Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,912
- 30,253
KINYOZI MWINGEREZA NA BARZA YAKE KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Miaka ni 1950 kuendelea hadi 1960 hapo kwenye hiki kiwanja na hilo jengo alikuwa kinyozi jina lake Muingereza.
Mwingereza "saluni," yake ilikuwa Mtaa wa Kirk Street na Sikukuu chini ya mti.
Muingereza ndiyo alikuwa kinyozi akitunyoa watoto wengi wa Gerezani enzi hizo.
Muingereza alikuwa akitunyoa kwa mkasi na kitana na mbele kaweka kioo kilichoegeshwa kwenye mti uliokuwa ukitoa kivuli mahali hapo.
Sehemu hii imechukuliwa na CCM na inakusudiwa kujengwa ofisi ya chama.
Mkono wa kulia kutoka hapo kama unaelekea Mtaa wa Livingstone ilikuwa nyumba ya Bi. Mruguru bint Mussa, mama yao Abdul, Ally na Abbas Sykes.
Hapa kwa Mwingereza palikuwa na barza ya wana TANU wakikutana hapo kupeana taarifa za harakati dhidi ya Gavana Twining.
Abdul Sykes alikuwa akipita hapo barzani kwa Mwingereza akitokea nyumbani kwake Mtaa wa Stanley kaongozana na Julius Nyerere akienda kumsalimia mama yake Bi. Mruguru.
Zuberi Mtemvu alipounda chama chake cha Congress barza kwa Mwingereza lilishamiri kwa jinsi wanachama wa Congress na TANU wakikutana hapo wanavyoshambuliana.
Mwingereza alibaki hapo akinyoa hata baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 lakini alikuwa haachi kujinasibu kumjua vizuri Nyerere akiwaambia wanaomsikiliza kuwa yeye akimjua sana Nyerere kwani alikuwa akipita pale kazini kwake na Abdul Sykes wakienda kumwamkia kwa Bi. Mruguru.
Mwalimu iko siku alisimamisha msafara wake ghafla akiwa anakwenda kufungua viwanda vidogo vidogo Gerezani alipomuona Bi. Mruguru kasimama na watu wengine pembeni ya barabara Mtaa wa Sikukuu na Lindi akiangalia msafara wa Rais wa Tanzania Julius Nyerere ukipita unasindikizwa na mapikipiki.
Mwalimu alisimamisha msafara wake si mbali na ilipokuwa barza ya Mwingereza.
Mwalimu Nyerere alitoka kwenye gari akaenda kumsalimia Bi. Mruguru.
Hili lilikuwa halijapata kutokea.
Picha: Ilipokuwa barza ya Mwingereza, nyumba ya Bi. Mruguru kama ilivyo sasa na Mtaa wa Lindi nyumba zote za chini zikiwa zimevunjwa na kujengwa magorofa marefu na picha ya mwisho ni Bi. Mruguru bint Mussa.