Kingunge, Sumaye nje Kamati Kuu

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Kingunge, Sumaye nje Kamati Kuu

2007-11-07 10:20:29
Na Beatrice Bandawe, Dodoma


Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), jana ilimpitisha Bw. Yusuf Makamba, kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Wajumbe mashuhuri wa Kamati Kuu ya zamani ambao hawamo katika orodha ya sasa ni Bw. Kingunge Ngombare-Mwiru, Bw. Frederick Sumaye na Bw. Mizengo Pinda.

Aidha, Nec imepitisha jina la Bw. John Mkuchika, Mbunge wa Newala, kuwa Naibu Katibu Mkuu upande wa Tanzania Bara na Bw. Salehe Ramadhani Feroudh, kuwa Naibu Katibu Mkuu upande wa Zanzibar.

Kabla ya uchaguzi huo, nafasi ya Naibu Katibu Mkuu kwa upande wa Bara ilikuwa inashikiliwa na Bw. Jaka Mwambi ambaye katika orodha ya wajumbe wa sasa wa Sekretarieti hayumo.

NEC pia imemteua Bw. John Chiligati kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho. Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Bw. Aggrey Mwanri.

Aidha, imemteua Bi. Kidawa Himid Salehe kuwa Katibu wa Oganizesheni wakati Bw. Bernard Membe atahusika na mambo ya nje. Katika masuala ya Uchumi na Fedha, ameteuliwa Bw. Amos Makala.

Wajumbe wa Kamati Kuu, waliochaguliwa ni Dk. Maua Daftari, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Bw. Muhammed Seif Khatibu, Bw. Omar Yusufu Mzee na Bi. Fatma Said Ali.

Wengine ni Bw. Yusuf Hamad Yusuf, Samia Suluhu Hassan, Bw. Rostam Aziz, Bw. Andrew Chenge, Bi. Pindi Chana, Dk. Abdallah Kigoda, Bw. Abdulrahman Kinana na Bi. Anna Makinda.

Awali, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alipendekeza majina 30, kati ya hayo 15 kutoka bara na 15 visiwani.

Kwa mujibu wa Ibara ya 109 ya Katiba ya CCM, kifungu cha kwanza, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, itakuwa na wajumbe
wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati Kuu kupitia nyadhifa zao.

Miongoni mwao ni Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Waziri Kiongozi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na yule wa Baraza la Wawakilishi.

Akiongea mara baada ya kupitishwa kwa majina hayo, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Bw. Pius Msekwa, alitaja majina yaliyopendekezwa kugombea nafasi hiyo kwa upande wa Tanzania bara kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM .

Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. John Guninita, Bw. Adam Kimbisa (NEC, Dodoma), Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Bw. Willian Kusila, Bw. Kingunge Ngombale- Mwiru, Bw. Frederick Sumaye, Dk. Rehema Nchimbi, Bw. Mizengo Pinda na Bw. Stephen Wassira.

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, aliopendekezwa, ni Bi. Mwajuma Majid Abdallah, Ali Mzee Ali, Machana Othman Said, Salim Hemed Salehe, Usi Yahaya Haji, Mansour Yusuf Himidi, Haroun Ali Suleiman na Hamad Mansour Yusuf.

Bw. Msekwa alisema pamoja na kupendekeza majina hayo, Mwenyekiti ana nafasi 10 za wajumbe wa Kamati Kuu ambayo yeye mwenyewe atawateua.

Alisema kwamba kwenye Katiba ya CCM kuna kipengele kinachomruhusu Mwenyekiti kuteua wajumbe 10 watakaoingia kwenye Kamati Kuu kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Alisema jana Mwenyekiti aliteua majina ya watu wawili kati ya 10. Kati ya walioteuliwa ni pamoja na Bw. Cleopa Msuya, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya kwanza.

Mwingine ni Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya nane.

Bw. Msekwa alisema nafasi nane zilizobaki Mwenyekiti anaendelea kuzifanyia kazi na ataendelea kuteua wajumbe.

Majina ya wajumbe wa Kamati Kuu ya zamani pamoja na Mwenyekiti, Rais Kikwete, ilijumuisha pia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti bara, Bw. John Malecela na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed
Shein, Naibu Katibu Mkuu Bara, Kapteni Jaka Mwambi, Katibu Mkuu, Bw. Yusuf Makamba, Naibu Katibu Mkuu, Zanzibar, Bw. Salehe Ramadhan Ferouz, Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, Rais mstaafu wa awamu ya pili, Bw. Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Bw. Benjamin Mkapa, Mzee Rashid Kawawa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour.

Wengine ni Waziri Kiongozi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, Katibu Uenezi, Bw. Aggrey Mwanri, Bi. Kidawa Hamid Salehe, Bw. Rostam Aziz, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Bw. Pandu Kificho, Dk. Gharib Bilal, Abiud Maregesi, Bi. Anna Abdallah, Dk. Emmanuel Nchimbi na Amina Salum Ali.

Wengine ni Bw. Kingunge Ngombale Mwiru, Zakia Meghji, Ali Ameir Mohammed, Pindi Chana, Dk Salim Ahmed Salim, Haji Omar Heri, Anna Makinda, Abdulrahman Kinana, Samia Suluhu Hasan, Abdallah Kigoda, Dk. Asha Rose Migiro, Yusuf Mohamed Yusuf, Dk. Maua Daftari na Muhammed Seif Khatib.

Aidha, Bw. Msekwa alisema Chama cha Mapinduzi , kimepanga namna na kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambapo Mkutano wa kazi wa kwanza wa NEC utafanyika Butiama, mapema mwakani.

SOURCE: Nipashe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom