Kinyozi Mwingereza na barza yake katika historia ya uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
KINYOZI MWINGEREZA NA BARZA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

Miaka ni 1950 kuendelea hadi 1960 hapo kwenye hiki kiwanja na hilo jengo alikuwa kinyozi jina lake Muingereza.

Mwingereza "saluni," yake ilikuwa Mtaa wa Kirk Street na Sikukuu chini ya mti.

Muingereza ndiyo alikuwa kinyozi akitunyoa watoto wengi wa Gerezani enzi hizo.

Muingereza alikuwa akitunyoa kwa mkasi na kitana na mbele kaweka kioo kilichoegeshwa kwenye mti uliokuwa ukitoa kivuli mahali hapo.

Sehemu hii imechukuliwa na CCM na inakusudiwa kujengwa ofisi ya chama.

Mkono wa kulia kutoka hapo kama unaelekea Mtaa wa Livingstone ilikuwa nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa, mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes.

Hapa kwa Mwingereza palikuwa na barza ya wana TANU wakikutana hapo kupeana taarifa za harakati dhidi ya Gavana Twining.

Abdul Sykes alikuwa akipita hapo barzani kwa Mwingereza akitokea nyumbani kwake Mtaa wa Stanley kaongozana na Julius Nyerere akienda kumsalimia mama yake Bi. Mruguru.

Zuberi Mtemvu alipounda chama chake cha Congress barza kwa Mwingereza lilishamiri kwa jinsi wanachama wa Congress na TANU wakikutana hapo wanavyoshambuliana.

Mwingereza alibaki hapo akinyoa hata baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 lakini alikuwa haachi kujinasibu kumjua vizuri Nyerere akiwaambia wanaomsikiliza kuwa yeye akimjua sana Nyerere kwani alikuwa akipita pale kazini kwake na Abdul Sykes wakienda kumwamkia kwa Bi. Mruguru.

Mwalimu iko siku alisimamisha msafara wake ghafla akiwa anakwenda kufungua viwanda vidogo vidogo Gerezani alipomuona Bi. Mruguru kasimama na watu wengine pembeni ya barabara Mtaa wa Sikukuu na Lindi akiangalia msafara wa Rais wa Tanzania Julius Nyerere ukipita unasindikizwa na mapikipiki.

Mwalimu alisimamisha msafara wake si mbali na ilipokuwa barza ya Mwingereza.

Mwalimu Nyerere alitoka kwenye gari akaenda kumsalimia Bi. Mruguru.

Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Picha: Ilipokuwa barza ya Mwingereza, nyumba ya Bi. Mruguru kama ilivyo sasa na Mtaa wa Lindi nyumba zote za chini zikiwa zimevunjwa na kujengwa magorofa marefu na picha ya mwisho ni Bi. Mruguru bint Mussa.

Screenshot_20210916-105006_Facebook.jpg

Screenshot_20210916-105247_Facebook.jpg

Screenshot_20210916-105437_Facebook.jpg

Screenshot_20210916-105711_Facebook.jpg
 
Hiyo picha inaonyesha bado huyu mama alikuwa kijana wakati huo.

Naomba kuuliza la ziada. Hichi chama kikiitwa UTP kilikuwa na uhusiano gani na Congress na TANU?
 
Hiyo picha inaonyesha bado huyu mama alikuwa kijana wakati huo.

Naomba kuuliza la ziada. Hichi chama kikiitwa UTP kilikuwa na uhusiano gani na Congress na TANU?

Hiyo picha inaonyesha bado huyu mama alikuwa kijana wakati huo.

Naomba kuuliza la ziada. Hichi chama kikiitwa UTP kilikuwa na uhusiano gani na Congress na TANU?
Biti...
Bi. Mruuguru alizaliwa mwaka wa 1909 na kafariki 1974 akiwa na umri wa miaka 65.

UTP kilikuwa chama cha Wazungu na Congress chama cha Zuberi Mtemvu alichokiasisi kupinga TANU kuingia katika Kura Tatu mwaka wa 1958.

Uhusiano wa vyama hivi ni huo kuwa vyote vikipigania uhuru wa Tanganyika kwa sera tofauti.
 
Sehemu hii imechukuliwa na CCM na inakusudiwa kujengwa ofisi ya chama.

CCM wakijenga ghorofa refu basi wawapatie kina Sykes ghorofa mbili ktk jengo hilo. Mbali ya kubakisha historia ya mchango wa Bi Mruguru pia watakuwa wamewawezesha waswahili kumiliki makazi sehemu yao asilia.
 
CCM wakijenga ghorofa refu basi wawapatie kina Sykes ghorofa mbili ktk jengo hilo. Mbali ya kubakisha historia ya mchango wa Bi Mruguru pia watakuwa wamewawezesha waswahili kumiliki makazi sehemu yao asilia.
Bagamoyo,
Juma lililopita nilikuwa na ugeni nilitembelewa na rafiki yangu mmoja Prof.

Alitaka nimuoneshe sehemu ambazo yeye kazisoma na nyingine kuzisikia katika historia ya Tanganyika.

Tulikuwa Tanga, Bagamoyo, Dar es Salaam na Zanzibar.

Yeye ana fascination kubwa mno na mchango wa ukoo wa Sykes katika ukombozi wa Tanganyika.

Nilimpitisha ilipokuwa nyumba ya Abdul na Ally Sykes ambazo zote sasa ni ghorofa.

Nikampeleka kwenye nyumba ya Bi. Mruguru, barza ya Mwingereza na Mnazi Mmoja ilipokuwa inafanyika mikutano ya TANU na nikamwonyesha jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na ofisi ya CCM.

Nikamwonyesha hadi ilipokuwa studio ya Mohamed Shebe.

Alichonambia ni kuwa lazima sehemu hizi zote akina Sykes hawa wa leo waweke plaque na waeleze yale ambayo babu na baba zao walifanya.

Jibu langu la haraka kwake lilikuwa kama sheria inaruhusu kwani sehemu nyingine ni za umma mfano Mnazi Mmoja na ofisi ya CCM ingawa wao walishiriki katika ujenzi wao.
 
Back
Top Bottom