Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 6 hadi 8 Februari 2017, Mbunge wa Geita kwa tiketi ya CCM, JOSEPH MSUKUMA amefanya mashambulizi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, PAUL MAKONDA.
Mashambulizi hayo yameanza baada ya kushikiliwa kwa baadhi ya wasanii akiwemo WEMA SEPETU kutokana na kujihusisha na biashara na matumizi ya mihadarati. Vyanzo vya habari vinaonesha kuwa, Tangu WEMA SEPETU awekwe ndani , MSUKUMA amefanya jitihada ya kuwasiliana na Makonda ili aweze kumwachia WEMA kwa madai kuwa kumuweka ndani ni kumdhalilisha na kumvunjia heshima.
Kutokana na MSUKUMA kumshambulia MAKONDA, nililazimika kuingia chimbo ili kubaini chanzo kikuu. Nilijiuliza, je chanzo cha mashambulizi hayo ni WEMA SEPETU kuwekwa ndani ama kuna sababu zingine? Baada ya kuingia chimbo hakika nimebaini mambo makubwa na mazito.
Namhurumia sana mdogo wangu PAUL MAKONDA. Anahitaji kuongeza sala na maombi ili kikombe hiki kimuepuke.Wabaya wake na wabaya wa Raia Namba Moja wamepanga kumshughulikia kwa gharama zozote zile. Mashambulizi haya hayana itikadi za vyama. Wapo wana CCM na wapo wana UKAWA. Ni Mungu pekee ndiye atakayenusuru maisha ya RC Paul Makonda.
1. VITA YA UBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA 2020
Vyanzo vyangu vimebainisha kuwa PAUL MAKONDA ana mpango wa kugombea Ubunge Jimbo la Nyamagana mwaka 2020 kwa tiketi ya CCM. Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na Stanslaus MABULA rafiki mkubwa wa JOSEPH MSUKUMA.
Taarifa za ndani zinasema kuwa ikiwa Makonda ataamua kugombea jimbo hilo, Mabula hana chake. Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa MABULA ameingiwa na hofu kubwa. Hata hivyo, JOSEPH MSUKUMA, amemwambia kuwa kazi hiyo amwachie yeye. MSUKUMA hajawahi na hatakuja kushindwa. Atahakikisha kuwa Makonda anadhalilika na anapotea kisiasa kabla ya 2020.
Bunge litakuwa silaha muhimu ya maangamizi ya Makonda. Tayari maazimio yameshatolewa ili Makonda akajieleze kwenye kamati ya Bunge. Mkakati huo ukishindikana itaitishwa kura ya Kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu ili kumlazimisha achukue hatua dhidi ya Makonda. Mkakati huo ukishindikana mbinu za medani zitatumika.
2. FITINA ZA BENARD MEMBE, NJAA ILIYOINGIA BUNGENI NA KUKOSA PER DIEM YA SAFARI ZA NJE
Benard MEMBE hajakaa kimya kama watu wanavyofikiri. Bado anaendelea na mawindo ili 2020 agombee Urais kwa tiketi ya CCM. Membe hayupo happy kutokana na kusugua benchi tangu Rais Magufuli aingie madarakani.
Wapo vijana wake wanaoratibu mikakati ya kumshughulikia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr JOHN POMBE MAGUFULI. Hata hivyo, vijana hao wanaona hatari iliyo mbele yao kwani Magufuli ni Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Kutokana na hali hiyo, wameadhimia kushughulikia watu walio karibu naye.
Tarehe 7 Februari 2017 kabla ya kuanza vikao vya Bunge, NAPE MOSES NNAUYE, RIDHIWANI KIKWETE, JOSEPH MSUKUMA na wengine watatu ambao sitawataja kwa sababu maalum walikutana mahala ambapo wanapafahamu jirani na Ukumbi wa Bunge kupanga mikakati baada ya sekeseke la vita dhidi ya madawa ya kulevya lililowashwa na Makonda huku baadhi ya maswahiba wao wakiwa wahanga.
Kikao hicho kilipewa msukumo na simu iliyopigwa na BENARD MEMBE Jumapili tarehe 5 Februari 2017 kwenda kwa Nape akimtaka watumie mwanya huo kumsulubu Rais kupitia Makonda.
Sambamba na fitina za MEMBE, inadaiwa kuwa wabunge hasa waliokuwepo Bunge lililopita wanalalamika kuwa wana njaa kutokana na Sera ya Rais kubana matumizi. Pia uamuzi wa kudhibiti safari za nje umewafanya wabunge waishi maisha ya dhiki hasa ikizingatiwa kuwa wana mikopo mingi kwenye taasisi za kifedha.
Hata hivyo, wabunge hao wanaona kuwa hawana power ya kumshughulikia Rais Magufuli moja kwa moja na badala yake wameazimia kudeal na matawi yake. Wabunge hao wanamuona Makonda kama mtu wa Rais Magufuli kutokana na kuungwa mkono harakati nyingi anazofanya ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa Silaha, kusikiliza kero za wananchi na hili la madawa ya kulevya. Mkumbuke kuwa hapo awali kulikuwa na malalamiko kuwa Makonda anaingilia kazi za Mawaziri.
3. CHUKI ZA ANDREW CHENGE DHIDI YA RAIS MAGUFULI
Msidhani kuwa haya mambo yanaenda kienyeji. Hapana. Ni mkakati uliopangwa na ukapangika. Mtoa habari wangu aliniuliza swali, je unajua kwa nini Chenge aliongoza kikao cha Bunge tarehe 8 Februari 2017?
ANDREW CHENGE hana furaha kwa Magufuli kuwa Rais. Kwanza alikataa kumnadi wakati wa kampeni kwa madai kuwa ni fisadi. Pili Rais alikataa kumpa mkono. Tatu hajamteua nafasi ya uwaziri. Chenge anaona kuwa sehemu pekee ya kumsulubu Rais Magufuli ni kutumia kiti cha Spika ambapo yeye ni Mwenyekiti wa Bunge.
Ndivyo ilivyotokea tarehe 8 Februari ambapo kiti cha Spika kikikaliwa na Chenge ndicho kilichoruhusu mjadala wa Makonda Bungeni na kupelekea maazimio 4 ikiwemo kumtaka Makonda ajieleze mbele ya kamati kutokana na kauli yake kuwa Wabunge wakati mwingine wanasinzia bungeni hivyo anatakiwa mchekeshaji ambaye atawachangamsha.
4. MSUKUMA NI MWANA CCM ASIYE NA MAPENZI KWA RAIS MAGUFULI
Msukuma ni swahiba mkubwa wa EDWARD LOWASA. Uswahiba wao ulipungua baada ya LOWASA kuhamia CHADEMA. Hata hivyo, wakati Rais MAGUFULI anasaka wadhamini ndani ya CCM, alipofika mkoa wa Geita, aliambiwa kuwa wanachama wote wa CCM wamemdhamini LOWASA.
Pia MSUKUMA alificha mihuri yote ya CHAMA ili Rais asiwe na wadhamini ndani ya mkoa huo. Alifanikiwa kwa kiasi chake. Hata hivyo mkakati huo ulishindwa baada ya jitihada zilizofanywa na watu muhimu ambao kwa hapa sitawataja.
Kwa ufupi ni kwamba, MSUKUMA hampendi na hamuungi mkono Rais Magufuli. Siku moja alisikika akisema kuwa kama angekuwa yeye ndo mwenye Maamuzi ndani ya CCM, Rais MAGUFULI asingeruhusiwa kugombea tena mwaka 2020
5. MAHUSIANO NA WAFANYABIASHARA WA MADAWA YA KULEVYA
Fuatilieni wanaomshambulia Makonda kwa sasa. Ni wale wale. Ama wenyewe wanajihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya ama maswahiba wao wapo kwenye orodha ya Makonda ya awamu ya kwanza na ya pili. MSUKUMA=WEMA SEPETU, HALIMA MDEE, CHENGE=YUSUPH MANJI, NAPE=WEMA SEPETU. Is not a joke.
Nimalizie kwa kumsihi MAKONDA. Ikiwa utaamua kurudi nyuma katika vita hii maana yake ni kwamba umeridhia mkoa wa Dar es Salaam kuwa kituo cha mateja. Maji umeyavulia nguo sharti uyavue. Si kila mtu anaweza kuwa na ujasiri wa kuwataja Mapapa wa Madawa ya Kulevya kama Manji, Mbowe, Idd Azan nk. Umeleta tetemeko na mshtuko mkubwa. Hakuna mtu alitaraji kuwa utakuwa na ujasiri huo. Walidhani utaishia kuwataja mateja tu.
Wabaya wako wamedhamiria kukuangamiza kimaisha na kisiasa. Endelea kumuomba Mungu kwani dhamira yako ni njema. Watanzania tunakuunga Mkono kwa asilimia zote. Vita dhidi ya Madawa ya kulevya haijawahi kuwa nyepesi kote duniani kwa vile inahusisha watu wenye pesa. Baadhi ya nchi wale wote wanaothubutu kupambana na biashara hiyo huuawa. Sikutishi. Ila kwa vile umeamua kujitoa mhanga, naamini kuwa utashinda majaribu yote.
Wito kwa chama changu CCM, tumedhamiria kuondoa maovu yote chamani na katika nchi hii ikiwemo madawa ya kulevya na ufisadi. Tusiwe sehemu ya kuwakatisha tamaa wale wanaothubutu. Tuwaunge mkono na tuwatie moyo. Tuchukue hatua dhidi ya wale wanaokwamisha vita hizi.
Wito kwa Bunge. Naomba sana wabunge. Tusiwe na bias. Pale wenzetu wanapoguswa na kashfa yoyote, tusitafute mpenyo wa kuwatetea. Mhalifu ni mhalifu tu. haijalishi mahali alipo. Hii tabia ya kukumbatia wahalifu itatumaliza.
Wito kwa Rais MAGUFULI. Walinde wale wote wanaokusaidia katika mapambano mbalimbali. Wewe ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Tumia vyombo vyako kuwalinda vijana wako dhidi ya vitisho kama vya akina MSUKUMA ambaye amesema wabunge wamuachie suala la MAKONDA kwani anammudu na atapambana naye mtaani.
Huwezi kujua amejipanga kupambana na MAKONDA kwa kutumia silaha gani. Makonda akifa leo au kesho kwa kifo cha kutatanisha, MSUKUMA awe wa kwanza kuwajibishwa.