Kingunge nusura amng’oe Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge nusura amng’oe Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Oct 5, 2012.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]  na Mwandishi wetu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] MWENYEKITI wa Chama cha Mapunduzi, Rais Jakaya Kikwete, na sekretarieti yake wameponea tundu la sindano kung’oka baada ya mkongwe wa siasa nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, kutangaza mgogoro wa katiba ya chama hicho ambao ungehatarisha nafasi yake.
  Kingunge ambaye ameshika nafasi mbalimbali za uongozi nje na ndani ya chama, aliwasilisha hoja hiyo ya mgogoro wa katiba wiki iliyopita wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), iliyokuwa na ajenda ya kufanya uteuzi wa majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM.
  Habari kutoka ndani ya NEC, zilizema kuwa mara baada ya Rais Kikwete kufungua mkutano huo, Kingunge alinyoosha mkono akitaka kuwasilisha taarifa.
  Kabla ya kuruhusiwa, Rais Kikwete alimtaka mkongwe huo kuvuta subira ili atoe taarifa za vurugu za wakulima na wafugaji Loliondo na baada ya kumaliza kutoa taarifa hiyo kwa NEC, alimruhusu Kingunge kuzungumza.
  Alipopata nafasi, Kingunge alianza: “Mheshimiwa Mwenyekiti, samahani sana, nimesimama hapa kutangaza mgogoro wa Katiba.”
  Aliendelea: “Tukijiridhisha kwamba katiba imevunjwa, lazima tujadiliane na tuchukue hatua kwa faida ya chama. Hivi sasa chama kiko kwenye harakati za uchaguzi ndani ya chama baada ya katiba ya chama chetu kufanyiwa marekebisho.
  “Bahati mbaya sana marekebisho hayo yamefanywa na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu bila kupata baraka za Mkutano Mkuu kama katiba inavyotaka.
  “Katiba yetu inasema marekebisho yoyote ya chama lazima yapate baraka za Mkutano Mkuu isipokuwa tu kama kuna dharula, lakini kwa bahati mbaya mabadiliko yaliyofanywa hayana baraka za Mkutano Mkuu na hili sio jambo la dharula.
  “Kwa maana hiyo mchakato mzima wa uchaguzi unaoendelea ni batili, hivyo mchakato huo uvutwe na kuanza upya hadi hapo Mkutano Mkuu utakapopitisha marekebisho ya katiba,”
  Alisisitiza: “Huo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba uliofanywa na viongozi wa chama na ikithibika wamevunja katiba, wawajibishwe.”
  Wakati Kingunge akitoa hoja hiyo ya kutaka mchakato mzima kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa ufutwe kwa madai ya kukiuka katiba, baadhi ya wajumbe walikuwa wakishangilia kumuunga mkono.
  Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa mara baada ya kuwasilisha hoja hiyo, wajumbe na meza kuu walizizima na baadaye Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, alisimama kujibu hoja hiyo.
  Msekwa alianza kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyeongoza kamati iliyosimamia marekebisho ya katika ya CCM ya mwaka 1977 na anajua vizuri kipengele alichotumia Kingunge kutangaza mgogoro wa katiba.
  Msekwa alikisoma kifungu hicho ambacho kinasema: “Kusimamisha kwa maslahi ya CCM utumiaji wa kifungu chochote cha Katiba ya kuingizwa ndani ya Katiba, Uamuzi huo sharti uungwe mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na Theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM taifa, itafikisha uamuzi wake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.”
  Baada ya kusoma kifungo hicho, Msekwa alisema mabadiliko hayo ya katiba yalizingatia kifungu hicho na baadaye wajumbe wa pande mbili za muungano walipiga kura kuafiki mabadiliko hayo.
  Kwa mujibu wa Msekwa, NEC sasa inawajibika kutoa taarifa mbele ya Mkutano Mkuu kuhusu mabadiliko hayo, hivyo hakuna katiba iliyovunjwa.
  Ikumbukwe kuwa wakati wajumbe walipopiga kura kuridhia mabadiliko hayo, Kingunge alipiga kura ya hapana, kupinga mabadiliko hayo.
  Duru za kisiasa ndani ya NEC, zilisema kuwa baadhi ya wajumbe walihoji sababu ya Kingunge kutaka kumng’oa Kikwete na serektari yake wakati ana uwezo wakati wowote kumwona mwenyekiti wa chama na kujadiliana naye kama kuna makosa.
  “Bahati nzuri sana wajumbe wengine hawakusimama kuunga mkono, lakini jambo lenyewe lilikuwa baya, fikiria kama tungefuta mchato mzima na kuvunja sekretarieti maana yake CCM ingefia hapo,” alisema mmoja wa wajumbe wa NEC.
  Baadhi ya madiliko yaliyofanywa katika katiba ya CCM ni pamoja na kuwaondoa wazee wastaafu (marais) katika vikao vya NEC na kuwapa nafasi ya kuunda baraza lao.
  Mabadiliko hayo pia yameruhusu wana CCM kugombea NEC kupitia wilayani kwao ili kukisogeza chama mikononi mwa wananchi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Waigizaji tu hawa ndugu. Unaweza kukuta kuwa hata huyu mzee alitumwa tu aseme hivyo ili ionekane tu mbele ya macho ya dunia kuwa chama kina demokrasia.
   
 3. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Huyu Mzee aliwahi kuulizwa 'nini maana ya zidumu fikra za mwenyekiti?' Alianza kulia kama kachanganyikiwa na sherehe za kutoa kadi za uanachama zikaishia hapo baada ya siku 2 ugeni waakina...... ulifika namkumbka sana huyu KADA
   
 4. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mzee kamati kuu anawakilisha kundi gani au wapagani?
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  huyu mzee ni disappointment kwa taifa!
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Kingunge ni nani kwenye taifa la Tanzania.
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Je huyu mzee anaundugu na wasira?
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Yule mzee anaeamini siasa za ujamaa kama dini yake lakini alijimilikisha kituo cha Ubungo.
   
 9. Mwakitobile

  Mwakitobile JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe kijana wa juzi,hauwezi kujua ila kama unataka kujua vizuri muulize mzee wako kikwete anamjua vizuri,umenielewa Ridhwan(Ritz)
   
 10. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,490
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ilikuwa wapi iyo mkuu na mwaka gani
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo mzee ndio atamng'oa JK, Chadema bana kwa kupenda kuliwazana.
   
 12. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kama uchaguzi ungepigwa "ajua" sijui kama Ridhiwani angepita tena bila kupingwa.

  Kila kambi ingetaka iweke watu wake wilaya zote ili kupata wawakilishi wa kutosha NEC
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mkuu pitia upya sheria na kanuni za JF kuna kitu kinaitwa Name Calling.
   
 14. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa 1979 kambi ya mgulani
   
 15. m

  mamajack JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kundi la wataalamu wa jadi.
   
 16. m

  mamajack JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  interaption tafadhali,kituo cha ubungo alimilikishwa na magamba.
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2015
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kingunge yuko wapi siku hizi???

  nini kimemkumba??
   
Loading...