Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,745
Pengine hii ni fununu na sio tetesi.
Bila ya hiyana nimeona kukuleteeni habari nilizo zipata kuhusu kinyang'anyiro cha U-Rais wa Zanzibar mwaka 2010 ikiwa kila mmoja na pendekezo lake.
Pendekezo la Rais Jakaya Mrisho Kikwete ni Mohamed Aboud.
Pendekezo la Rais Aman Abeid Karume ni Dr.Shein
Pendekezo la Rais mstaafu Dr.Salmin Amour Juma ni Dr.Gharib Bilal
Pendekezo la Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ni Dr.Hassan Mwinyi.
Wako wengine ambao hawana nguvu kama hao waliopendekezwa vigogo nao ni Ali Juma Shamhuna, Vuai Nahodha, Haroun, na Mansour Yusuf Himid.
Lengo la Rais Kikwete kumpendekeza Mohamed Aboud, ni rais wa Zanzibar mwaka 2010 atoke Pemba(Mpemba) ili kupunguza manung'uniko ya Wapemba na kuuondoa ule aliouita mpasuko, na chuki.
Pendekezo na lengo la Rais Aman Karume kumpendekeza Dr.Shein, linakaribia na la Rais Kikwete, la zaidi ni msimamo wa Dr.Shein nikama msimamo wa Dr.Omar Ali Juma,kwa Wapemba na Pemba kwa jumla.
Pendekezo na lengo la Dr.Salmin Amour Juma, kumpendekeza Dr.Gharib, ni kupingana na pendekezo la Amani Karume, na zaidi
ni mwana mtandao asiyetetereka yuko makini.
Pendekezo na lengo la Ali Hassan Mwinyi kumpendekeza Dr.Hassan Mwinyi, kwanza ni mtoto wake, pili ni kuidhibit zaid Zanzibar, kwani Rais wa Tanzania itakuwa ni M-Bara na Zanzibar ni M-Bara.
Hizo ndio habari zilizopatikana, lakini maswali mengi yalijitokeza hususan kwa pendekezo la Rais Kikwete na Rais Aman Karume, kuwapendekeza Wapemba Dr.Shein na Mohamed Aboud, wakati itikadi ya CCM,M-PEMBA hatawali,hapewi Nchi, hapewi Serikali, leo ilikuwa kuwaje kupendekezwa Wapemba....Mpemba?