Kiongozi atakayekuja kunyoosha nidhamu ya nchi hii ana shughuli pevu!!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,978
5,025
Nilikwenda leo ofisi moja ya chuo kikongwe cha afya ili nipate huduma niliyohitaji. Nilifika pale saa 2 kamili nikaambiwa mhusika hayupo, 3:15 hayupo, 4:30 hayupo, 6:00 hayupo, niliporudi saa 7:35 nikamkuta ila akaniambia anapata lunch hivyo nirudi baadaye. Nikasitiri hasira zangu nikaondoka. Cha ajabu saa 8:24 nikaenda ofisini sikumkuta. Hasira ikanipanda kidogo nichane hata document nilizokuwa nazo. Huo ni mfano tu lakini ofisi nyingi za umma ziko hivyo. Wafanyakazi wengi ni wavivu kwa sababu mwisho wa mwezi mshahara unaingia. Unakuta ofisi ina malimbikizo ya kazi kibao lakini wahusika wanachelewa kufika, wanawahi kuondoka na muda wanaokuwepo ofisini hawafanyi kazi. Rais atakayekuja kuirekebisha hii tabia atachukiwa sana kwani wakosaji wengi unapowabana wanahisi wanaonewa. Lakini ni lazima atokee mtu wa kutunyoosha ili tuachane na huu ukiritimba. Ni bora achukiwe kwa muda mfupi lakini mambo yaende vizuri na baadaye watamfurahia kwa kuwafanya wawe waleta maendeleo! Wafanyakazi wa serikali tuamke na kuachana na mazoea ya bora liende, maendeleo hayaji kwa namna hii! Wenzetu wanapaa na sie tunatambaa,ndo maana vijana wengi wanaogopa mashirika binafsi eti unapigishwa sana mzigo. Kuna haja ya kuanza kulipa watu mshahara kwa masaa aliyofanya kazi ili watu wajitume!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom