Kingunge awaponda wanawake wanaotaka usawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingunge awaponda wanawake wanaotaka usawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 19, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,050
  Trophy Points: 280
  MWANASIASA mkongwe nchini, Kingunge Ngombare-Mwiru ameuponda mkakati wa wanawake kutaka kugawana sawa nafasi za uongozi na wanaume akisema wananchi wanahitaji viongozi bora wa jinsia yoyote ile na siyo sura ya mwanamke au mwanaume.

  "Njia bora za kuwatumikia watu siyo kugawana nafasi baina ya wanaume na wanawake, bali kuwatendea wema kwa kazi za maendeleo na kudhibiti njia zote za rushwa kwa viongozi," alisema.

  Kingunge alisema hayo juzi alipoulizwa maoni yake baada ya kuhudhuria warsha ya mkakati wa kuongeza idadi ya wagombea wanawake kwenye majimbo iliyoandaliwa na Chama cha Wabunge wanawake (TWPG) jijini Dar es Salaam ambapo moja ya maazimo ya warsha ni kuhakikisha wanawake wanagombea ubunge kupitia majimbo ili idadi ya wabunge iwe asilimia 50 kwa 50.

  Alisema malengo ya wananchi si kuwaona wabunge wanawake kwenye majimbo, bali ni kuona maendeleo na kuhakikisha viongozi wabovu, wasiojali maendeleo wanaondoka kwenye uongozi na kwamba kwa bahati mbaya viongozi wabovu wengi ndio watoa rushwa.

  "Tukifanikiwa kuzuia rushwa tutapata viongozi wazuri wanawake au wanaume," alisisitiza na kuongeza kwamba kwa sasa rshwa ni kero ndani na nje ya vyama vyote vya siasa.

  Kauli ya kiongozi huyo inatolewa wakati baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakikilaumu Chama Cha Mapinduzi kwamba kimejenga mfumo wa kuwapendelea wanaume katika uongozi na hata kuteua wagombea wa ubunge kwenye majimbo.

  Baadhi ya washiriki walisema CCM inaongoza nchini kwa kuwanyima wanawake nafasi kubwa za kugombea au kuteuliwa hususani kugombea urais au kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na hata kuongoza taasisi nyeti kama polisi au Jeshi la Wananchi.

  Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini (TCD) , Pius Msekwa akifungua warsha hiyo alisema tatizo la wanawake kukosa majimbo linachangiwa na muundo na mifumo ya vyama vyote ambayo inawatenga wanawake kwenye uongozi nyadhifa za juu.

  Kauli hiyo ilipingwa na baadhi ya washiriki walipojadili ambapo walisema kambi ya upinzani imejitahidi kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake zikiwemo za chama cha PP- Maendeleo kuteua mgombea mwanamke wa Urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2005 na Chama cha SAU kumteua mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

  Walisema nacho cha UDP kiliwahi kuwa na Katibu Mkuu mwanamke , Teddy Kasela Bantu ambaye baadaye alihamia CCM.
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kwa heshima na taadhima tunamuomba na yeye ang'atuke kwenye madaraka umri umekwenda ...mwaka huu asigombe kabisaaa
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ngombale is very right. tatizo letu si kiongozi mume au mke, tatizo ni viongozi waadilifu wanaojua nini Tanzania tunahitaji. Tunahitaji viongozi sio wa kuonewa huruma ili kuchaguliwa bali wenye uwezo wa kuongoza au mwanamume au mwanamke au vyote viwili.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  1st lady, huyu Mzee anazeeka vibaya na kuropoka yasiyostahili kila anapofungua kinywa chake.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  awe sahihi au not atuitaji maoni yake angatuke kama mwl na simba wa vita
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kingunge ni mshauri wa Rais wa mambo ya siasa kwahiyo mimi nilitegemea ushauri huu angempa Jakaya; lakini ni Kikwete huyo huyo aliyewatamkia wanawake kuwa kuanzia mwaka hu kila ngazi ya maamuzi ya sera za nchi wanaume watakuwa 50% na wanawake 50%. Je inawezekana kuwa Jakaya hakuthamini ushauri wa Kingunge na kama ni hivyo kwanini aendelee kuwa mshauri ambapo ushauri wake hauthaminiwi?
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,050
  Trophy Points: 280
  unatafuta kurogwa wewe
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Kwa hili japo Kingunge ni mzee sana na anahitaji kupumzika kwa kustaafu yuko sahihi. Kinachohitajika sii uwiano wa fifty fifty kwenye uongozi la, tunahitaji kiongozi mweye kukidhi viwango vya kiuongozi awe mme au mwanamke. Kwa mfano form za kugombea nafasi mbali mbali zinavyotolewa hakuna sharti la kwamba mgombea awe na jinsia gani. Wanawake kubaki kulilia nafasi za upendeleo na ushahidi tosha kwamba hawaja-qualify to compete. Hatari ya kulilia uwiano wa kijinsia utatupeleka kutaka pia uwiano wa kidini serikalini na pia wazee kwa vijana na kabila kwa kabila na mpaka wakati huo nchi itakuwa ishaacha kutawalika tayari.
   
 9. annamaria

  annamaria Senior Member

  #9
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Midume tu tangia nchi imepata uhuru and we have not witnessed progress isipokuwa mi Buzwagi na mi Richmonduli na...,why sasa nchi tusipewe wanawake?
  go women go..
   
 10. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Si umri tu Dada !!mengine hayasemeki kwani sote tunakwena huko huko, kuna wengine wanafika umri hata sura huwa hazitizamiki tena.
   
 11. B

  Bull JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunachotaka ni utendaji mzuri sio SEX, mambo yakupeana madaraka kwa kuoneana huruma au urafiki tumeshaona madhara yake, sasa yaishe

  Umri is just a Number, tunahitaji wazee pia kwenye nchi hii tuache tabia mbaya ya age discrimination

  Huyu mzee yuko sawa kabisa, tumeshaona wanawake wengi wenye sura nzuri kilasehemu wengiwao performance ZERO
   
 12. Katoma

  Katoma Senior Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani ubunge wa kingunge si ni wa kuteuliwa na rais?
   
 13. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  FL1, Kingunge alikuwa mbunge wa Kilwa hadi mwaka 2000 ambapo aliamua kung'atuka ubunge. Toka 2000 hajagombea ubunge. Mkapa alimteua kuwa mbunge mwaka 2000, na Kikwete alimteua tena kuwa mbunge mwaka 2005.

  Kingunge, pamoja na matatizo yake (ukusanyaji ushuru usioridhisha Ubungo Bus Terminal, kutetea mafisadi, kuponda wapambanaji dhidi ya ufisadi, kuitetea Serikali hata unapoboronga), namuunga mkono kwa hili moja tu, la kuwataka wanawake kugombea nafasi, si kusubiri wanaume wawatengee nafasi za upendeleo kwa sababu ya jinsia yao.

  Kinachohitajika ni wanawake kujitokeza zaidi kugombea majimboni, na kuungana mkono kwa wanaofaa. Kuna dhana kuwa wanawake huwa 'hawapendani', hivyo hunyimana kura hata kama mgombea sifa anazo.

  Wabunge wanawake kutoka majimboni kama Anna Makinda, Jenista Mhagama, Anna Kilango wanapambana na wanaume na kushinda, kwanza ndani ya vyama vyao, na baadaye kupambana na wagombea wa vyama vingine.

  Wabunge ambao wameshafahamika zaidi kwa wananchi wanatakiwa sasa kwenda kugombea majimboni ili waongeze idadi wa wabunge wanawake.

  Kama sijakosea, Anna Kilango alikuwa mbunge wa kuteuliwa hadi 2005, mwaka huo akagombea ubunge jimboni na kushinda. Wanawake wengine waige mfano wake.
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Katika hoja hii Kingunge kaongea point tupu, mengineyo ni personal attacks tu, tujadili hoja..
   
 15. w

  wasp JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AnnaMaria je umesahau ya Waziri wa Fedha Mh. Zakhia Meghji alipolizwa na Gavana wa BOT marehemu Daudi Balali kwenye sakata la EPA mpaka akaidhinisha malipo hewa ya usalama wa Taifa? Yule mwingine tukampa urais wa Bunge la Africa kule Cape Town halafu akaanza ufisadi wa kupokea mshahara huku kwenye Bunge la nyumbani na Bunge la Africa pamoja na kutoa ajira kwa wakwe zake! Swala sio uongozi wa 50% wanawake na 50% wanaume bali ni uadilifu wa mtu. Tunao mifano mingi mizuri kama Professor Anne Tibaijuka, Dr. Aisha Rose Migiro. Kwa msimamo huu nampa bigup Mzee Gaetan Kingunge Ngombale Mwiru.
   
 16. annamaria

  annamaria Senior Member

  #16
  Jan 21, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Kwenye ubunge Kingunge is right usiwe wa kubebana manake wengi wanaobebwa huko hawana sifa isipokuwa ni ujanja ujanja tu wa kujuana na wenye mamlaka.Uwekwe uwanja sawa wanawake wenye sifa nao wakasimame majimboni na kuuza sera zao.
  Mimi nazungumzia kwenye appointments hasa katika nafasi nyeti.Tangia hii nchi ipate uhuru walau ni JK ndiye amejitahidi kuwateua wanawake kushika wizara nzito nzito.Ilikuwa ni unaibu waziri,sanasana wizara ya jamii,wanawake na watoto!
  Inawezekana Meghji alipotoka.Lakini huo ni mfano mdogo tu wa kinamama wachapakazi na waadilifu tulionao Tanzania ukilinganisha na kinababa wengi walioshika nafasi mbalimbali serikalini na katika mashirika ya umma ambao ndio wameifikisha hii nchi hapa ilipo.
  Sasa kwanini tena tuendelee na haohao kina baba?Kwanini tusiwe na Rais mwanamke au walau Waziri mkuu?Kwasababu wapo kinamama wengi tu wenye sifa za kutukuka na wanao uwezo wa kuziendesha hizo ofisi.
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,176
  Trophy Points: 280
  Alichosema Kingunge na kichwa cha thread tofauti.
   
Loading...