Kiongozi anaeona kuchelewa kwa mradi ni kawaida tena anaongea kwa kutetea hilo

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,637
Kutokana na kuibuka kwa hoja kwanini mradi wa Bwawa la Mwl. Nyerere umechelewa na huko asilimia karibu 45 hadi sasa, na kimkataba ilitakiwa asilimia karibu 90. Mhe. sana Waziri wa nishati, Makamba akasimama kutoa maelezo.

Katika maelezo yake, ambayo yalijaa maneno matupu, na si kueleza watanzania kwa nini mradi umechelewa, na lini sasa utamalizika. Waziri huyu alitumia muda mwingi kusema kuchelewa kwa mradi au miradi ya kimkakati ni jambo la kawaida kwani hata ujerumani mradi wa kimkakati ulichelewesha. Hivyo haina haja ya kushangaa miradi inapochelewa. Tuchukulie jambo la kawaida.

Nimewaza sana katika hili! Hivi tunaviongozi wa namna gani, yaani anatetetea kuchelewa kwa mradi ni kawaida. Tena kwa kulinganisha na Ujerumani, bila kutwambia Ujerumani huo mradi wao ulichelewa kwa sababu gani na ulikuwa ni mradi wa nini? Inamaana Ujerumani mradi ukichelewa basi nasisi iwe kawaida?

Najua Makamba kaingia kakuta mradi huko nyuma, angetuonesha sasa anamikakati ipi na lini anategemea mradi utamalizika, asitetee tu ucheleweshaji.

Je, huyu ni kiongozi anae waza nje ya box kweli? Anatetea katika maongezi yake, tukubaliane naye kuwa haya mambo ya kuchelewa tuishi nayo na nikawaida. Nilitegemea angeonesha kutofurahishwa na ucheleweshaji ulofanyika. Na kutuambia sasa mradi utakwenda kwa speed, na lini utakamilika. Ili tuone utofauti wake katika utendaji.

Huyu mweshimiwa, ndiye tunategemea awe Rais, basi nchi hii itachelewa kwa kila kitu. Kwani kwake ucheleweshaji ni kawaida anautetea. Kila siku atatoa mfano wa nchi ya Ulaya iliyochelewesha mradi wa kimkakati, bila kutaja aina ya mradi na sababu za ucheleweshaji. Makamba umeniangusha.

Nilidhani unakuja na mikakati mipya, lakini nakuona unafanya mambo ya kimazoea, na huna jipya. Unapenda vijimaneno kucheza navyo ila sioni uongeapo unalenga nini hasa kuleta mabadiliko chanya.
 
Nakumbuka pia wakati alipokuwa waziri wa mazingira, huyu Makamba ndio alikuwa analeta figisu za kutoa vibali vya hilo bwawa kujengwa. Mpaka akatumbuliwa na Magufuli.

Nyuma ya pazia, alikuwa anahongwa na mabeberu ili acheleweshe ujenzi wa bwawa au azuie kabisa. Magufuli akamfyeka fasta baada ya kubaini uhuni aliokuwa anaufanya na wazungu.

Sasa pele limepata mkunaji. Tumekwisha.

Nchi iko mikononi mwa wazungu na mafisi.
 
January anatamani afanye mambo yake tu na si ya watanzania.

Ni rahisi sana kumalizia bwana la nyerere kuliko kuweka Tr70 kwenye gesi.
 
Endelea kutuhabarisha mkuu, enhee, walimuhonga kiasi gani hao mabeberu?!!!
 
Anyway Kifupi kama viongozi upcoming vijana wanakuwa na spidi slow kwenye mambo kuliko old dogs Kuna tatizo

Mategemeo mfano ya Magufuli alijaza vijana kila Kona akitegemea watakuwa na spidi kuanzia akina Nape,akina Makamba nk lakini baadaye aligundua hamna kitu mpaka wizara ya makamba ya mazingira akamtoa akamuweka Babu mbunge wa Ilala Ndipo mifuko ya Plastic ikaondoka kazi iliyomshinda kijana Makamba!!!

Vijana ambao at least wali prove capable Sana Ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mongela,mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mtaka na kijana mkuu wa Soko la hisa Dar es salaam Jina nimesahau

Vijana wengi spidi ya kazi hawana Ni akina business as usual.Very sad
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom