku appreciate wazo lenyewe tumerukia kwenye lawama na kuponda...probably hilo nalo ni tatizo letu la kitaifa...inapotolewa hoja nzuri badala ya kuichukulia positively na kutafuta jinsi ya kuifanikisha tunakimbilia kufanya uchambuzi ulio negative, ambao mara nyingi hauwi well-researched.

  Litakuwa jambo la faraja sana kuona, wazo hili linafanyiwa kazi na kutoa matunda...hapo "great thinker's forum' itakuwa imetoa mchango mkubwa kwa taifa.

  Nikirejea kuhusu utamaduni wa kujisoemea, ninakubaliana na MMM kwamba mazoea hujengwa....hakuna linaloshindikana...kama ilivyo sasa hatuna mazoea ya kusoma magazeti na vitabu..tukianzia chini mashuleni, majumbani na kwenye jamii kwa ujumla kujenga utamaduni wa kusoma..inawezekana.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,384
  Trophy Points: 280
  Mada ya Kasheshe imenikumbusha tu hapa.. we have been here..
   
Loading...