Kinondoni kutawala nchi si sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinondoni kutawala nchi si sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Netanyahu, Sep 9, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna mdau aliniletea taarifa za kutisha kuhusiana na wilaya ya kinondoni mkoani Dar es salaam.Akaniambia wagombea wote wa Uraisi wa vyama vyote vya siasa wana nyumba na makazi yao ya kudumu wilaya ya Kinondoni.Mawaziri na manaibu waziri karibu wote wana makazi yao na nyumba zao za kudumu wilaya ya kinondoni.

  Asilimia zaidi ya tisini ya wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania wana nyumba na makazi ya kudumu wilaya ya kinondoni.Wanachofanya uchaguzi ukifika ni kujiondokea kwenye vijiwe vyao kwenye majumba yao ya fahari wilaya ya Kinondoni na kusambaa nchi nzima mawilayani kwenda kuwazuga wananchi huko kwenye mawilaya mikoani wawape kura wakaendelee kujilia vyao Kinondoni.

  Hivi huko mawilayani kwenye majimbo ya uchaguzi hakuna wakazi wa kudumu waishio huko ambao maisha yao ya mwaka mzima huwa huko wawezao kuteuliwa kugombea huko

  Hivi ni lazima mgombea awe mkazi wa kudumu wa kinondoni aliyejenga na kuishi kinondoni? Na hivi ni lazima wagombea wengi wanaoteuliwa kugombea ubunge na kupewa viti maalum vya ubunge ni lazima wawe wakazi waliojenga nyumba na wanaoishi kinondoni?

  Makatibu wakuu wa mawizara nao ni hivyo hivyo kama huna nyumba na si mkazi wa kinondoniuwezekano wa kuteuliwa ni mdogo maana nao asilimia kubwa ni wakazi wa kudumu wenye nyumba kinondoni.

  Hivi ni lini serikali itateua mawaziri wa kutoka wilayani ambao makazi yao na nyumba zao za kudumu ziko kule na mwaka mzima huishi kule kuwa mawaziri au manaibu mawaziri? Au tuseme wilaya ya kinondoni ndio kuna watawala na wabunge wazuri kuliko wilaya zote za Tanzania ndio maana inapewa nafasi kubwa? Hata wakuu wa mikoa asilimia zaidi ya tisini ni wakazi wenye nyumba na makazi ya kudumu wilaya ya kinondoni.Hivi kinondoni kuna siri au umamuluki gani

  Ni lini vyama vya siasa vitapata wenyeviti wasio wakazi wenye nyumba na makazi wilaya ya kinondoni?

  Bunge letu halina nguvu kubwa ya kukemea mafisadi sababu mafisadi ni wakazi wa wilaya ya kinondoni na wabunge wengi nao ni wakazi wa kinondoni na serikali kwa sehemu kubwa wenye nafasi nyeti wanatokea kinondoni basi hawatafunani maana masingasinga hawa wa kinondoni hufahamiana kwa vilemba ndio maana mifisadi inaendelea kutanua na hakuna wa kuigusa kwani ni timu yao ya kulewa pombe kinondoni

  2010 inakaribia na tutaona tena wakazi wenye nyumba na makazi yao kinondoni wakiwemo akina Lowasa ,Rostam Azizi na wengineo wakikurupuka kutoka kinondoni kwenye mahekalu yao wakikurupuka kwenda kutafuta ubunge huko kwa waliolala wakazi wa kudumu kwenye mijimbo ya uchaguzi mawilayani huku wakilindwa na vyama vyao vilivyoapa kuhakikisha kinondoni ndio itaongoza kutoa wagombea ubunge na viongozi wan chi.

  Anyway nadhani siasa za nchi zinatakiwa mabadiliko lakini mabadiliko yatakuwa ni magumu kama chi itaendelea kushikiliwa na wakazi wa kinondoni kuanzia bunge,serikali na majaji,majeshi yote.Sidhani hata kiusalama kama ni sahihi kulundika watu wengi kwenye nafasi nyingi za juu na nyeti ambao ni wakazi wa kudumu wa eneo moja.

  Wadau naomba kutoa hoja kwenye bunge huria la Jamii Forum
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Good analysis. Ni ukweli mtupu
   
 3. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hee nami nina nyumba kunduchi kumbe mi ni kiongozi!!!teh teh teh..
   
 4. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Analysis nzuri.

  Kwa hiyo tusitegemee kuendelea, kwa sababu katikati manispaa ovyo kuliko zote ni Kinondoni na huko ndio viongozi wenu wanakotoka.

  Haya bwana.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  na ubaya ni huu, hata tukimteua mtu toka Tunduru awe katibu mkuu wa wizara yetu fulani akifika dar ana kaa kidogo Temeke kwa jamaa zake na baadae anahamia Kinondoni. Hata mbunge wetu amehamia kinondoni na kuacha nyumba yake Segerea.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo hata macd wana nafasi ya kuja kuwa viongozi...?
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nentanyahu (jina kali by the way) hapo umeshindilia msumari ndiiii,maana JK,Mzee wa Kiraracha Mrema, Freeman Mbowe, Lipumba ni kweli wote ni wakazi wa Kinondoni na wote wana ambition ya kukamata inji hii(of course JK ye tayari).
   
 8. m

  mtanzaniaraia Member

  #8
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo siyo kuwa wakazi wa kinondoni,tatizo baada ya kuwa viongozi wanafanya juhudi gani za kuendelezamaeneo mengine hasa ya maeneo yao wanakotoka?
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Hivi, unakoishi ni sehemu ya sifa za kuchaguliwa kuwa kiongozi?
   
 10. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinondoni bado ina maeneo mengi tu, na hujazuiwa kuishi huko pia! Ina maana wangekuwa wana makazi Temeke hata kama ni wabunge wa majimbo ya mikoani isingekuwa ishu kwako? Au pointi yako ni ipi hasa?
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba hata mimi napendelea kinondoni only kwa sababu ya maandari yake nzuri, Kinondoni not environmentaly poluted compared to Ilala na Temeke!!! Nani anataka kufa kwa kansa za koo kwa mimoshi ya viwanda??? Hali ya Beach beach pia ni murua jamani, yaani ka upepo mwanana muafaka kabisa. Kinondoni hata watoto wangu wote watakuwa na makazi huko!!!!! Kama nina nyumba Ilala na temeke ni za biashara!!!!
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ni kweli kabisa ila kuna haja ya kuwa na mikakati ya kupanua jiji kwa nje ya mji na sio Kinondoni
   
 14. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi hata Msasani kwa Nyerere na Warioba pia ni Kinondoni?
   
 15. moto ya mbongo

  moto ya mbongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 336
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  Utafiti uloufanya kuhusu watu kuishi Kinondoni sioni kama kuna tatizo kwani ni kati kati ya jiji.

  Ukichunguza zaidi utagundua kuna maeneo mengine yanapendwa kama vile Kwa Komba,Kibaha Maili 1, Mafinga na kwingineko.

  Cha muhimu wawatumikie wananchi wasibaki kuwakimbia na kwenda pindi kampeni zinapokaribia.
   
 16. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,357
  Likes Received: 3,120
  Trophy Points: 280
  kwa kuwa ikulu haipo kinondoni basi waache wenyewe warundikane huko.........tunawakaribisha wilaya ya temeke kuna viwanja vingi tu na bei ndogo......
   
 17. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,734
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Mi nafikiri kuwa kama asilimia 60 ya viongozi wa juu wa nchi hii wanatoka wilaya kinondoni basi wilaya hiyo ilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa USAFI,USALAMA,MIUNDO MBINU YA BARABARA,MAJI TAKA NA SAFI, MAWASILIANO, NIDHAMU NA MENGINEYO lakini kinondoni ndio imekuwa inaongoza katika uchafu, wizi,utapeli hasa wa viwanja,ukahaba,zinaa, nk humo ndio viongozi wetu wanapoishi. mamlaka zilizopo zinawatukuza viongozi kiasi cha kwamba hawajui madudu na bugudha wanazozipata wananchi wa kawaida.
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mwingine akisema Wizara karibu zote, Ikulu maofisi makubwa yapo wilaya ya Ilala utasemaje?

  Nchi nyingi huwa na residential district / section kwa viongozi e.g, Oysterbay (although I hear it is increasingly going to the dogs), ambako viongozi wengi pamoja na diplomatic corps hukaa, hivi utasema hizi districts ndizo zinatawala nchi?

  Tukiendekeza hivi tutafikia kulalamika mpaka kusema kwa nini samaki wote wanapatikana majini.

  Cha kufanya ni kuhakikisha standard of living ya sehemu zote inakuwa acceptable.Kwangu mimi swali si kwamba mbona viongozi wote wanakaa wilaya ya Kinondoni, swali ni kwa nini Wilaya ya Temeke haina huduma muhimu.

  Kama alivyosema Jiwe, hii mentality ya kwa nini isituletee moyo wa kutaka kulogana -this is essentially what this is- bali tuwe na ambition ya ku achieve.

  Muandishi amefanya causative link sehemu ambayo haipo, ameona kama kukaa Kinondoni ni requirement ya uongozi, wakati if anything, kukaa Kinondoni kunaweza kuwa ni matokeo ya uongozi.

  Bottom line ambayo muandishi ame i squander, ni kwamba sehemu zote ziwe na miundombinu inayoruhusu maisha bora.
   
 19. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Netanyahu,

  Karibu
   
Loading...