KIONGOZI BORA HUKUBALI KUKOSOLEWA

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,685
1,111
Kiongozi bora ni yule mwenye kukubali kukosolewa na kukosoa kwa kuwa amebeba dhima nzito ya kuwaongoza waliompa dhamana hiyo. Kuogopa kukusolewa ni dalili ya kuwatalawa waliokupa dhamana na si kuwaongoza,unapowaongoza wananchi unatakiwa uwe kiongozi unaye kunjika ambaye kukosolewa ni sehemu ya changamoto ya uongozi wako.

Una weza kuwa kiongozi mzuri Sana lakini watesi wako wakakufanya Mungu mtu katika uongozi wako kwa kuwa hawataki uguswe wala kukosolewa,hizo ni dalili mbaya ambazo zinapelekea kujijengea sifa ya kuogopwa hata pale unapo Fanya makosa,kwa kuwa tu umeshawajengea wananchi wako dhana ya hofu juu ya uongozi wako.

Farao/Firauni alikuwa mtawala katika nchi ya Misri ambaye hakupenda kabisa ushauri wenye mwelekeo wa kuukosoa utawala wake, hali iliyopelekea kujiita Mungu na kufanya kufuru iliyopitiliza,matokeo yake Mungu aliye hai hakumuacha hivi hivi,mpaka kesho kutwa hayati huyu Ana dhalilika ili kila umma wa Mwenyezi Mungu uone na kumjua kafiri huyu. Pamoja na adhabu anayoitumikia akiwa maiti,ndani ya utawala wake Allah aliweza kumwinua kiongozi aliyeweza kuonyesha sifa na uvumilivu wa kiuongozi kwa kuwakomboa Wayahudi waliokuwa utumwani Misri,kiongozi ambaye hata hao Wayahudi walihoji na kudhihaki uwezo wa Mungu,lakini mwisho wa siku walitoka ndani ya utawala wa kidhalimu mpaka mauti yalipo mkuta kiongozi huyo aliyepewa dhima hiyo ya kuwaokoa toka utumwani.

Kwa nini sisi binadamu wa kizazi hiki tunashindwa kusoma Alama za nyakati ambazo tunaishi tukiwa na mifano mingi ya watawala na viongozi wa dunia hii Kama ilivyo bainishwa kwenye vitabu vitakatifu!

Tumeletewa itikadi mpya yenye jina la Demokrasi,utawala wa watu wenye kutoa Uhuru na misingi ya utawala bora,misingi yenye kujenga utashi wa watawaliwa kuwa na sauti ya kuhoji na kukosoa lakini pia kuwajengea Uhuru wa kutoa habari na kupata habari. Misingi hii katika tawala za Kiafrika imegeuzwa kuwa haki moja tu ya kufanya chaguzi hata Kama chaguzi zenyewe si uhuru na haki. Lakini watawaliwa hao hawana haki ya kuhoji mamlaka halali ya watawala hao,ikiwa ni pamoja na kupoka uhalali wa Uhuru wa kutoa habari na kukosoa tawala hizo.

Matokeo ya ukandamizaji wa demokrasia ni kufungiwa kwa vyombo vya habari vyenye mrengo wa kukosoa na kubainisha maovu ya watawala kwa kivuli cha uchochezi. Kukamatwa kwa watu wenye mrengo wa kunyooshea tawala hizi vidole kwa matendo mabaya ndani ya tawala hizo.

Kila jambo lenye hasara lina faida pia,kwa tawala hizi wenye kunufaika ni wale waliokubali kuishi kinafiki na kujipendekeza kwa watawala wakitegemea fadhila ya kutunukiwa vyeo ambavyo ni machungu kwa watawaliwa.

Mfalme Nekabudreza alipingana na ndoto alizoota zikiashiria kudondoka kwa utawala wake,ilifikia hatua ya kuwadhuru washauri wake ambao walikuwa watafsiri wa mambo mbalimbali yajayo,lakini mwisho wa siku Mwenyezi Mungu aliweza kumuibua kiongozi ambaye ni Daniel na kuangusha utawala ule dhalimu.

Ni wajibu wetu wana wa Afrika na dunia hii kushauri watawala wetu kuwa uongozi ni dhamana iliyobeba dhima nzito katika kuwatumikia wanao ongozwa ili kufikia matakwa ya walio wengi ili kuweza kuzivusha tawala zetu kuwa sehemu salama tunazo paswa kuishi wana wa Adam. Lakini tusitumie nguvu kubwa kudhibiti wakosoaji wenye mrengo wa kujenga misingi imara ya uongozi wa nchi zetu kwani tukiogopa kukosolewa ni dalili za kuzipeleka nchi zetu kwenye mkono wa chuma ili kuwafunga makufuli midomo isiyoweza kuvumilia. Tukibadilika ,Afrika itabadilika pia na kuwa sehemu salaam kwa wana wa Afrika.

Free Ben,bring back Wasanane
 
Tanzania hakuna kiongozi hata mmoja anaekubali kukosolewa awe wa serikali au wa vyama vya siasa hata boss makazini
 
Lazima
Tanzania hakuna kiongozi hata mmoja anaekubali kukosolewa awe wa serikali au wa vyama vya siasa hata boss makazini
Lazima tubadilike ili tuweze kutimiza malengo ya uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom