Kingunge naye hatimaye kaamua kuiponda Serikali ya Kikwete

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,919
3,206
katika hotuba za kigoda cha Mwalimu Nyerere, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amesema ni aibu kwa serikali kuleta wawekezaji kwenye kilimo wakati wapo vijana watanzania walio maliza chuo kikuu wanazurura mtaani bila ajira. Hao wawekezaji wanachuma hapa wanapeleka nchini kwao.

Akasema ni kama kwenda kuleta maji mbali wakati yapo hapa hapa.

Pia amesema kuna viongozi wa chama na serikali wanamiliki ardhi kubwa wakati wapo wananchi wengi hawana ardhi.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,637
116,794

From muasisi wa taifa to wakili wa mafisadi.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,951
287,542
Kingunge aiponda serikali
• Sendeka, wanazuoni wataka maamuzi magumu

na Waandishi wetu
TANZANIA DAIMAMMOJA wa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru, amewashambulia viongozi wa serikali kwa kutumia umaskini wa Watanzania kujitajirisha.

Kingunge, ambaye amewahi kuwa waziri katika awamu zote za serikali tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa msemaji mkuu katika kongamano la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM ) jana, alisema vitendo vya viongozi wa serikali vikiwemo vya kumiliki ardhi kubwa, vimewafanya Watanzania wengi hasa wakulima wadogo kuishi maisha yaliyojaa dhiki.

Katika kongamano hilo lililofanyika kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Kingune alisema viongozi wengi serikalini wamepuuza maadili ya uongozi yaliyotiliwa mkazo na Mwalimu Nyerere, na hivyo kuua mipango mizuri ya muasisi ya utawala wa awamu ya kwanza ya kuinua hali ya wakulima wadogo wadogo hapa nchini.

Ngombale Mwiru alishangaa kuona serikali badala ya kuinua wakulima wa Tanzania kwa kuwasaidia kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija, inaruhusu wawekezaji kutoka nje ya nchi ambao wanachochuma kinaenda kunufaisha mataifa ya nje.

Aliongeza kuwa hakuna sababu ya kuleta wawekezaji katika sekta ya kilimo na kuwaacha maelfu ya vijana wanaohitimu elimu ya vyuo vikuu wakihangaika kutafuta kazi.

“Kuleta wawekezaji wa nje ni sawa na kwenda kuteka maji mbali wakati unayo karibu yako,” alisema Mzee Kingune ambaye ni kiongozi pekee anayeshikilia rekodi ya kuandika ilani ya uchaguzi ya CCM katika chaguzi kuu tatu zilizopita.

Kingunge alisema ili kuondokana na hali hiyo, lazima kuwe na viongozi wa namna mpya, wenye uchungu na wananchi, sio wale wanaofaidika kupitia umaskini wa wananchi.

“Tunataka mapinduzi, mageuzi ya ndani, kujisafisha ili turudi kwenye misingi. Tunataka viongozi wa namna mpya, mko kwenye chama kutetea misingi ya chama. tunataka chombo cha kuongoza, si suala la maneno ila msimamo wa dhati na vitendo vyake,” alisema.Alisema CCM inahitaji mageuzi ya dhati ndani ya chama ili kuenzi kwa dhati nia ya waasisi wa CCM.

Sendeka ataka wabovu waondolewe

Akichangia katika kongamano hilo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, aliitaka CCM iache kuwa vuguvugu katika kuwashughulikia viongozi wanaobainika kuvurunda katika utumishi wao, badala ya kutumia maneno laini.

Sendeka alisema kuwa CCM katika chaguzi kuu tatu zilizopita iliahadi kuwa serikali ingeunganisha nguvu zake kutoka uchumi tegemezi kwenda unaojitegemea, lakini akashangazwa kuona wawekezaji wanasamehewa karibu shilingi bil. 900.

Aliongeza kuwa wakati taifa likimkumbuka Mwalimu Nyerere, upo uporaji mkubwa wa rasilimali za taifa yakiwemo madini, huku taifa likikabiliwa na hali ngumu ya uchumi.

Alidai kuwa kwa sasa kodi haikusanywi ipasavyo na wageni wanachukua ardhi na kuhamisha madini bila wasiwasi.Alishauri kuwa ili taifa liondokane na hali hiyo, lazima viongozi wawe na msimamo mkali katika masuala ya kitaifa, kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere ambaye amedai hakuwa vuguvugu katika mambo ya msingi ya nchi, kama ilivyo kwa wanasiasa wengi siku hizi ambao hushindwa kusimamia sheria na kanuni.

Wanazuoni wanena

Profesa Shivji, walimbana muasisi huyo wa chama kuhusiana na kufumbia macho mabavu ya vyombo vya dola kutumika kwa mabavu kuwahamisha watu katika vijiji vya ujamaa.

Profesa Issa Shivji wa UDSM, alisema kushindwa kwa ufanisi wa yale aliyoyaasisi Mwalimu Nyerere kunatokana na usaliti wa baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake, takriban miaka 25 iliyopita.

Alisema wasaidizi hao walitumia mfumo wa ukoloni mambo leo kuleta uwekezaji na ubinafsishaji, na hivi leo matunda yake ndiyo yanaonekana.
Alisema Mwalimu Nyerere alisimamia jamii na siasa za kizalendo, sasa limejitokeza tabaka jipya linalopinga ujamaa na kufanya ubepari ushinde.

Akijibu hayo, muasisi huyo alisema kuwa enzi hizo Mwalimu Nyerere alisisitiza mambo ya vijiji vya ujamaa yaamuliwe na vijiji vyenyewe, ingawa utekelezaji wake unaweza kuhojiwa na kuongeza kuwa kuna maeneo mengi ya maendeleo yamekuwepo wakati ushirikiano wake umekuwa wa kulazimisha kama utumwa.

Alisema utekelezaji wa kuhamisha watu kwenda vijijini ulitofautiana sana na zipo sehemu ambazo kilimo kilibadilika kutoka kile cha jadi mpaka ukulima wa kisasa.

Alidai kuwa kama kungekuwa na mikakati endelevu tangu awali na kutumia uzoefu ule wa vijiji vya ujamaa, hivi sasa taifa lingefikia hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya kilimo.
Alishauri vijana wanaomaliza vyuo vikuu nchini na vyuo vingine mbalimbali, kuwekeza katika kilimo badala ya kutegemea wawekezaji wakubwa.

Alisema vijana waliosoma wakiwezeshwa kwa maarifa, mitaji na ardhi wataweza kutoa ajira kwa wengine.
Kingunge pia alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kutokubali kupokea ushauri wenye manufaa kwa taifa.

“Mimi tulikuwa tunatofautiana na Mwalimu katika baadhi ya mambo, lakini alikuwa na kichwa kizuri. Mtabishana atanyamaza karibu siku nzima,” alisema na kuongeza kuwa, ajabu viongozi wa sasa hawataki kupokea mawazo yanayokwenda kinyume na wanavyotaka.

Alitoa mfano jinsi alivyojaribu kuwashauri viongozi wa serikali kuadhimisha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Aprili 13, siku ambayo alizaliwa, badala ya ile ya kifo chake.

“Nimejaribu kuwaomba wenzangu… ama hatuelewani naona nikisema hapa mnaweza mkanielewa. Tarehe ya leo ni siku ya majonzi na simanzi, mimi inanipa taabu kwa sababu niliweza kusaidiana na familia ya mwalimu kule London mpaka alipofariki,” alisema.

Aliongeza kuwa hakuona siku hiyo kama inafaa, kwa kuwa watu wakubwa waliofariki dunia katika historia, siku yao ya kukumbukwa kitaifa huwa ni siku ya kuzaliwa.

Huko katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam, Dk. Ezavel Lwaitama, amesema kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere angelikuwa hai leo, angekibadili Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutafuta kingine mbadala kwa maendeleo ya taifa.

Akichangia mada katika kongamano lililofanyika chuoni hapo, Lwaitama alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kufanya hivyo, kwa kukibadili chama cha TAA na kuwa TANU kabla ya kukiboresha zaidi na kuunda CCM.
“Kubadili chama ni jambo la kawaida hata Mwalimu Nyerere, muasisi wa taifa alivunja chama cha Tanganyika African Association (TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa na kuanzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mwaka 1977.

Alisema Mwalimu Nyerere alikuwa mjamaa wa kweli kwa maneno na vitendo na chama kinachojiheshimu lazima kiige mfano wa Mwalimu kwa kukaa pembeni kutokana na mapungufu yake.

Alifafanua kwamba CCM aliyoiacha Mwalimu sio ya leo kwa vile watu walioaminiwa kushika madaraka wengi wao wanatuhumiwa kwa wizi, ubadhirifu na ufisadi, kutokana na taifa kuongozwa na baadhi ya viongozi wasio kuwa na chembe ya uzalendo kwa nchi na wananchi kwa ujumla.

Alisema ni jambo la kujiuliza ni kwa kiwango gani uzalendo unaweza kuhimizwa ili uwasaidie vijana katika kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya nchi na mustakabali.

Aliongeza kwamba matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu na jimbo la Igunga yanatia shaka juu ya uzalendo wa baadhi ya viongozi, ikiwa ni pamoja na kudhoofisha msisimko wa uzalendo.Alisema dhana ya uzalendo inaweza kuchukuliwa kama kiini cha mjadala kuhusu uongozi wa nchi na mustakabari wa taifa ulivyo sasa.

mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,939
Hana lolote huyo ni mnafiki. Amekuwa madarakani ktk almost awamu zote nae pia amechangia ktk kunyonya wananchi maskini. Anadhani tumesahau tenda ya kukusanya ushuru ubungo bus terminal na parking fee mjini. Hela yote anatia ndani.
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
484
Sijaisoma yote, kwani mwandishi kaanza kwa kukosea, kinginge hakuwahi kuwa waziri wakati wa nyerere wala mwinyi,
 
Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Unajua ni mbaya sana Mzee kuwa mnafiki.

Hivi huyu Kingunge nae anajiona msafi, wakati fisadi mkubwa.

Alikuwa wapi siku zote kusema hayo maneno au ndio kila Fisadi kaishajua akitaka kuonekana msafi ni kumponda mwenzeo JK
 
Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,479
6,168
Pengine naye ameamua kugeukia busara ili akifa maneno yake naye yakumbukwe!!!!

Tuendelee kumuangalia jamani!!!
 
Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,768
892
Pengine naye ameamua kugeukia busara ili akifa maneno yake naye yakumbukwe!!!!

Tuendelee kumuangalia jamani!!!

Vipi pale Ubungo Bus Stand alikuwa anakusanya ushuru pamoja na ushuru wa magari mjini.

Chakushangaza eti alikuwa analipa serikalini Milioni 1 na nusu pale Ubungo kwa siku.

Zinazopaki anazichukuwa ipo siku Wananchi wataziitaji hizo pesa zao
 
Njopa

Senior Member
Nov 18, 2010
192
30
Kingunge aiponda serikali
• Sendeka, wanazuoni wataka maamuzi magumu

na Waandishi wetu
TANZANIA DAIMA

MMOJA wa waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru, amewashambulia viongozi wa serikali kwa kutumia umaskini wa Watanzania kujitajirisha.

Kingunge, ambaye amewahi kuwa waziri katika awamu zote za serikali tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa msemaji mkuu katika kongamano la Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM ) jana, alisema vitendo vya viongozi wa serikali vikiwemo vya kumiliki ardhi kubwa, vimewafanya Watanzania wengi hasa wakulima wadogo kuishi maisha yaliyojaa dhiki.

Katika kongamano hilo lililofanyika kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Kingune alisema viongozi wengi serikalini wamepuuza maadili ya uongozi yaliyotiliwa mkazo na Mwalimu Nyerere, na hivyo kuua mipango mizuri ya muasisi ya utawala wa awamu ya kwanza ya kuinua hali ya wakulima wadogo wadogo hapa nchini.

Ngombale Mwiru alishangaa kuona serikali badala ya kuinua wakulima wa Tanzania kwa kuwasaidia kuendesha kilimo cha kisasa na chenye tija, inaruhusu wawekezaji kutoka nje ya nchi ambao wanachochuma kinaenda kunufaisha mataifa ya nje.

Aliongeza kuwa hakuna sababu ya kuleta wawekezaji katika sekta ya kilimo na kuwaacha maelfu ya vijana wanaohitimu elimu ya vyuo vikuu wakihangaika kutafuta kazi.

"Kuleta wawekezaji wa nje ni sawa na kwenda kuteka maji mbali wakati unayo karibu yako," alisema Mzee Kingune ambaye ni kiongozi pekee anayeshikilia rekodi ya kuandika ilani ya uchaguzi ya CCM katika chaguzi kuu tatu zilizopita.

Kingunge alisema ili kuondokana na hali hiyo, lazima kuwe na viongozi wa namna mpya, wenye uchungu na wananchi, sio wale wanaofaidika kupitia umaskini wa wananchi.

"Tunataka mapinduzi, mageuzi ya ndani, kujisafisha ili turudi kwenye misingi. Tunataka viongozi wa namna mpya, mko kwenye chama kutetea misingi ya chama. tunataka chombo cha kuongoza, si suala la maneno ila msimamo wa dhati na vitendo vyake," alisema.Alisema CCM inahitaji mageuzi ya dhati ndani ya chama ili kuenzi kwa dhati nia ya waasisi wa CCM.

Sendeka ataka wabovu waondolewe

Akichangia katika kongamano hilo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, aliitaka CCM iache kuwa vuguvugu katika kuwashughulikia viongozi wanaobainika kuvurunda katika utumishi wao, badala ya kutumia maneno laini.

Sendeka alisema kuwa CCM katika chaguzi kuu tatu zilizopita iliahadi kuwa serikali ingeunganisha nguvu zake kutoka uchumi tegemezi kwenda unaojitegemea, lakini akashangazwa kuona wawekezaji wanasamehewa karibu shilingi bil. 900.

Aliongeza kuwa wakati taifa likimkumbuka Mwalimu Nyerere, upo uporaji mkubwa wa rasilimali za taifa yakiwemo madini, huku taifa likikabiliwa na hali ngumu ya uchumi.

Alidai kuwa kwa sasa kodi haikusanywi ipasavyo na wageni wanachukua ardhi na kuhamisha madini bila wasiwasi.Alishauri kuwa ili taifa liondokane na hali hiyo, lazima viongozi wawe na msimamo mkali katika masuala ya kitaifa, kama alivyokuwa Mwalimu Nyerere ambaye amedai hakuwa vuguvugu katika mambo ya msingi ya nchi, kama ilivyo kwa wanasiasa wengi siku hizi ambao hushindwa kusimamia sheria na kanuni.

Wanazuoni wanena

Profesa Shivji, walimbana muasisi huyo wa chama kuhusiana na kufumbia macho mabavu ya vyombo vya dola kutumika kwa mabavu kuwahamisha watu katika vijiji vya ujamaa.

Profesa Issa Shivji wa UDSM, alisema kushindwa kwa ufanisi wa yale aliyoyaasisi Mwalimu Nyerere kunatokana na usaliti wa baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake, takriban miaka 25 iliyopita.

Alisema wasaidizi hao walitumia mfumo wa ukoloni mambo leo kuleta uwekezaji na ubinafsishaji, na hivi leo matunda yake ndiyo yanaonekana.
Alisema Mwalimu Nyerere alisimamia jamii na siasa za kizalendo, sasa limejitokeza tabaka jipya linalopinga ujamaa na kufanya ubepari ushinde.

Akijibu hayo, muasisi huyo alisema kuwa enzi hizo Mwalimu Nyerere alisisitiza mambo ya vijiji vya ujamaa yaamuliwe na vijiji vyenyewe, ingawa utekelezaji wake unaweza kuhojiwa na kuongeza kuwa kuna maeneo mengi ya maendeleo yamekuwepo wakati ushirikiano wake umekuwa wa kulazimisha kama utumwa.

Alisema utekelezaji wa kuhamisha watu kwenda vijijini ulitofautiana sana na zipo sehemu ambazo kilimo kilibadilika kutoka kile cha jadi mpaka ukulima wa kisasa.

Alidai kuwa kama kungekuwa na mikakati endelevu tangu awali na kutumia uzoefu ule wa vijiji vya ujamaa, hivi sasa taifa lingefikia hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya kilimo.
Alishauri vijana wanaomaliza vyuo vikuu nchini na vyuo vingine mbalimbali, kuwekeza katika kilimo badala ya kutegemea wawekezaji wakubwa.

Alisema vijana waliosoma wakiwezeshwa kwa maarifa, mitaji na ardhi wataweza kutoa ajira kwa wengine.
Kingunge pia alieleza kusikitishwa kwake na tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kutokubali kupokea ushauri wenye manufaa kwa taifa.

"Mimi tulikuwa tunatofautiana na Mwalimu katika baadhi ya mambo, lakini alikuwa na kichwa kizuri. Mtabishana atanyamaza karibu siku nzima," alisema na kuongeza kuwa, ajabu viongozi wa sasa hawataki kupokea mawazo yanayokwenda kinyume na wanavyotaka.

Alitoa mfano jinsi alivyojaribu kuwashauri viongozi wa serikali kuadhimisha kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Aprili 13, siku ambayo alizaliwa, badala ya ile ya kifo chake.

"Nimejaribu kuwaomba wenzangu… ama hatuelewani naona nikisema hapa mnaweza mkanielewa. Tarehe ya leo ni siku ya majonzi na simanzi, mimi inanipa taabu kwa sababu niliweza kusaidiana na familia ya mwalimu kule London mpaka alipofariki," alisema.

Aliongeza kuwa hakuona siku hiyo kama inafaa, kwa kuwa watu wakubwa waliofariki dunia katika historia, siku yao ya kukumbukwa kitaifa huwa ni siku ya kuzaliwa.

Huko katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam, Dk. Ezavel Lwaitama, amesema kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere angelikuwa hai leo, angekibadili Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutafuta kingine mbadala kwa maendeleo ya taifa.

Akichangia mada katika kongamano lililofanyika chuoni hapo, Lwaitama alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kufanya hivyo, kwa kukibadili chama cha TAA na kuwa TANU kabla ya kukiboresha zaidi na kuunda CCM.
"Kubadili chama ni jambo la kawaida hata Mwalimu Nyerere, muasisi wa taifa alivunja chama cha Tanganyika African Association (TAA) kutoka jumuiya ya kutetea maslahi ya kijamii na kuwa chama cha siasa na kuanzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU) mwaka 1977.

Alisema Mwalimu Nyerere alikuwa mjamaa wa kweli kwa maneno na vitendo na chama kinachojiheshimu lazima kiige mfano wa Mwalimu kwa kukaa pembeni kutokana na mapungufu yake.

Alifafanua kwamba CCM aliyoiacha Mwalimu sio ya leo kwa vile watu walioaminiwa kushika madaraka wengi wao wanatuhumiwa kwa wizi, ubadhirifu na ufisadi, kutokana na taifa kuongozwa na baadhi ya viongozi wasio kuwa na chembe ya uzalendo kwa nchi na wananchi kwa ujumla.

Alisema ni jambo la kujiuliza ni kwa kiwango gani uzalendo unaweza kuhimizwa ili uwasaidie vijana katika kushiriki kikamilifu kwenye maendeleo ya nchi na mustakabali.

Aliongeza kwamba matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu na jimbo la Igunga yanatia shaka juu ya uzalendo wa baadhi ya viongozi, ikiwa ni pamoja na kudhoofisha msisimko wa uzalendo.Alisema dhana ya uzalendo inaweza kuchukuliwa kama kiini cha mjadala kuhusu uongozi wa nchi na mustakabari wa taifa ulivyo sasa.

Kingunge ni mnafiki kama walivyo viongozi woote wa ccm hata Sendeka! Kilango nk Yeye amewaibia sana Awatanzania pale stendi kuu ubungo na nusura pale Machinga complex! Mbona kama wao wasafi hawamuenzi Nyerere? Nyerere alsiema wazi " CCM sio mama yangu na anaweza kuihama kama mwelekeo wake ni potofu" wao wako wapi Unafikiiiiiiiiiiiiiiiii tu, watauwawa na kufauata nyayo tuknana na unafiki wao. If you live in glass house do not throw stones!!! ni wakati sasa tunawataka watu wanodhani kuwa wao ni safi watoke huko, huu sio wakati wa kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Acheni unafiki
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
17,865
8,675
They know the problems...kama kuna sehemu tunacheza mchezo mbaya basi ni huu wa kuruhusu ardhi kuendelea kuvamiwa bila utaatibu. Lets wait for a big problem ahead. Watu wenye njaa na dhiki hawatakuwa na lolote la kupoteza kama ardhi nayo itakuwa siyo yao.
 
Mzee Wa Rubisi

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,759
437
Amechelewa kusema,anatengeneza mazingira ya kufa vema hili akumbukwe kwa kusema hivyo.
Ikumbukwe kashiriki kutunga irani za chama sasa anasema nini,Alipokuwa mbunge na mshauri wa rais mbona ajitokezi kupinga yanayofanywa sasa.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,200
25,626
Huyu mzee anaweza kuamia CDM ukisika CDM wanamkaribisha na kumuita mpambanaji mzalendo wa kweli wanampa na magwanda avae
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom