Kinondoni wamkumbuka Idd Azan

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wakuu za asubuhi? Jana nilikuwa Kinondoni maeneo kadhaa, ikiwemo Mkwajuni, baadaye Vijana pale.

Pale Vijana, nilikuta baadhi ya wakazi walikuwa wakijadili kuwa, upinzani usingeshinda ubunge wa jimbo hilo 2015 kama siyo yale mafuriko ya Lowassa aliyehamia Chadema kutoka CCM na kuuimarisha Ukawa.

Walisema kuwa, baadaye Mbunge aliyeshinda kupitia Cuf alijitoa na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi na kisha kushinda ubunge wa marudio kupitia CCM.

Wakasema pamoja na hayo, wanaamini Mbunge aliyekuwepo mpaka 2010, Idd Azan alikuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Jimbo hilo.

Walisema Azan alikuwa akiwasaidia katika shida binafsi, hasa wanawake wajane, wakongwe na wazee wasio na kipato.

Wamesema hata kama Mbunge wa sasa amejitahidi kuleta maendeleo, lakini Azan naye alifanya mazuri yake ambayo wapiga kura bado wanamkumbuka.

Mzee mmoja aliyejitaja kwa jina la Kisangi alisema amewahi kwenda kumlilia Azan shida ya ada ya mtoto wake nyumbani kwake, Tandale Kwa Bibi Paka akakuta wananchi kubao nje wakitaka msaada na mbunge huyo aliwasaidia.

Walisema kipindi cha Azan michezo ilibamba sana jimboni humo kuliko wakati mwingine wowote.

Nilichojifunza, wananchi wanajali sana mtu anayewasaidia kwa shida binafsi za kimaisha.
 
Hicho kijiwe mlikutana wenye fikra fupi.

Ule uchaguzi mlikimbia na masanduku ya kura, mkuu wa mkoa, wa wilaya, OCD wote wakajazana kwenye chumba cha kuhesabia kura, halafu bado mnaamini CCM walishinda kihalali?!
 
Mtoa Uzi wewe ni bonge la fala hakuna mbunge aliyeua vijana kama idi azani kwa kuwapaa madawa ya kulevya bure.

Hata huyu aliyopo sasaiv ni kilaza hakuna kitu.
 
Wakuu za asubuhi? Jana nilikuwa Kinondoni maeneo kadhaa, ikiwemo Mkwajuni, baadaye Vijana pale.

Pale Vijana, nilikuta baadhi ya wakazi walikuwa wakijadili kuwa, upinzani usingeshinda ubunge wa jimbo hilo 2015 kama siyo yale mafuriko ya Lowassa aliyehamia Chadema kutoka CCM na kuuimarisha Ukawa.

Walisema kuwa, baadaye Mbunge aliyeshinda kupitia Cuf alijitoa na kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi na kisha kushinda ubunge wa marudio kupitia CCM.

Wakasema pamoja na hayo, wanaamini Mbunge aliyekuwepo mpaka 2010, Idd Azan alikuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Jimbo hilo.

Walisema Azan alikuwa akiwasaidia katika shida binafsi, hasa wanawake wajane, wakongwe na wazee wasio na kipato.

Wamesema hata kama Mbunge wa sasa amejitahidi kuleta maendeleo, lakini Azan naye alifanya mazuri yake ambayo wapiga kura bado wanamkumbuka.

Mzee mmoja aliyejitaja kwa jina la Kisangi alisema amewahi kwenda kumlilia Azan shida ya ada ya mtoto wake nyumbani kwake, Tandale Kwa Bibi Paka akakuta wananchi kubao nje wakitaka msaada na mbunge huyo aliwasaidia.

Walisema kipindi cha Azan michezo ilibamba sana jimboni humo kuliko wakati mwingine wowote.

Nilichojifunza, wananchi wanajali sana mtu anayewasaidia kwa shida binafsi za kimaisha.
Ni ujinga kuleta uzi wa kusifia mbunge kusaidia mtu shida zake binafsi, hio sio kazi ya mbunge. Ndo nyie mnamuomba mbunge barabara.
Sema tu unampigia debe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom