Kiongozi CHADEMA jela kwa kumuangalia hakimu vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiongozi CHADEMA jela kwa kumuangalia hakimu vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Asha Abdala, Dec 27, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  na Moses Ng'wat, Mbozi

  UONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, unakusudia kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu ya miezi miwili jela iliyotolewa na mahakama ya wilaya dhidi ya kada wa chama hicho Wallece Kaminyoge, kwa madai kuwa alimuangalia vibaya hakimu, tena kwa jicho dogo kama kidonge cha ‘piriton’.

  Wakati chama hicho kikiandaa utaratibu huo, hakimu mkazi wa wilaya hiyo, Nenura Kajanja, aliyetoa adhabu hiyo, ameibuka na kupinga hoja hiyo ya viongozi, na kudai kuwa ni haki kwa kila aliyehukumiwa kukata rufaa kama hakuridhika na maamuzi yaliyotolewa dhidi yake.

  Akizungumza na Tanzania Daima, jana, wilayani hapa, Katibu wa CHADEMA, Godfrey Siame, alisema chama hicho hakijaridhishwa na hukumu hiyo na kwamba wana wasiwasi huenda ilitawaliwa na ushawishi wa kisiasa kutokana na kesi ya msingi iliyowasilishwa na chama hicho ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

  Alifafanua kuwa wakiwa katika mazingira ya mahakama ya wilaya mjini Vwawa desemba 14, mwaka huu, kwa lengo la kwenda kusikiliza mwenendo wa kesi waliyofungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa kijiji cha Mlowo, baada ya tarehe hiyo kufika wakiwa wameandamana na Wallece Kaminyoge, anayetumikia kifungo hicho, walikaa hadi majira ya saa tisa bila kuitwa na muda wa kusikiliza kesi ulipomalizika waliingia masjala ili kupewa tarehe ya kesi yao ndipo ilipotokea kutokuelewana na hakimu huyo.

  Aliongeza kuwa baada ya kumuuliza hakimu huyo aliamuru askari aliyekuwepo mahakamani hapo kumuweka chini ya ulinzi kada huyo kwa maelezo kuwa alimuangalia vibaya, tena kwa jicho dogo kama piritoni.

  “Kwa kweli tulimuomba amsamehe kama kosa lilikuwa hilo, lakini hakimu hakutuelewa na kusimamia kauli yake, huku akituhakikishia kuwa atamfunga tu,” alisema Siame.

  Siame alisema baada ya hapo mtuhumiwa huyo alipelekwa kituo cha polisi Vwawa na kufunguliwa mashtaka lakini walimuomba mkuu wa kituo wamuwekee dhamana na alikubali kwa ahadi ya kumrudisha siku inayofuata.

  Alisema siku ya desemba 15 walimfikisha kituoni hapo na hatimaye alipelekwa mahakamani na kesi yake ilikuwa ya tatu kutajwa na hatimaye kuhukumiwa miezi miwili bila kujitetea.

  “Tunajua hatuna uwezo wa kuingilia uhuru wa mahakama, lakini kwa hili tungependa haki itendeke tunaona kama mwenzetu kaonewa tena kwa ushawishi wa kisiasa,” alisema Siame.

  Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake, hakimu huyo mkazi wa wilaya ya Mbozi, Nenura Kajanja, alisema kila mshtakiwa ana haki ya kukata rufaa ya kupinga maamuzi dhidi yake kama ana wasiwasi na si kuzua mambo kama wanavyofanya viongozi hao wa CHADEMA.

  Akieleza yaliyotokea hadi kuchukua hatua ya kumhukumu kifungo hicho miezi miwili, Kajanja alisema ilitokana na kada huyo wa Chdema kudharau mahakama na kumuonyesha ishara ya matusi.

  Alisema siku ya Desemba 14, kabla ya kuingia chumba cha mahakama aliwakuta watu hao wakiwa masjala na alipowataka kutoka nje ili kupisha shughuli nyingine ziendelee, mshtakiwa huyo alikuwa mbishi na baadaye alimnyooshea kidole cha katikati ambacho tafsiri yake huwa ni matusi.

  Alisema hakuishia hapo kwani hata walipoingia katika chumba cha mahakama mshtakiwa huyo alipoulizwa maswali alijibu kwa mkato, bila kujali kuwa kufanya hivyo ni kuidharau mahakama.

  “Niambie wewe ndugu mwandishi wa habari mtu kama huyo ungeweza kuchukua hatua gani?

  “Mimi nasema hivi: katika vitabu vya sheria hakuna kifungu kinachoeleza kumhukumu mtu ati kwa sababu amekuangalia vibaya au vizuri, maelezo yao ni ya ajabu sana,” alisema Kajanja. Alisema baada ya kugundua kuwa mshtakiwa hakuwa tayari kujutia wala kujifunza makosa yake ndipo alipomhukumu kifungo hicho kwa kutumia kifungu cha sheria namba 144(k). Viongozi hao wa CHADEMA wilayani Mbozi walidai kuwa kesi ya msingi iliyofunguliwa mahakamani hapo ni ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa kijiji cha Mlowo ambapo mgombea wake, Rodrick Sanga, alishindwa na mgombea wa CCM.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu ni miongoni mwa mahakimu wapumbavu kabisa kupata kutokea katika nchi hii..ndio maana hata jina lake ni Kajanja..dawa yake ni kupigwa mawe maopaka auwawe...pumbavu kabisa anadhalilisha taaluma ya sheria kwa kiasi kikubwa sana
   
 3. e

  echonza Senior Member

  #3
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona ubabaishaji unakomaa kiasi hiki nchini kwetu? Kama hayo hapo juu ni ya kweli basi Tanzania inaelekea kubaya. Inakuwaje mtu ahukumiwe pasipo kujitetea? Je, kulikuwa na ushahidi gani kuhusiana na vitendo hivyo vinavyodaiwa kutendwa na mtuhumiwa?
  Vinginevyo sasa watu tutakuwa tunaviziana tu hata tuna tofauti zetu za kuujirani zikawekewa mazingira mtu kupelekwa mahakamani kwa kubambikiziwa kesi isiyo na msingi wowote! Tunayokazi kweli kweli!!
   
 4. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa kwanini usiwasaidie wewe?fani ya sheria ndiyo fani yako.
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,190
  Likes Received: 996
  Trophy Points: 280
  Huyu hakimu amenikumbusha yule hakimu aliyemhukumu mbwa kifo kwa sababu tu eti mwenye mbwa alimwita jina la immigration. Mahakimu wa aina hii inabidi wachunguzwe kwa makini huenda wanapanda kwenye mimbara zao wakiwa wameisharashia gongo kidogo. Eti kaniangalia vibaya, jamani mahakimu kama hawa sii watawahukumu vifongo watu wote wenye makengeza(macho mkasi) kwa madai kwamba wamewaangalia vibaya??
   
 6. b

  bnhai JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,206
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Huko ni kuchezea pesa za walipa kodi. Nadhani hata kama angepatikana na hatia ni bora kumfunga kifungo cha nje na si hivyo. Vinginevyo magereza zinajazwa watu hovyo.
  Ila na yeye hakimu amechuma janga ajindae kula na wa kwao maana tayari kila mtu anamtazama vilivyo. Soon or later atajutia maamuzi ya kijinga ya kusukumwa na munkari badala ya sheria
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndiyo Tanzania yetu!!
   
 8. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mkoa wa mbeya siasa 24/7/365
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  bongo MUFILISI
   
 10. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mahakimu mikoani huko ni miungu watu,wanatoa hukumu za ajabu sana,sijui wanatumia sheria za wapi. Kama huna watu wa kukusaidia kisheria umekwenda.

  Mara nyingi huwa wanachukua mambo ya mitaani na kuyahamishia mahakamani. Kunahakimu huko Rukwa alidaiwa deni lake la bia lililokaa miezi minne,kesho yake mwenye baa akakamatwa akasumbuliwa sana mahakamani.
   
 11. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  wanaokwenda jela wote si wenye hatia..........
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata mimi ningekuwa Hakimu, ningemfunga huyo jamaa. Tena nadhani hukumu aliyopewa ni ndogo sana. Ingefaa awekwe ndani kwa miezi si chini ya 6. Huwezi kudharau mahakama halafu ukaachiwa tu.
   
 13. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii nayo itakuwa kesi ya aina yake!! Huyo Hakimu ana ushahidi, Au ni yeye mwenyewe aliona makengeza?
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huu ndio mfumo wa sheria katika taifa letu na pia kama ndio mahakimu kama hawa basi ni hatari sana katika ustawi wa jamii yetu
   
 15. N

  NAHUJA JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 15,003
  Likes Received: 15,564
  Trophy Points: 280
  mwe mwe mwe jamani
   
Loading...