Kinyesi cha paka kina siri gani kitabibu au kwenye ulimwengu wa kiroho?

Aug 16, 2016
43
56
Wakuu,

Nimeleta hili swali baada ya kufuatilia baadhi ya tiba au vitu vinavyotumika kwenye utabibu/ uchawi au uaguzi kuwa vina fuatana sana na tabia na upatikanaji wake.

Kwa mfano, mwanzoni mwa miaka ya 80, nikiwa kijana mdogo, nilibahatika kukaa karibu na mganga mmoja wa kienyeji maeneo ya Kwa Simsokwe, Busale , Kyela Mbeya. Mganga huyo alikuwa maarufu sana kipindi hicho na amejenga karibu tu na barabara. Sijui kama bado anajishughulisha na hizo kazi au la. Nakumbuka alikuwa anatutuma kutafuta vitu mbalimbali vya uganga na anatulipa pesa.Vitu alivyokuwa anatulipa ni kama vifuatavyo:

1. Wadudu fulani jamii ya beetle, wanachimba vishimo vidogo vidogo kwa kurudi kinyumenyume na hutengeneza kashimo kaliko wazi mithili ya "funnel"kwenye udongo tifu tifu halafu wenyewe hukaa chini wakisubiri wadudu wadogo watumbukie na wao hupata mawindo. Wadudu hawa yule mganga alikuwa anawakausha anachanganya na mizizi na kutibia wanawake walioachwa au waliotelekezwa na wanaume. Mwanaume akiwekewa dawa hiyo kwenye chakula, hujirudi ( kama wadudu wenyewe wanavyotembea kinyumenyume) na kuwapenda wake zao kuliko ilvyokuwa mwanzo!

2. Kuna viwavi fulani hutengeneza viota vyao kwa kujijengea vimiti vilivyozungushwa juu ya utando fulani wa sufi laini. Wadudu hawa hupenda kuninginiza hivyo viota vyao juu ya miti mirefu na hivyo ni adimu sana kupatikana. Sisi tulikuwa tunaenda porini kuvitafuta na tulikuwa tunalipwa hadi shilingi tano kwa kimoja (enzi hizo shilingi tano ilikuwa na thamani sana). Wadudu hawa mganga alikuwa anawakaanga mpaka wanageuka masizi. Halafu yale masizi alikuwa anayachanganya na ndumba zake, na mchanaganyiko huo anautumia kwa watu wenye kutaka bahati. Kwa hiyo uadimu wa mdudu hutibu bahati...kwani bahati nayo ni kitu adimu!!

3.Kuna mmea fulani ukiugusa husinyaa kama vile umekosa maji. Kwa waliosoma Biology watajua kuwa hii ni namna ya mmea kusurvive condition fulani fulani. Mganga alikuwa anatutuma kutafuta majani na mizizi ya mti huu na alikuwa anatumia kwa ajili ya kuongezea ujasiri kwa watu ambao wanapenda wakiongea au kuamrisha kitu fulani waogopwe...nk

Sasa mie nilikuwa madadisi na kila nikitumwa nilikuwa namuuliza mganga kwanini anatafuta vile vitu, na ndo nikapata kujua kuwa kuna uhusiano mkubwa sana wa tabia ya kitu na tiba katika ulimwengu wa kiroho. Sasa kwa mtindo huo huo, leo nimejikuta nataka kujua.

1. Kwanini paka wanafukia mavi yao na hata kama ndani hakuna sehemu ya kuficha kinyesi, basi atakunya kwenye unga au sukari au popote pale atakapoweza kuficha, na huhakikisha amejiridhisha kuwa hayanuki, na wala haonwi?

2. Je kinyesi cha paka chaweza kutumika kama dawa katika ulozi au tiba? Kama ni tiba ni ipi hiyo?

3. Je, kwa tabia ya paka, nimesikia watu wakiagizwa wapeleke paka mweupe kwa mganga na wengine wanasema paka mweusi ni mkosi. Je hutumika kwa ajili gani?

Wakuu akina mshana jr , na wengineo hebu tutafakari kidogo na mtujuze kama mnaelewa lolote....
 
Kwa mujibu wa maelezo yako inaonesha hsya mambo ya kishirikina unayajua na unataka kuthibitisha utafiti wako kwa kulinganisha na majibu utakayopata humu. Rudi kwa huyo mganga wako umuulize au ngoja waje wajuzi naona hata Jf wamo!!
 
Kwa mujibu wa maelezo yako inaonesha hsya mambo ya kishirikina unayajua na unataka kuthibitisha utafiti wako kwa kulinganisha na majibu utakayopata humu. Rudi kwa huyo mganga wako umuulize au ngoja waje wajuzi naona hata Jf wamo!!
Hahaa, mkuu usiogope sana ushirikina. Hata dini zetu tunazoziamini sana ni mambo ya ushirikina tu..ila yataka uzamivu sana kujua kwamba ushirikina ni sehemu muhimu sana ya maisha ya binadamu!!
 
Paka ukikuta/ukiwaona wanagegedana aidha kuna jambo baya linatokea
 
Kwa mujibu wa maelezo yako inaonesha hsya mambo ya kishirikina unayajua na unataka kuthibitisha utafiti wako kwa kulinganisha na majibu utakayopata humu. Rudi kwa huyo mganga wako umuulize au ngoja waje wajuzi naona hata Jf wamo!!
Nami nilitaka nimwambie hivyo hivyo. Mavi ya paka hajayaelezea na hajatuambia kama alikuwa akitumwa na yenyewe ayatafute. Mbona hajauliza mavi ya ng'ombe au mbuzi zaidi ya paka na hakutumwa?
Jamaa anakautafiti kake au ana majibu sasa anataka kuoanisha je yatalingana ama vipi?
 
Back
Top Bottom