Kiongozi bila aibu unajisifia kutibiwa nje ya nchi?

Greek

Member
Nov 8, 2010
68
1
Inaudhi sana. Kiongozi bila aibu unadai kuwa ni haki yako kutibiwa nje ya nchi? Badala ya kutoa wazo la kujenga hospitali ili wote tutibiwe hapa. Alafu kesho utasema hata wewe haujui kwani Tanzania ni masikini, haiendelei na maisha yanazidi kuwa magumu.
Au ndio tutaishia kusema western wanatunyonya
Shiiit..!
 
Ndio walichomuahidi ccm na akakubali kuungana nao,sasa anaanza kukosa hoja na anaanza kujitetea.
 
Mwanasiasa ni mwanasiasa tu. Seif Shariff naye ni mwanasiasa kama wengine. Hana lolote ni porojo tu.
 
Inaudhi sana. Kiongozi bila aibu unadai kuwa ni haki yako kutibiwa nje ya nchi? Badala ya kutoa wazo la kujenga hospitali ili wote tutibiwe hapa. Alafu kesho utasema hata wewe haujui kwani Tanzania ni masikini, haiendelei na maisha yanazidi kuwa magumu.
Au ndio tutaishia kusema western wanatunyonya
Shiiit..!

Kuna vitu angalau viwili hivi ambavyo mashabiki wa CUF hupenda sana kuvitumia kama rejea ili kuonesha kwamba wao (CUF) ni wanaharakati wa mageuzi Tanzania navyo ni:-

(i) Mauaji ya mwembechai
(ii) Mauaji ya Pemba

Kama kweli haya matukio yalitokana na harakati za CUF kupigania wanyonge, kauli anazotoa Katibu Mkuu (Maalim Seif) leo zinatia kichefuchefu. Kama kweli damu hizo za WANYONGE zimechangia kumweka madarakani kauli zake zilitakiwa sana kuwa katika muonekano wa kuwajali WANYONGE na sio za maringo kama alivyofanya.

Kauli za "MIMI NA FAMILIA YANGU TUNASTAHILI KUTIBIWA NJE" si za kiuanamapinduzi bali za mlevi wa madaraka anayeonekana kusahau alikotoka na waliochangia kumfikisha hapo alipo. Sawa, hata kama anastahili kama alivyosema, angetoa tu kauli ya kiungwana angeeleweka. Kwani asiyestahili matibabu mazuri ni nani? Au hapo ndio kilele cha harakati zako (na CUF) zote Mh hata kusababisha umwagaji damu kule Pemba na Mwembechai? Kama ndivyo, umechemsha vinginevyo simama upande wa wanyonge.
 
Hayo ndio matunda ya demokrasia ya kinafiki wachache ndio wanaostahili kupata huduma muhimu, lingekuwa jambo la busara kama Maalim Seif angejenga hoja ya kimsingi kuboresha huduma za hospitali ya V.I Lenin, ukizingatia waziri wa afya Juma Duni ni kiongozi wa CUF, si amini kabisa kama alichotibiwa India MOI wangeshindwa kumsaidia lakini huyu ni CCM hakuna cha ajabu alichokifanya, hayo ndiyo aliyokuwa akiyapigania miaka yote sasa kayapata, amesahau wapemba wenzake hawana hata aspirini.
 
angalieni nini amesema mukivamia mutapotea nanuku siovibaya kwa kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kumuhudumikia yule alo mchagua ....na vile vile hata raia kama ana matatizo yasiyoweza kutibika nchini atasafirishwa pia.mwisho wakunukuu.mwenye akili timamu akichambua maelezo ataelewa seif anawajali raia.
 
Pumba, unatetea hata yasiyobebeka, hayo ya kwake yalishindikana ndo akaenda nje? Hukuzaliwa na CUF ndugu yangu,..
 
Hata mimi nilishangaa sana ati "ninahaki ya kutibiwa nje ya nchi" nikasema duu hapa sasa patamu na wala hakusema kama anampango wowote wa kuboresha huduma za afya vijijini ili na sisi tupate huduma stahili. SIMPLY UBINAFSI AT ITS BEST.
 
Atuambie toka ameingia alishapeleka watz wangapi nje kirahisirahisi hivyo nje kutibiwa?
 
Back
Top Bottom