Uchaguzi 2020 Kingwendu atia nia ya ubunge Kisarawe, aapa kumng'oa Jaffo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,599
141,415
Mwigizaji mkongwe wa vichekesho hapa nchini, Rashid Mwinshehe maarufu kama "Kingwendu" amesema kwa mara nyingine atagombea ubunge wa Kisarawe kupitia chama chake cha CUF na safari hii ameapa kumng'oa mshindani wake mkuu Suleiman Jaffo

Maendeleo hayana vyama!
Screenshot_20200623-074312~2.png


Kingwendu amesema anagombania Ubunge sababu Mbili.

Sababu ya kwanza ni awahudumie Wananchi sababu yeye anaishi Kisarawe na amekulia Kisarawe hivyo matatizo ya Wananchi ya Kisarawe anayajua. Kasema Kisarawe ina matatizo makubwa ya Maji, Shule, huduma za Afya na Barabara. Hivyo anataka kwenda Bungeni kuwasemea Wananchi.

Sababu ya pili ni kwamba anataka kuitwa Mheshimiwa na kujitengenezea jina. Kasema kwenye Sanaa jina analo na anafahamika ila bungeni anafahamika zaidi.

Kakanusha kwamba kule bungeni hafuati mpunga kama watu wanavyodai kwani hata Kisarawe Mpunga upo Wanalima wenyewe.

Kasema yeye ni Mwanachama wa CUF na ataendelea kuwa CUF hadi CUF itakapo kufa.

Kingwendu amesema kuwa alitetereka mwaka 2015 baada ya kuuza gari mbili pamoja na kuua baadhi ya biashara zake kisa Uchaguzi na kuongeza kuwa mwaka huu amepania sana na lazima ashinde kwa sababu watu wa Kisarawe wamemmis sana.

Ameongeza kuwa mwaka 2015 sikuhongwa kama watu walivyokuwa wanadai bali Mh. Suleiman Jafo alishinda kiuhalali kabisa. “Mimi ndio nimemshauri Stive Nyerere akagombee kwao Iringa aachane na Kinondoni watoto wa mjini hawawezi hawa”

===

Kingwendu ni mchekeshaji wa siku nyingi nchini Tanzania, na ameshiriki katika maigizo mengi ya vichekesho na watu maarufu kama Mzee Small na Majuto, na hivi karibuni amepata tuzo kem kem za kuwa mwigizaji maafuru wa vichekesho
 
Back
Top Bottom