Kingunge Ngombale Mwiru: Nilitofautiana na kupata matatizo na viongozi wa kanisa Katoliki, Nikaacha kwenda Kanisani

But leo amekujakuzikwa kwa misingi ya kanisa alilokuwa analikosoa maisha yake yote ya utu uzima. Amezikwa Kikatoliki.
 
Mwanasiasa huyu amemalizia maisha yake kwa kushindwa katika itikadi zake akiwa hai. Itikadi hizi ninazozungumzia ni mbili: Itikadi za kisiasa na imani. Kisiasa, Kingunge amejijengea imani binafsi ya ujamaa. Akajikita kwenye chama cha TANU na hatimaye CCM. Siasa ya ujamaa imedhihirika kushindwa na mwenyewe kukihama chama cha CCM. Amekufa akiwa si mwana CCM. Amefeli kwa hili. Kiimani, Kingunge ameiaminisha dunia kuwa dini ni upuuzi. Hakuwahi kuwa muumini wa dini japo alibatizwa mkatoliki. Hajawahi kulihudumia kanisa katoliki kwa lolote mpaka mauti yake. Kwenye kitanda cha mauti pale Muhimbili akatubu na kurudi kanisa katoliki. Akazikwa kikatoliki. Hivyo kudhihirisha kufeli katika itikadi aliyoishi maisha yote kuwa dini ni upuuzi. Hivyo, Kingunge ni hazina iliyofeli katika itikadi zote. Ni fundisho tosha kwa wasomi wetu wote uchwara.
 
Anayeota ni yule anaye kanusha kitu ambacho kipo, kina exist na kujifanya hakipo ili tuu kuji please!.

Muungano upo na una exist, uwe ni uvamizi, uliingiwa kwa halali, au kwa shinikizo, it doesn't matter much, kitu muhimu ni muungano upo na una exist!.

Muungano huu ni kama ndoa, ndoa ikiishafungwa, na kuwa consummated, ndoa hiyo ni ndoa halali na wanandoa wapo wakitimiza majukumbu ya ndoa hivyo. Hata kama mwanzo bibi Harusi alibakwa, alilazimishwa, alishurutishwa, alihadaiwa, as long as amekubali kuolewa kwa kusaini hati ya ndoa, na hadi leo bado anadumu kwenye ndoa hii, ndoa hii ni halali, na uwepo wake, unahalalisha kila kilichotokea kabla kwa kanuni ya the end justify the means!, muungano upo na utadumu milele!.

P.
hakuna chocote kinachoonesha kama kuna muungano kama mzee unao uthibitisho au ushahidi please tuwekee tuone hapa ila kinachoonekana wazi ni ukoloni na sio chengine
 
Namnukuu
“Sina ugomvi na uwepo wa Mungu na hili siyo la kuhoji, isipokuwa ndani ya Biblia na vitabu vingine vinavyoitwa vitakatifu, yapo mambo yanayofikirisha na kujenga uwanja mpana wa kuhoji. Binadamu mkamilifu anapaswa kuhoji na kuwaza juu ya kile anachosoma, kuambiwa na hata kufanya na haya ndiyo yanatutofautisha na wanyama wengine,”
Concrete argument.
 
Sawa!, lkn mwisho wa siku aliamua kumrudia MUNGU.
Umejuaje?? Yeye alikuwa anamjua Mungu kinamna nyingine na sio kwa mtazamo wa hizi dini.
Unajua hata wew ukijiweka pembeni na hayo mambo huwa mara nyingi ndugu ndio wanakuwa kwenye wakati mgumu na sio wew...
Wanakuzikaje?? Je wakufukie tu? Hawana utaratibu mwengine zaidi ya ule waliouzoea... familia ilikuwa haina namna.
 
Figganigga,
Kila nikisoma makala hii ya Nsajigwa Nsa'Sam sichoki kuirudia. Huyu Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru ni mmojawapo wa Great Thinkers wa JamiiForums.

Shukrani sana Mkuu Figganigga kwa uzi unaoelezea great thinkers wa JF tuwe na tabia zinazofanana na Mzee Kingunge ktk kuhoji kila kitu na siyo kuwa watu wa mapokeo, kushangilia au kupongeza bila kuhoji.
Mzee kingunge alielezea jambo kuhusu safari ya maisha yake kifikra.

Nilipenda sana kusoma vitabu na nilisoma vingi…baadhi ya vitabu vilipigwa marufuku, lakini hata hivyo navyo nilikuwa mdadisi kutaka kuvipata na kuvisoma…

Ni katika kusoma vitabu ndipo nilipokutana na vitabu hivi vya Bw Thomas Paine: “The Age of reason”, “The rights of man” na “Common sense”…

Huyu Tom Paine alikuwa Mwana fikra huru (Freethinker).

Tom Paine aliuliza kuhusu imani za kidini, kuhusu pia tawala za kifalme na kimalkia (monarchy), pia alitetea mapinduzi ya Ufaransa, na aliunga mkono vita vya wamarekani kuwa taifa huru, kutoka utawala wa Mwingereza…

Maandishi ya huyu bwana (Thomas Paine) yalinipeleka hatua nyingine ya juu katika kuijua dunia na jamii, alisema Mkongwe Kingunge…

Yalinipaisha upeo wangu wa kuhoji mpaka ikafikia hatua ambapo kwa mambo ya imani za dini nikaanza kuwa na mtazamo tofauti..!...
Credit to : Nsajigwa Nsa'Sam PhD
 
Back
Top Bottom