Kingunge Ngombale-Mwiru azikwa Kikristo makaburi ya Kinondoni; Rais Magufuli, Lowassa, Kikwete washiriki

kimpango

JF-Expert Member
Apr 24, 2011
600
716

DVRcTNTWAAAFnSb.jpg
Viongozi waandamizi wa vyama na serikali waliohudhuria msimba na Nguli wa siasa za Kijamaa Kingungunge Ngombale Mwiru
Magu.jpg

Rais Magufuli akiwa anaweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa nguli wa siasa za kijamaa Kingunge Ngombale Mwiru
DVQqpbrXcAAKcwi.jpg large.jpg

Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA mh Edward Lowassa akiwa na mkewe Regina Lowassa kwenye msiba wa marehemu Kingunge Ngombale Mwiru. Kulia ni waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba

Mbowe.jpg
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa mh Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru.

DVRI9UBX0AEnOxu.jpg

Viongozi mbalimbali waandamizi waliohudhuria mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru
39-600x448.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza mamia ya Watanzania kutoa heshima za mwisho Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Nipo njiani naelekea Karimjee hall, nitawajulisha kila kitu kinachojiri huko. Pia mwingine aliyetangulia anaruhusiwa kuongeza maana siwezi kucover corner zote

Kingunge aliyefariki dunia Februari 2,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zaidi soma => TANZIA: Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru afariki dunia! Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi
=============

Ratiba ya mazishi ya Baba yetu mpendwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (Baba Kinje)

Jumatatu tarehe 5/2/2018
==>Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.

==>Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote

==>Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu

==>Saa 6:00 mwili kuwasili karemjee halll Kwa kuagwa - Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu

==>Saa 9:00 aalasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini kinondoni

==>Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko

==>Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani Kwa chakula cha jioni. Waombolezaji wote

==>1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote

==>3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli ya Mzee wetu

Tunawashukuru sana Kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu

Mungu awazidishie Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Omary A Kimbau (Mwenyekiti wa kamati ya mazishi)
 
Apumzike kwa amani baada ya kazi kubwa aliyoifanya kwa nchi
Viongozi wetu ni mfano wa kuigwa pamoja na tofauti zao hawaachi kutabasam wanapokutana ni ishara ya uvumilivu
 
Acha tu apumzike, baba yetu;
Mungu amsamehe dhambi zake zote;
alale salama;
Naamini watakutana na Mwl. Nyerere,
sijui wataongea nini;
................Natamani hata nimtume salamu za baba yangu na
mama yangu ila basi tu;................
 
Back
Top Bottom