heshima nicholaus
Member
- Dec 26, 2011
- 16
- 3
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Boniface Jacob wakati kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo Sekondari Tanzania (UMISETA) kwa Wilaya ya Kinondoni yaliyofanyika shule ya SekondariMakongo leo Jumapili 22/5/2016,ikiwa zimeshirikishwa shule kutoka Majimbo matano ya Dar es salaam.
Akiongea Mstahiki Meya amesema Halmashauri inapambana kurudisha maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na matajiri ili vitumike kwa ajili michezo katika kukuza vipaji vya vijana katika Manispaa ya Kinondoni.Amemtaka Afisa elimu Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni kuangali viwanja ambavyo vimeharibika achukue greda la Manispaa lipo viwanja vichimbwe ili vijana wacheze kwenye viwanja vyenye hali nzuri.
"Tulikuwa na mazungumzo na waziri viwanja virudishwe kwa wananchi mfano uwanja wa KIFA na UFI, vijana wapate maeneo ya kucheza, tukianza leo kuweka msisitizo katika michezo usishangae 2030 kuwaona vijana wetu wanashiriki kombe la dunia au vipi wanamichezo?" Amesema Mstahiki Meya.