Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Mapema leo waziri wa Nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia siasa alikutana na waandishi wa habari ofisini kwake. Alizungumza mengi na kubwa ambalo binafsi nililichukulia ni mwelekeo wa kiongozi huyo kutaka "suluhu" na upinzani. Msisitizo mkubwa aliuonesha pale alipozungumza kuhusu Uzalendo "wetu sote" na ya kuwa tofauti za sera na itikadi zisitufanya Watanzania kujiona siyo kitu kimoja. Alipojaribu kuelezea hiyo tofauti alishindwa kutaja neno ujamaa na kwa dakika chache alijiuma uma meno na kusema "Sisi CCM tunazo sera .. na itikadi.. za.. tunazo itikadi; na vyama vingine wanazo sera na itikadi zao".
Bila ya shaka lengo kubwa ni haja ya ofisi hiyo kuona kuwa licha ya tofauti zetu Watanzani tunaendelea kuwa kitu kimoja. Nilivyochukulia ni kuwa alikuwa anajibu mwelekeo unaoonekana sasa hivi ambapo "wazalendo" wanaonekana ni wale wa upinzani zaidi na walio weusi. Kiufupi, Kingunge naamini ametumwa kuja kutaka suluhu na wapinzani... wapatane naye?