Kiongozi awaambia wananchi mwaka 2015 waweke sura mpya kuanzia urais mpaka udiwani

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,650
1,250
Katika hali ya kukinadi chama kinachojiita chama tawala,kiongozi huyo ngazi ya wilaya alijikuta akiwaambia wananchi ktk mkutano wake ktk jimbo moja lililopo mpakani na nchi ambayo sasa wanafanya uchaguzi wa rais, mwakani wanahitaji kuona sura mpya kuanzia kwenye Urais,wabunge hadi udiwani.

Aliwaambia itakuwa haina maana rais mpya diwani mpya mbunge kuukuu,kufanya hivyo ni sawasawa na nguo nyeupe kuweka kiraka cheusi katikati.

Mwisho alimalizia kusema kwamba walioanza na JK wataondoka na JK,kauli ambayo inabainisha dhairi alikuwa akimpiga dongo mbunge wake ambaye hawapikiki chungu kimoja.

Wanajf tuijadili hiyo kauli kwa mapana yake kama inaweza kuwa na tija ktk uchaguzi wa mwakani kwa vijana wanaodhamilia kugombea maeneo mbalimbali katika chaguzi za ubunge na udiwani kupambana na wabunge wakongwe waliodumu bungeni zaidi ya muongo mmoja.Karibuni.
 

uwemba1

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
991
1,000
Tatizo umeweka kila kitu kapuni majina yake, eneo la tukio na details mhimu halafu tuchangie! Ulitakiwa uweke open unachokiongelea sio mafumbo hata kama jukwaa haliaminiki siku hizi wewe jiamini weka wazi
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Yaani ninvyoisubiri hiyo 2015 Mungu anipe uzima kuanzia serikali za mitaa mpaka urais ccm hawapati kura yangu na za marafiki zangu tupo wengi.
 

Ngonini

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
2,024
1,195
Yaani ninvyoisubiri hiyo 2015 Mungu anipe uzima kuanzia serikali za mitaa mpaka urais ccm hawapati kura yangu na za marafiki zangu tupo wengi.

Kama hapa JF kila mtu atapa watu 99 wakumsindikiza mwakani kwenda kuinyima ccm kura basi ndo utakuwa mwisho wao!
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,774
2,000
Huu ni unabii kwa wataz wote kuwa CCM haitakiwi kuwepo kabisa mwaka 2015 ing'olewe pamoja na mizizi yake yote.
 

ligera

JF-Expert Member
May 17, 2014
2,650
1,250
Tatizo umeweka kila kitu kapuni majina yake, eneo la tukio na details mhimu halafu tuchangie! Ulitakiwa uweke open unachokiongelea sio mafumbo hata kama jukwaa haliaminiki siku hizi wewe jiamini weka wazi

kuwa mbunifu ,acha uzembe wa kufikiria,hujawai kusoma hadithi za kufikirisha ,kama kitabu cha kuli,shida,alfu ulela, nk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom