Kinondoni, Dar: Hamza mohammed, Polisi Watatu na mlinzi mmoja wauawa katika Majibizano ya Risasi

Naamini kabisa sio tukio la kigaidi, bali ni mtu amevutugwa tu akili okamtoka kidogo ndio hayo yote yakatokea, bahati mbaya sana kwetu kila tukio linalotokea tunalinalinasinibisha na siasa! Na kuja na matokeo ya jumla kwa kitu ambacho mtu anakitasfiri kwa mapenzi na ufuasi wa chama cha siasa!

Bahati mbaya nyingine ni police wetu kupoteza ushahidi muhimu, kwa jeshi lenye weledi, vifaa na ushirikiano hili tukio ni dogo sana kiasi ambacho wangeweza kumkamata kabla hajaleta madhara.
Nikweli ila wewe umetazama kwa video nirahisi kujua hivyo ila polisi wao wasingeweza kujua ni mmoja au ni wengi eneo la tukio ndiyo maana walikuwa wanachukua tahadhari kubwa ,wewe ukusikia wananchi walivyo sema ....waliwapigia kelele polisi wasimshambulie mlinzi wa kampuni binafsi ndiyo wakajulishwa kuwa ni peke yake alikuwepo wakati huo huyo jamaa alikuwa kesha uliwa
 

Ni tukio la kushangaza na lenye maswali mengi kwa sasa hivi hakuna ajuae Ukweli ngoja tusubiri taarifa ya jeshi la polisi.

Mpaka muda huu tayari ndugu wa Bwana Hamza wamechukulia wako polisi kwa mahojiano zaidi.
Lakini tujiulize
1. Hamza ni nani ?
2. Ni raia wa Nchi gani ?
3. Anafanya Kazi gani ?
4. Kama tukio hili tutaliweka kwenye kundi la Ugaidi tujiulize kwanini shumbulio lake liliwalenga Askari polisi pekee licha kuwa na nafasi ya kuwadhuru raia waliokuwepo karibu nae mfano kwenye Daladala.
4. Ukitazama vizuri baadhi ya video utaona jamaa alikuwa anashambulia na kukwepa (swali) mafunzo haya aliyapata wapi au tuseme ameiga kwenye Movie??
......................
Huo ni Upande mmoja wa maswali lakini Kuna upande mwingine umejaa tetesi kwamba huyu Bwana Hamza ana mgodi huku Chunya mkoani Mbeya ambao waliachiwa na Marehemu Baba yao. Tetesi hizi zinadai kwamba siku ya tukio Bwana Hamza alikuwa kwenye mipango ya kufanya Biashara ya Madini na suala hili Kuna maafisa wa jeshi la polisi walikuwa wanalijua sasa basi Kuna kitu cha ajabu Sana kikatokea na kukwamisha hiyo biashara. Ni kitu gani hicho ngoja kwanza jeshi la Polisi limalize Kazi yake May be litatueleza ukweli narudia tena May be.
**********
REJEA.
Nenda kwenye Post za Millard Ayo (Instagram) Kuna Dereva tax anaefanya shughuli zake karibu na nyumbani kwa Akina Hamza amekiri ni kweli Hamza na ndugu zake wengine waliachiwa Mgodi huku Chunya mkoani Mbeya na Marehemu Baba yao.

Lakini pia Kuna kipande cha ujumbe amekipost Le Mutuz nitakiweka hapa ili uunganishe matukio.

Swali la Mwisho. Hamza ni kichaa au ana tatizo la Akili ??
Siku chache zilizopita Kuna watu walikamatwa na Madini feki huko Dar es laam. Please hii nayo usiiweke mbali ukianza kuunganisha matukio

View attachment 1908534
 
Binafsi najisemea kuwa watanzania weng hatujui matukio na hatuchukui muda wetu kujisomea na kufuatilia mambo. Ndo maana tukio hili linachukuliwa kirahisi sana na linamaelezo meng ya tofauti tofauti na mepesi. Ukisikiliza shuhuda mmoja mmoja utaamini haya niandikayo pia ukifuatilia comment za watu. Mtu anachukulia bunduki n kama manati na mtu anachukulia mwalifu hasa wa kutumia silaha kama kibaka wa mfukoni.

Mtu anaona kama askari kama si watu ila wajinga flani na wazembe nyakati zote. Ila nature ya askari na majesh yote yaliyo kwenye sare rasmi huwa n watu wa lawama sana na ni target rahisi sana maana wanaonekana na kufahamika kirahisi tofauti na wasiona na sare.
Kilichowakuta askari wa uingereza. Ufaransa na marekan pale iraq nadhan wajuvi wa mamabo watakuwa wanaelewa nn kilikuwa kinawaponza.

Yote kwa yote tujifunze kuviheshmu vyombo vyetu vya ulinz na usalama maana naamin sote tunaopiga kelele mitandaon tungepewa silaha alafu ndo tuwe katka utekelezaji wa kazi ile asilimia kubwa wangekimbia maana ogopa sana bunduki ambayo milio yake ukiisikia unajua umeelekezewa wewe mtutu wake. Pili eneo mapambano huwa linatisha zaid ya vile tumeona kwenye video. Pia tukumbuke wakat mtu unapambana wakati huo unakuwa na familia tena unaitegemea nayo inakutegemea zaid.

Nihitimishe kwakusema kama hujawahi shuhudia maganda ya risasi yakidondoka karibu ya mwili wako kamwe huwezi jua meng kuhusu matukio ya utumiaji wa silaha. Na kama hujawahi kuwa mhanga wa kutekwa kwa kutumia silaha huwezi jua hofu inayokuwa mioyon mwa watu walio na uhai na roho moja.
Tuombee aman nchi yetu tuombe matukio kama haya yasijitokeze katka nchi yetu.
 
Inasikitisha sana kwa askari kuporwa silaha ,askari inatakiwa ume active ,kama umeshika mtutu inatakiwa 20m mtu unammonitor anavyokuapproach,ukimuona haeleweki unamuamuru Hands Up akikaidi inapiga moja kwa hewa kisha ukimuona anataka kuchukua kitu mfukoni unawesha ya mguu kisha unamuattach fasta.

Polisi inabidi warudi mafunzoni,yaani jamaa anatamba dakika 30 nzima na askari wapo kibao wanaogopa,check baada ya jamaa kudongoka ndani ya dakika wakajitokeza askari kanzu wenye mitutu na wa mavazi kama 50 hivi,yaani inashangaza walikuwa kibao lakini walikuwa wanamuogopa jamaa mmoja tu.
Alivopora silaha akawaua hao police aliowapora silaha.? Hao walioporwa walikuwa wangapi na wameuawa wangapi.? Jumla ni Vifo vingapi kujumlisha na wale wanne waliouawa wakati wa kushambuliana.?
 
Inasikitisha sana kwa askari kuporwa silaha ,askari inatakiwa ume active ,kama umeshika mtutu inatakiwa 20m mtu unammonitor anavyokuapproach,ukimuona haeleweki unamuamuru Hands Up akikaidi inapiga moja kwa hewa kisha ukimuona anataka kuchukua kitu mfukoni unawesha ya mguu kisha unamuattach fasta...
Unayajua mazingira yaliyopelekea wao kuporwa hizo silaha?

Vipi kama hao askari walikuwa ambushed na huyo jamaa akafanikiwa kuwaua au kuwadhuru na hivyo kuweza kuzichukua silaha walizokuwa nazo kiurahisi zaidi?

Ni rahisi sana kukosoa ukiwa umekaa mbali na eneo la tukio tena baada ya kupita masaa tele kuliko ungekuwepo hapo huku ukishuhudia tukio in real time.
 
Inawezekana hilo pia
Ila Gaidi kaacha kushambulia Ubalozi na wananchi anawaambia ondokeni pia kuongea na yule mtoto na kuwaambia madereva waondoke na magari yao
Ugaidi upo ila hii sio mbinu za kigaidi labda iwe mbinu mpya...
Mkuu ugaid n mpana sana na usijiwekee mpaka katika mambo nyeti kama haya. Gaid ama ugaid haujawah taki kikubwa ila kama lililotokea. Kwa wakati wako jitahid kusoma sheria ya ugaidi pia kujifunza viashiria vya ugaid namna ugaid unavyopenya.pia na malengo ya magaidi.
 
Ni jambo la kheri sana hawa Polisi wanaoitumikia CCM badala ya wananchi na kupora mali za raia kuendelea kuuawa.Mungu bariki sana yule gaidi.
View attachment 1908590
8860003675.jpg
 
Alivopora silaha akawaua hao police aliowapora silaha.? Hao walioporwa walikuwa wangapi na wameuawa wangapi.? Jumla ni Vifo vingapi kujumlisha na wale wanne waliouawa wakati wa kushambuliana.?
Mjuba ata kufuatilia huwezi..unachosha watu
 
Scenario inayosemwa ni kua zile silaha alinyang'anya maaskari baada ya kutaka kumwonea kimakosa , haya mambo yanafanyika sana hasa wale wanaitwa tigo wanaozunguka na pikipiki ni washenzi sana wale , hapo mtambambika kesi kua alishirikiana na gaidi walioko Zambia kwa sababu mnajua hawezi ongea lakini damu yake ita wa hunt mmoja baada ya mwingine na hamtatoboa !!
Hata kama madai yako ni kweli, je kuna haja ya kuchukua hatua za kipumbavu kama alivyochukua mwenzako huyu unayejitahidi kumtetea? Jicho kwa jicho wameliteketeza gaidi la kisomali
 
Jeshi la polisi wasibebane ktk hili inaonekana huyu Bwana kafanyiwa dhuluma na polisi ndio maana hakuwa na shida la Raia Bali polisi ili kulipiza kisasi. Ni polisi akina Nani hao wamemfanyia dhuruma? ...Ni muda Sasa Rais kumwondoa sirro na waandamizi wengine kulisafisha....Kama watu wanadhulumiwa na kuona solution Ni kupambana kwa risasi Basi tunajenga Taifa jipya kabisa.

Polisi wamejengewa hii tabia ya dhuluma na watawala waliopo madarakani, kama hawa hawa polisi ndio wanaotumika na watawala waliopo madarakani ili kupora chaguzi, unategemea kuna wa kumzuia mwenzake? Kinachofanyika kwa polisi na watawala hawa ni kile waswahili wasemacho, nilinde kwa jua, nikulinde kwa mvua. Hapo polisi wanahakikisha ccm wanaingia madarakani kwa kupora chaguzi, kisha ccm wakishaingia madarakani wanawaachia polisi wale rushwa na kupora wananchi.
 
Ameshuhudia ila mengne yanamaswali. Maana tulichokiona kwenye video na anachokisema kunasehemu vinakinzana na hii n kwa kawaida kwa binadamu kutaka kuonekana wameshuhudia kutoka mwanzo mpaka mwisho
Wabongo tunaupiga mwingi kwenye kutoa ushahidi
 
Back
Top Bottom