Kingine Kilichochangia kumwangusha Dr. Slaa ni hiki hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kingine Kilichochangia kumwangusha Dr. Slaa ni hiki hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Johnsecond, Nov 8, 2010.

 1. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Malalamiko ya wanaharakati wengi na waangalizi wa kimataifa walisema kuwa watu waliojiandikisha na waliopiga kura kuna tofati kubwa sana. Yaani waliojitokeza ni wachache sana ukilinganisha na waliojiandikisha. Swala ni kwamba wengi hawakujitokeza kwa kuwa walisema hata wakimpigia kura Dr. Slaa matokeo hayatabadirika. Slaa jipange kulipeleka kundi hili kupiga kura next uchaguzi na watanzania woote wapenda mabadiriko tujipage vizuri.

  my take: ambao hawakupiga kura walio wengi ni kwa sababu wamechoshwa na CCM.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hizi ni katika propaganda au cheap-politics ambazo zimepandwa na wanaccm, kuwa chama hicho hakiwezi kung'oka madarakani hata iweje.
  Mifano ni mingi inayopinga dhana hii, mimi naamini kuwa mtu kutopiga kura ni ukosefu wa uelewa, period!
   
 3. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  mkuu hata mimi nina notion hiyo inahitajika nguvu ya ziada kulileta kundi hili kwenye sanduku la kura
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  na nec hii ipo kazi kubwa !
   
 5. i

  itembajr Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe uliyeweka hii mada nadhani hauko makini cuz kuna vijana wengi majina yao hayakuwekwa kwenye orodha ya wapiga kura..........acheni maneno yenu ya uongo uongo........
   
 6. R

  Renegade JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,769
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  Wewe acha umbumbu Slaa hakuangushwa ameibiwa kula.
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huu ni upupu tu.Mtoa hoja umetuletea nadharia ya nzuri ambazo hazina uthibitisho. katika uchaguzi huu kulikuwa na dosari kuu mbili ambazo mpka sasa NEC haijatoa meelezo mazuri kama majibu halali. Kwanza, kulikuwa na tatizo katika suala la idadi ya wapiga kura, yaani waliojiandikisha kupiga kura ni wangapi? (Tume ilitaja Milioni 19). lakini swali kuhusu idadi hiyo ni kuwa je, inawezekana kuwa nusu ya Watanzania ni wapiga kura?(Tume wamekaa kimya). Pili, daftari la wapiga kura halikuwa wazi mapema na hatimaye wengi hawakuona majina yao na hawakusaidiwa.Je, Tume ilijibu nini kuhusu hilo?
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Kama huna jipya si bora usome hoja za watu wengine ukala jiwe kama wengi wafanyavyo??
  Hapo juu hamna kitu kabisa analysis za kizamani za CCM.

  CCM ilishinda ndiyo kwa ninimsitangazie hayo matokeo kwenye majimbo???
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu ukifahamu matokeo halisi unaweza kuona kuwa CAHDEMA walifanya kila wanaloweza, hawakuharibu kama watu wanavyodhani. Pamoja na nguvu yooote ya dola, na kuzuia potential voters wa CHADEMA bado matokeo ni mzuri. Muhimu ni kuwa somehow mafisadi waliona ni vigumu sana kukubali upinzani uingie madarakani. Jaribu ku-imagine Lowassa, Mramba, Chenge, Rostam etc etc wangekuwa katika hali gani kama opposition wangeshinda, huenda wengine wangekimbia nchi?? nchi ingekuwa tofauti sana sasa. Hata kama mimi ningekuwa fisadi ningechakachua tu.
   
 10. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Msimlaumu mleta mada, kuna ukweli kiasi fulani kuwa kuna watu hawakuenda kupiga kura kisa CCM i ngeshinda tu. Sababu ziko nyingi.
   
 11. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Haya ndiyo nayaona yalichangia kwa mtazamo wangu
  1. Idadi inayosemwa ya waliojiandikisha inatia shaka sana, kuna namba nyingi sana hapo katikati hazina watu, kwa mfano kwenye kituo changu kuna namba zaidi ya mia mbili ziko empty, Kuna haja ya NEC kulifanyia kazi hili, vinginevyo ni kujidanganya kwamba tuna wapiga kura zaidi 19ml.

  2. Hakuna uwanja sawa kwenye siasa za Tanzania kuanzia ngazi za chini kabisa, mfano, Msimamizi wa uchaguzi Kata ni mtendaji kata, wilaya ni mkurugenzi wa Wilaya, wote hawa wanapatikana kisiasa (kutokana na chama tawala), huko juu NEC Taifa sina haja ya kueleza.

  3. Kuchelewa kubandikwa kwa majina ya wapiga kura vituoni ili yahakikiwe mapema, hii ingetoa muda wa kutosha kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

  4. Kulikuwa na hali tete siku za mwisho za kampeni hali iliyopelekea baadhi ya wapiga kura (Hasa wazee na kina mama) kutojitokeza kwa wingi kupiga kura kwa hofu kwamba huenda uchaguzi ungekuwa na vurugu.

  5. Elimu ya uraia kwa wapiga kura pamoja na wale walioteuliwa kusimamia zoezi zima la uchaguzi.

  6. Uwezo wa kifedha wa vyama vya upinzani kulinganisha na ule wa CCM ( ilipelekea baadhi ya maeneo kutokuwa na mawakala wa vyama vya upinzani hivyo kurahisisha uchakachuaji wa kura)
   
 12. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Naona mko wengi mliopewa kazi ya kuwarudhisha wananchi baada ya kuona rafu za kipindi hiki zilikuwa na kufuru Mungu...:rip:mkuu
   
Loading...