Kinondoni: Mhandisi Natty atua Dar es Salaam, ana lundo la nyaraka

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Mhandisi Mussa Natty, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kinondoni, ametua Dar es Salaam tayari kwa uchunguzi dhidi yake. Mhandisi Natty, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Babati kabla ya kusimamishwa kupisha uchunguzi,ameshakusanya nyaraka za kutosha na kutisha za kujibu tuhuma dhidi yake. Yuko tayari.

Mhandisi Natty anasubiri tarehe husika ya kuitwa na kuhojiwa ili auanike ukweli wa sakata la tuhuma dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuuzwa kwa ufukwe wa Coco pamoja na ujenzi wa kifisadi wa barabara mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni. Mhandisi huyo yuko tayari kujinasua na kuwanasa wahusika hasa.

Kubenea ameanza, Natty atamaliza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Mbona mnahangaika naye sana huyo Natty.
Si msubiri akatoe huo ukweli ,tujue mbivu na mbichi.
 
DC Daudi Bashite pressure inapanda, pressure inashuka.

Wewe Daudi wewe! Unadhani wajina wako Daudi Bashite ana hofu? Yule aliyekuwa anambeba na kumfungia viatu bado anakumbukumbu za mahaba ya Daudi hivyo akiletewa za kuleta atamtetea kwa "baba" ambaye naye kupitia KK watatoa maagizo kama yale ya Baraza.
 
Kwa hiyo mnatishia nyau nani?

Alikuwa wapi siku zote kuzitoa?

Lakini si hoja.Swala ni katika utekelezaji wa hiyo mikataba je alitenda sawa? Kama aliona kuna upungufu je alishauri mamlaka husika ziangalie upya au aliamua kupelekapeleka tu bora liende?

Mikataba hata kama ilisainiwa miaka sitini iliyopita kazi iko kwa mtekelezaji akiona siyo ndivyo kama msomi na mtaalamu lazima abonyeze alarm kama hakufanya hivyo hilo zigo lake ataliongezea kwenye hilo zigo la nyaraka alilobeba.
 
Zikitimia 40 atatafuta pa kutokea ...ana sifa sana huyo jamaa na kiburi cha mafisadi wenzake
 
Duh afavali aje maana tumeulizana sana inakuwaje maji yanapita pembeni ya kalavati badala ya kupita katikati
 
Nimesha kaa kwenye kiti mbele ya tv na popcorn zangu nangoja movie ianze. Ingependeza kama hii issue ingewekuwa " public inquiries" kwani wananchi wangeweza kuona ukweli upo wapi.
 
Aisee, hapo patamu sana ngoja tusubiri

Ukimnyonga mtu bila kupata pesa inakusaidia nini? Tanzania inataka kupata pesa yake ndani ya muda mfupi kuliko China.Ujue mtu akikwepa kodi china kesi hizo huchukua muda mrefu mno sio hizo siku saba yaweza kuwa hata mwaka.Pesa serikali inakuwa haijapata inahangaika tu na kesi tu. Magufuli anatoa siku saba tupe chetu vinginevyo unafilisiwa na kwenda Jela.Tanzania kazi yetu si tu ku-COPY na KU-PASTE ndio maana tunaitwa Tanzania wale wanaitwa CHINA

Si kila kitu unaiga china..China watu wengi mno kupunguza population njia moja ni hiyo ya kunyonga nyonga watu.Hata ukitapeli kitanzi.
 
Wewe Daudi wewe! Unadhani wajina wako Daudi Bashite ana hofu? Yule aliyekuwa anambeba na kumfungia viatu bado anakumbukumbu za mahaba ya Daudi hivyo akiletewa za kuleta atamtetea kwa "baba" ambaye naye kupitia KK watatoa maagizo kama yale ya Baraza.

huyo shosti wa DC Daudi Bashite alienda ikulu juzi bwana Pombe akawaambia walinzi wamtimue coz hamjui yeye anamjua Baba yake tu.
Nguzo za DC Daudi Bashite huko Ikulu zimeshavunjwa.
 
Mhandisi Mussa Natty, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kinondoni, ametua Dar es Salaam tayari kwa uchunguzi dhidi yake. Mhandisi Natty, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Babati kabla ya kusimamishwa kupisha uchunguzi,ameshakusanya nyaraka za kutosha na kutisha za kujibu tuhuma dhidi yake. Yuko tayari.

Mhandisi Natty anasubiri tarehe husika ya kuitwa na kuhojiwa ili auanike ukweli wa sakata la tuhuma dhidi yake ikiwa ni pamoja na kuuzwa kwa ufukwe wa Coco pamoja na ujenzi wa kifisadi wa barabara mbalimbali katika Manispaa ya Kinondoni. Mhandisi huyo yuko tayari kujinasua na kuwanasa wahusika hasa.

Kubenea ameanza, Natty atamaliza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ningeliuwa yeye namwaga mboga tu. Kwa nini watu baadhi waburuzwe wakati wakubwa wapo na hawaguswi?
 
Back
Top Bottom