Kinondoni, Dar: Yaliyojiri kwenye mkutano na wa Wanahabari na viongozi wa vyama 8 vya siasa


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,178
Points
2,000
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,178 2,000
Leo Jumatatu, Aprili 15, 2019, Viongozi Wakuu wa Vyama 8 vya Siasa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, watakuwa na mkutano wa waandishi wa habari utakaofanyika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA, Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Vyama 8 vya Siasa ni (NCCR-Mageuzi, ACT-Wazalendo, NLD, CHAUMMA, CCK, UPDP CHADEMA na DP) .


Viongozi wa vyama nchini wamekutana leo na waandishi wa habari kutoa tamko kuhusu yanayoendelea nchini.


=========

UPDATES:


VIONGOZI WA VYAMA NANE VYA UPINZANI WAKIONGOZWA NA MBOWE WAPINGA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Sisi, Viongozi wa vyama nane vya siasa, baada ya kukutana na kufanya majadiliano ya kina kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini, kwa umoja wetu tumefungua kesi katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga sheria ya vyama vya siasa namba 1 ya mwaka huu 2019, ambayo kama mnavyojua imeanza kutumika rasmi mwaka huu baada ya muswada wa sheria hiyo kupitishwa na Bunge mwaka jana, ukatiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli tarehe 13 Februari, 2019 na kuchapwa kwenye Gazeti la serikali la Februari 22 mwaka huu wa 2019.

Vyama 8 vya siasa kwa umoja wetu tumefungua kesi Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) kupinga Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 1/2019, kesi hiyo imesajiliwa na imepewa Na. 3/2019, walalamikaji wakiwa ni mimi @freemanmbowetz na wenzangu wa 4 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania.
Sheria hiyo pamoja na kupigiwa kelele na wadau mbalimbali wa nje na ndani ya nchi, vyama vya siasa, asasi za kiraia, mashirika ya dini, vyama vya wanataaluma na wapenda demokrasia kuwa sheria hii ni mbaya na haifai bado wabunge wa Ccm waliupitisha muswada huo baadae kutiwa saini na Rais.

Kwa bahati mbaya maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali, hata mabadiliko ambayo yalipendekezwa na Kamati ya bunge ya sheria na katiba bado katika hatua ya mwisho ya kupitisha muswada ule ulipitishwa kama Serikali ilivyotaka bila kujali maoni ya wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa.

Katika nchi yetu kuna weza kuwa na kiburi na jeuri ya viongozi wetu kwamba wao wanachokitaka lazima kiwe bila kujua Watanzania au wadau wengine mbalimbali wanalalamikia nini au wana maoni gani kuhusu mambo mbalimbali katika nchi yao.

Sheria ya vyama vya siasa Na. 1/2019 iliyosainiwa na Rais tarehe 13 mwezi Februari mwaka huu wa 2019, ni ya kunyonga vyama vya siasa, sasa ni sheria rasmi, jambo hili limetusikitisha sana tunaona jinsi gani demokrasia inavyokwenda kufa katika nchini. Yani wale washindani wetu ndiyo wanakwenda kuwa waamuzi wa hatima ya vyama vyetu vya siasa, tumelazimika kuitafuta haki katika Mahakama ya Afrika Mashariki kutokana na ukweli sheria hiyo ni mbaya, imetungwa kwa nia mbaya inafanya shughuli za siasa kuwa jinai.

SEHEMU YA 2

Tumeitaka Mahakama ya Afrika Mashariki kuingilia kati na kuzuia sheria hii kutumika na itangaze sheria Ile na batili inayokiuka vifungu vya 6/7 na 8 vya mkataba wa ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa hiyo vyama 8 tumefungua kesi hii kupitia kwa viongozi wetu.

Tumepeleka kimsingi mambo mawili Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) - La kwanza kuipinga ile sheria kwamba inakiuka misingi ya ujenzi wa demokrasia katika nchi yetu na Mahakama ya Afrika Mashariki ina mamlaka ya kuingilia kati na kuitafsiri ile sheria kuamua itumike au isitumike.

Jambo la pili tumeomba kwa kipekee EACJ iizue Serikali ya Tanzania kuendelea kuitumia ile sheria hadi hapo hilo suala la msingi litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi, hilo ni jambo ambalo tunalipinga na tumeitaka Mahakama ya Afrika Mashariki ( EACJ) isimamie haki na ione haki inatendeka.

Tunaona ni kwa jinsi gani demokrasia inavyokwenda kuminywa, mshindani wetu hataki mbinu halali za kushindana kwa hoja, sera za kisiasa, wanatunga sheria kwa kutumia wingi wa wabunge wa ccm ndani ya bunge kutengeneza sheria ambazo zinawaumiza Watanzania wakiwemo Ccm wenyewe.

Vifungu ambavyo vimekiukwa ni vingi, vipo vifungu zaidi ya 12 ambavyo tunavilalamikia katika sheria ile ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa, kwa hiyo Serikali imepewa siku 45 kujibu malalamiko yetu.

Fikiria 2019 tuna uchaguzi wa serikali za mitaa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameharamisha shughuli za vyama vya siasa kwamba viongozi wote hawa wa vyama vya siasa, ambao sio wabunge na madiwani hawawezi kufanya uenezi wa vyama vyao alafu serikali hii hii inatangaza uchaguzi.

Na Waziri Mkuu anasimama bungeni bila aibu anasema tutakuwa na uchaguzi mwishoni mwa Oktoba mwaka 2019 wa serikali za mitaa,hawa wadau wa siasa wamezuiwa kufanya siasa, Rais anakiuka Katiba anasema wenye ruhusa kufanya siasa ni wabunge na madiwani kwenye maeneo yao. Aliyemwambia Rais na CCM kuwa miliki ya siasa za nchi iko mikononi mwa wabunge na madiwani ni nani? Kwamba wao tu ndo waruhusiwe kufanya siasa katika maeneo yao, huu ni uvunjaji wa Katiba, hivi wanategemea tunakwenda kwenye uchaguzi kwenye mazingira gani? .

SEHEMU YA 3

Miaka 4 vyama havijajijenga, vyama vya siasa vinajijenga wakati wote kisera na kimuundo, bora Chadema tuna madiwani na wabunge kidogo tunaweza tukafanyafanya siasa na sio maeneo yote viongozi sisi wa Chama hatuwezi kufanya siasa zaidi kwenye majimbo yetu.Tunakabiliwa na matatizo makubwa ya udikteta ambao unanyemelea taifa, maamuzi ambayo yanadharau katiba, wale waliopewa dhamana ya uongozi wamejigeuza miungu watu; Spika analigeuza bunge kama ni chombo chake binafsi hataki kusikiliza mawazo ya wabunge.

Bunge linavyoendeshwa sivyo,ni mali ya watu, kwa hiyo sisi kama wabunge wa Upinzani na mimi kama Kiongozi wa Upinzani haya mambo yanayozungumzwa na Spika hayakuwa maazimio ya bunge ,bunge halijamtuma CAG akazungumze na Rais.
Tuko kwenye bunge la bajeti ambalo lina mambo makubwa ya kujadili mapato na matumizi ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha lakini tunachukulia mjadala wote huo kwa utashi wa mtu, sio azimio la bunge ni mtu ametoa maoni yake, tuwaache watu waseme.

Serikali iruhusu vyama hivi sasa vikafanye siasa maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa sio zile siku tu za kampeni, vyama vinahitaji kujipanga,vitajipangaje? wao wanazunguka nchi nzima na magari ya serikali kwa gharama za serikali ndege za serikali wanajieneza wao.

Wanatumia magari ya serikali, ndege za serikali kwa gharama za serikali, vyombo vya habari vya umma wamefanya vyao wanajieneza wao, vyama vyama vya Upinzani wamevifunga kamba wanatangaza uchaguzi wa serikali za mitaa wanataka tuingie kwenye uchaguzi kwa kampeni kwa siku 7.
fb_img_1555365359711-jpg.1072556

fb_img_1555365499914-jpg.1072558fb_img_1555365505680-jpg.1072559
 
Blessed

Blessed

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2011
Messages
2,811
Points
2,000
Age
32
Blessed

Blessed

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2011
2,811 2,000
Okay! tupe updates mkuu!
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,929
Points
2,000
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,929 2,000
hahahah Zitto wanakuona wa maana siku hizi, wanakuvuta vuta!!!!
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,185
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,185 2,000
Wapenda unyonyaji habari hii ya vyama kutoa tamko la pamoja hawatataka kuisikia kabisa, wanataka turudi kwenye chama kimoja cha siasa ili waendelee kubwiya, wakifa wawarisishe na watoto wao kubwiya...wakifa wawarishe pia watoto wao.... yaani kama ule ukoo wa ....... ; Baba, Mama, Mtoto, Mjukuu, Vitukuu wotee ......
 
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2015
Messages
2,847
Points
2,000
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined May 18, 2015
2,847 2,000
Haahaa naona kila mtu anauliza vipi hawajavamiwa?.....Inaonekana ni kawaida wakivamiwa na polisi lakini itaonekana si kawaida endapo wasipovamiwa haahaa This is tz
 
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
12,558
Points
2,000
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
12,558 2,000
Kwenye hicho kikao, ACT sio ndio kikubwa kwanini Mbowe awe Mwenyekiti wa kikao badala ya Zitto, hii sio sawa, wakianza kuvurugana polisi hawako hapo shauri yao..
 
K

KIBST

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2017
Messages
500
Points
1,000
K

KIBST

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2017
500 1,000
Watupe kwanza mrejesho wa kile kikao walicho keti ZANZIBAR na KUJA NA TAMKO YA ntoke vipi 2019.....
Vinginevyo ni UZUZU tu kuwasikiliza hawa.....
 
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2008
Messages
12,718
Points
2,000
Ngongo

Ngongo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2008
12,718 2,000
Ni mwanzo mzuri katika mashirikiano baina ya vyama vya siasa.
 

Forum statistics

Threads 1,285,932
Members 494,834
Posts 30,879,374
Top