Kiongozi asie na maarifa ya katika siasa na kuendesha uchumi, ni mzigo mzito kwa chama chake na kwa wananchi wake kwa ujumla

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,987
144,318
Kiongozi yoyote wa kisiasa asie na maarifa ya kawaida kabisa katika kuendesha uchumi na kufanya siasa,kiongozi wa aina hiyo ni mzigo kwa chama chake, na pia watu wote aliokabidhiwa jukumu la kuwaongoza.

Sometimes ni bora ukamudu/ukafanya vizuri katika uchumi kwani uchumi unaweza kukubeba kisiasa ila ukikosa vyote,basi ujue umeshafeli na umewaangusha waliokuamini.

Kujenga ushawishi wa kisiasa kwako binafsi na kwa chama chako unashindwa na unabaki kutumia mbinu mbovu na zisizo faa kukujenga wewe na chama chako kisiasa,na kama haitoshi,hata katika uchumi pia unafeli,hakika unageuka liability kwa chama na kwa unaowaongoza.

Ukishindwa katika haya,ni bora kujiuzulu na katika nchi za watu wasiotaka kuchezewa,wataandamana kukutaka uondoke ofisini iwe mnvua iwe jua.
 
Mwalimu nyerere alikuwa mzuri kwenye mengine ila kwenye uchumi alifeli alihitaji washauri kama kina Kambona wangemsaidia
 
Wenzetu huwezi pewa leseni ya udereva kama we we si tajiri maana ukiwa tajiri au mfanyabiashara mkubwa ni lazima utaujua uchumi kivitendo.Usipoujua uchumi utawasomesha namba Watu wako ukidhani unawakomoa kumbe unajifunga kamba shingoni,maana uwasomeshao namba ndio wakuleteao mapato.Kiuchumi tafsiri ya kusomesha namba na kukaza vyuma ni kuuwa sekta binafsi at the end makusanyo yatapungua.
 
Watanzania kukubali kulishwa takataka! Mnaona kama Kambona ndio angeigeuza nchi hii kuwa ulaya! Kwa taarifa yako uchumi na vipimo vyake vilikwa bora wakati wa Mwl kuliko awamu hizi ambazo mshahara wa Mwl wa shule ya msingi hauwezi hata kumfikisha katikati ya mwezi!
Mwalimu nyerere alikuwa mzuri kwenye mengine ila kwenye uchumi alifeli alihitaji washauri kama kina Kambona wangemsaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi yoyote wa kisiasa asie na maarifa ya kawaida kabisa katika kuendesha uchumi na kufanya siasa,kiongozi wa aina hiyo ni mzigo kwa chama chake, na pia watu wote aliokabidhiwa jukumu la kuwaongoza.

Sometimes ni bora ukamudu/ukafanya vizuri katika uchumi kwani uchumi unaweza kukubeba kisiasa ila ukikosa vyote,basi ujue umeshafeli na umewaangusha waliokuamini.

Kujenga ushawishi wa kisiasa kwako binafsi na kwa chama chako unashindwa na unabaki kutumia mbinu mbovu na zisizo faa kukujenga wewe na chama chako kisiasa,na kama haitoshi,hata katika uchumi pia unafeli,hakika unageuka liability kwa chama na kwa unaowaongoza.

Ukishindwa katika haya,ni bora kujiuzulu na katika nchi za watu wasiotaka kuchezewa,wataandamana kukutaka uondoke ofisini iwe mnvua iwe jua.
Mashairi ya pangoni ndiyo mwendo hivi sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endelea kujiuliza, sasa hivi hayo mashirika yako wapi?
Kuyaua kumesaidia nini kuliko yalipokuwepo?
Ajira zimeongezeka?
Elimu na matibabu bure vimeongezeka kama ilivyokuwa wakati wa Mwl?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwalimu akuwahi ongeza tija wala kukuza uchumi vyote alivotumia ni vilivoachwa na wakoloni kuanzia pesa na hazina zote alizotumia
 
Back
Top Bottom