Kinondoni: Waliobomolewa nyumba zao waanza kulipwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Baadhi ya waliobomolewa nyumba zao ili kupisha upanuzi wa barabara jijini Dar Es Salaam chini ya mradi wa DMDP wameanza kulipwa fidia zao hivi leo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyozinduliwa jana na Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda.

Zoezi hilo limeanza kufanyika hivi leo katika ofisi za Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Mthamini wa majengo wa Manispaa Bwana Einhard Chidaga ambapo ameeleza kuwa katika halmashauri ya Kinondoni barabara 11 ndizo zilizohusishwa na kati ya hizo barabara tano zimeanza kujengwa katika awamu ya kwanza kutokana na kutokua na kikwazo cha fidia na barabara sita zimechelewa kujengwa kutokana na hatua za ulipwaji wa fidia, barabara hizo ni pamoja na Makanya, Tandale kisiwani, kilimani pamoja na barabara ya kilongawima.

Aidha Bwana Chidaga ameeleza ameeleza kuwa zoezi hili halitawahusisha kwa sasa wale wote wasiokuwepo kwenye barabara hizo sita na badala yake watalipwa katika awamu itakayofuata na kuongeza kuwa zoezi hili ni endelevu mpaka septemba 15 ulipaji wa fidia utakuwa umekamilika kwani wakandarasi wameshapatikana na wanatarajiwa kuanza kazi mwezi Oktoba 2017.

Sambamba na hayo Mthamini majengo ametoa wito kwa wananchi kwa kuwataka watulie na wajaribu kua makini na wafuatilie matangazo na maelekezo yanayotolewa na serikali ili kuepusha changamoto na usumbufu utaoweza kutokea. Hata hivyo wananchi kwa upande wao wameipongeza na kuishukuru serikali kwa hatua ulipofikia mradi huo.
 
Ngoja na mie nikae mkao wa kula maana na nilikuwa na kibanda cha urithi panda izo
 
Back
Top Bottom