Kiongozi anedhibiti wapinzani na vyombo vya habari mara nyingi huwa na element za wizi na ufisadi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,984
Ukiona kiongozi yoyote yule duniani katika Taifa lolote anatumia nguvu nyingi kudhibiti vyombo vya habari na wapinzani wake ujue mara nyingi anafanya hivyo ili kuficha maovu yake kama vile uminyaji wa haki za rai,utesaji wa raia pamoja na wizi na ufisadi.

Na pia kiongozi asietaka uwazi katika serikali yake mimi huwa sina imani nae kabisa maana ni lazima mtu ujiulize anaficha nini wakati yote anayoyafanya anayafanya kwa niaba yenu kupitia dhamana mliomkabidhi sasa iweje awafiche?

Mara nyingi viongozi wa aina hii duniani huwa wagumu kuachia madaraka na wakiamua kuachia madaraka basi huhakikisha wanarithiwa na vibaraka wao watakaolinda maovu yao pamoja na mali zao walizochuma kifisadi.

Mifano ya viongozi hawa ni kama Mobutu wa Zaire,Idd Amini Dada wa Uganda,Napoleon wa Ufaransa na wengineo wengi.

Kiongozi mwingine wa aina hii alikuwa ni Benito Mussolini aliekuwa kiongozi wa Italia ambae unaweza kumsoma kupitia hii link HAPA

Ukimsoma huyo utapata somo zuri sana na utagundua jambo muhimu sana maana mtawala huyu mwanzoni alifanyia kazi malalamiko ya wanachi na kujizolea sifa kibao lakin baadae ikawa kinyume chake.

Ogopeni sana viongozi wa aina hii maana watawaacha mlio wengi mkiwa masikini huku wao na washirika wao wa karibu wakijineemesha kwa kutumia jasho lenu.
 
Kwani ulikuwa wapi mkuu kujua hilo? Check huyo jamaa SISONJE ndio utajua kuwa ulichoandika ni sawa.

Swissme
 
Mifano ya viongozi hawa ni kama kina Mobutu wa Zaire,Idd Amini Dada wa Uganda na wengineo wengi..
Umekuwa mwogamwoga sana siku hizi. Why, kwa ninii? Nasikia huko kwenu mzee mwenyewe ananegoshieti tender za kununua ndege, train za kutumia umeme usiokuwepo na ujenzi wa viwanja vya ndege.
 
Usijali ipo siku atahamia upande uliopo ili muwasunte wanaomtetea saiv wakihoji wizi na ufisadi wake
 
Tutajie kiongizi ambae si mwizi hapa tz

Naam umekuja vizuri sana. Kwa hiyo unataka kutuambia umekubali kuwa viongozi wote wa Tanzania ni wezi ndio maana unasaka asiye mwizi?

Swali zuri sana. Sasa tuwaache hawa viongozi wa vyama ambao hayo yao ni makundi ambayo yanapaswa kudhibitiwa na hao wanao wahusu. Twende kwenye serikali yetu sote.

Kama viongozi wote wa serikali ni wezi (according to your point) hiyo serikali haitufai kabisa bora tutafute nyingine kwa kutafuta hao wasio wezi kama ulivyo uliza.
 
Ukiona kiongozi yoyote yule duniani katika Taifa lolote anatumia nguvu nyingi kudhibiti vyombo vya habari na wapinzani wake ujue mara nyingi anafanya hivyo ili kuficha maovu yake kama vile uminyaji wa haki za rai,utesaji wa raia pamoja na wizi na ufisadi.

Na pia kiongozi asietaka uwazi katika serikali yake mimi huwa sina imani nae kabisa maana ni lazima mtu ujiulize anaficha nini wakati yote anayoyafanya anayafanya kwa niaba yenu kupitia dhamana mliomkabidhi sasa iweje awafiche?

Mara nyingi viongozi wa aina hii duniani huwa wagumu kuachia madaraka na wakiamua kuachia madaraka basi huhakikisha wanarithiwa na vibaraka wao watakaolinda maovu yao pamoja na mali zao walizochuma kifisadi.

Mifano ya viongozi hawa ni kama Mobutu wa Zaire,Idd Amini Dada wa Uganda,Napoleon wa Ufaransa na wengineo wengi.

Kiongozi mwingine wa aina hii alikuwa ni Benito Mussolini aliekuwa kiongozi wa Italia ambae unaweza kumsoma kupitia hii link hapa chini:

https://www.google.com/url?sa=t&sou...sATAf&usg=AOvVaw0SsywSLdfJ74I8XZoyYdIm&ampcf=

Ukimsoma huyo utapata somo zuri sana na utagundua jambo muhimu sana.

Ogopeni sana viongozi wa aina hii maana watawaacha mlio wengi mkiwa masikini huku wao na washirika wao wa karibu wakijineemesha kwa kutumia jasho lenu.
Wengine ni Mugabe wa Zimbabwe, Magufuli wa Tanzania, Kagame wa Rwanda, Nkuruzinza wa Burundi, Museveni wa Uganda, Kabila wa Congo na Bashite wa Dar es salaam
 
255f0310a03c0946962283ec65697b8c--star-gaze-military-cap.jpg

Baba Jesca wa Zabanga Kuku Ngbendu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom