real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Imeshawahi kuweka kinyongo moyoni? Kinyongo ni hisia ya kutomfurahia, kumchukia au kutotaka kuhusiana na mtu kwa sababu ya mambo yaliyokuudhi.
Kwa ujumla hii ni hisia mbaya sana kwa sababu hutawala akili na moyo kwa muda mrefu. Mara nyingi kinyongo huisha tu pale mtu anaposhawishika kusamehe.
Kuishi na kinyongo ni kitendo cha hatari sana kiafya. Ni kitendo cha hatari kwa sababu husababisha mwili kukusanya tindikali nyingi ambayo mwisho wa siku huathiri utendaji kazi wa viungo mbalimbali vya mwili.
Kinyongo, kama vilivyo vitendo vingine hutumia nishati ya mwili. Nishati ya mwili huzalisha tindikali na kwa kuwa kinyongo ni kitendo ambacho ni endelevu, basi huzalishaji wa tindikali mwilini nao unakuwa endelevu.
Ni vigumu kuelewa ni kwa nini tindikali ni kitu cha hatari sana ndani ya miili yetu, bila kuelezea maana na dhana japo kwa ufupi, tindikali yenyewe na kitu kingine chenye uhusiano wa karibu na kemikali ijulikanayo kama alkali.
Tindikali ni kitu chochote ambacho kinaongeza wingi wa atomu za hewa ya hydrogen zilizobeba umeme chanya katika kimiminika chochote