kingereza ni tatizo vyuo vikuu vya tanzania hali inayosababisha wageni kushindwa kujadili na wa tz

kituro

Senior Member
Dec 25, 2010
176
15
jana niliongea na wanafunzi wachache wageni ambao wanatoka nje ya tanzania. niliongea kwanza na wanafunzi wa msc. badae nikaongea na wanafunzi wa bsc. wanafunzi wa msc walisema wao wanatamani sana kujuwa kiswahili ila wanafunzi wa kitanzania wanawaongelesha kingereza nikauliza mnafikili ni kwanini? wakasema wao waliambiwa na baadhi ya rafiki zao kuwa wanafunzi wa msc. wanapenda kutumia kingereza kwao kama sehemu ya mazoezi ya kuongelea kingereza na watu wengine wasio wanafunzi wakijuwa anaongea na mtu wa nje pia hutumia kingereza. akanijibu mfano hata wewe hapa unatumia kingereza tu, mie nikajibu mimi natumia kingereza kwakuwa nikitumia kiswahili mtaniuliza mambo mengi kuwa niwaelezee hamjanielewa, wakasema siyokweli. nikawahakikishia kuwa ukweli ndiyo huo. wanafunzi wa bsc wamesema wawapo kwenye mijadala wanafunzi wakibongo huwa wanasoma swali kwa kingeleza na kuendelea na maelezo ya kiswahili wakisema tutumie kingereza ili na wenzetu waelewe wanabaki kimya. hiyo inaashilia kunatatizo kubwa kwenye kingereza. na wanasema hata walimu wanachanganya sana wanapofundisha.ndugu zangu katika jf nawasilisha uchunguzi wangu nilioufanya jana.
 
Mbona sijaelewa hapa unataka kufikisha ujumbe gani au na wewe ndo kiswahili ujui. na hiyo bsc na msc unamaanisha nini?
Au tuandikie kwa kimombo tujue moja.
 
Hata mimi sijaelewa. Nani hajui nini? Umetuchanganya kidogo fafanua tafadhali.
 
Kituro...ni kitu gani unataka kusema hapa,maana naona unachanganya madawa tu,msc ni master of science au bsc ni bachelor of science au???,ata hivyo bado ujaeleweka bwana mdogo
 
Tatizo letu watanzania wengi hata wale walioenda shule ni kwamba kiingereza hatujui, kiswahili fasaha hatujui na vitu vingine vingi. Watu wako bize kusoma na kuangalia udaku nadhani na mpira tu. Yaani kwa kifupi ni taifa lililoenda mrama kielimu na kila kitu. Wakati wa Mwalimu ilikuwa bora kidogo na hao wachache waliobahatika kuelimishwa walielimika kweli. Kwa kizazi kilichokwishaharibika haiwezekani kuwabadilisha, ni kupoteza muda. It is a wasted generation. Ufumbuzi ni kupeleka nguvu kuwajenga watoto wanaozaliwa na kukua sasa.
 
Kiingereza ni tatizo, pia hata kiswahili. Wanafunzi hawafundishwi msingi mzuri wa lugha. Kutumia kiswahili muda wote sio sababu ya kutojua kiingereza wakati unafundishwa shuleni maana kuna nchi kama SA ambako kuna lugha mbalimbali zinatumika (zulu, khosa, n.k) lakini wanafunzi wanaongea kiingereza kizuri.

Changamoto kwa wanafunzi ni kufanya bidii katika kujifunza lugha hiyo muhimu ktk dunia hii ya utandawazi. Kwahiyo tusilaumu mfumo na kutumia kama sababu ya kutojua lugha unayofundishwa. "It is not about how you start, but rather, how you finish", hili tunaweza kujifunza kwenye mbio za "marathon". Pia kuna dhana kwamba waliosoma zamani wanajua vizuri zaidi lugha hiyo kuliko wa sasa, lakini kikao cha jana na leo cha bunge kimethibitisha kwamba hiyo ni hadithi ya kufikirika tu......

jana niliongea na wanafunzi wachache wageni ambao wanatoka nje ya tanzania. niliongea kwanza na wanafunzi wa msc. badae nikaongea na wanafunzi wa bsc. wanafunzi wa msc walisema wao wanatamani sana kujuwa kiswahili ila wanafunzi wa kitanzania wanawaongelesha kingereza nikauliza mnafikili ni kwanini? wakasema wao waliambiwa na baadhi ya rafiki zao kuwa wanafunzi wa msc. wanapenda kutumia kingereza kwao kama sehemu ya mazoezi ya kuongelea kingereza na watu wengine wasio wanafunzi wakijuwa anaongea na mtu wa nje pia hutumia kingereza. akanijibu mfano hata wewe hapa unatumia kingereza tu, mie nikajibu mimi natumia kingereza kwakuwa nikitumia kiswahili mtaniuliza mambo mengi kuwa niwaelezee hamjanielewa, wakasema siyokweli. nikawahakikishia kuwa ukweli ndiyo huo. wanafunzi wa bsc wamesema wawapo kwenye mijadala wanafunzi wakibongo huwa wanasoma swali kwa kingeleza na kuendelea na maelezo ya kiswahili wakisema tutumie kingereza ili na wenzetu waelewe wanabaki kimya. hiyo inaashilia kunatatizo kubwa kwenye kingereza. na wanasema hata walimu wanachanganya sana wanapofundisha.ndugu zangu katika jf nawasilisha uchunguzi wangu nilioufanya jana.

Jamani kwa swala la kiswahili na kiingereza, nasema hivi, TZ itaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu kama hatutaamua kwa kauri moja kuwa watoto wetu wawapo shule wanaenda kujifunza vita vya maisha wanaenda kujiweka tayari kushindania kazi, kwahiyo waziri mwenye dhamani ndiye anaetakiwa kuwa na mwanga wakusema baasi, watoto wetu kuwa vibarua wawageni, nilikwisha sema hapa mwazoni kuwa, baadhi ya watu wanafurahia kiswahili kuingia kwenye FB nikawaambia kuwa tukubali tusikubali tunajiweka chini ya gereza letu wenyewe bila kujua, haiwezekani tujivunie lugha ya nyanya, wakati haitupeleki popote.
Jamani Serikali inapaswa kuona aibu St. Mary's nashule zake watoto wao wanaweza kuonge kiingereza wakati shule za serikali kuwa mbumbu siku zote, elimu siyo chuo kikuu, ni ndani ya msingi wa elimu ndiko kwenye elimu, samaki akikauka kumkunja ni kazi, kwahiyo kiingereza kifundiswe kuanzia kindergaten.
Tusipoamua baasi tumeamua kuwa mabozi kwa wageni, elimu ya msingi ndiyo elimu kuu ya nyumba ambayo ni chuo kikuu.
 
Kituro...ni kitu gani unataka kusema hapa,maana naona unachanganya madawa tu,msc ni master of science au bsc ni bachelor of science au???,ata hivyo bado ujaeleweka bwana mdogo

haswaaa! mie niliwaambia kuwa wanafunzi wa kutoka njw ya nchi wanashindwa kujadiliana na wabongo kwasababu waswahili wanashindwa kuwasiliana na wageni kwa kingereza. (tatizo lugha)
 
Kiingereza kitu gani bwana!! Wageni wanapokuja kwetu wanapaswa kujua namna ya kuwasiliana na wazawa. Infact kujua lugha ya kigeni ni vizuri ila isiwe jambo la kujilinganisha na South Africa, n.k. Kuna nchi nyingi zimepiga hatua kwa kujimudu ktk lugha zao,circuit boards za electronic devices baadhi zina maelezo ya kichina ,kijapan,kirusi... Sasa swala la msingi hapa ni kukazania kisawahili,kuhakikisha kila mtanzania anafahamu kiswahili fasaha kwa kuandika na kuzungumza. Hivi ni kwanini makampuni ya software na mengine mengi huwa wanajitahidi kutafuta soko kwa kutafsiri manuals za products zao kwa lugha nyingine za kigeni? Ni kwamba wachina,wahindi,warusi,wajerumani.... wanazijua lugha zao kwa ufasaha,na ni watumiaji wazuri wa lugha zao. Sasa sisi waTz tukazanie kukikuza kiswahili,na hata wageni wakija walazimike kujifunza na hapo ndipo tutaona mabadiliko. Hata wataalamu wa IT na fani mbalimbali wajitahidi kushirikiana na wataalamu wa lugha ya kiswahili kuhakikisha wanatoa products/services kwa kiswahili kizuri/fasaha.

Watu wengi tunapojadili makala mbalimbali kwa kiswahili waga tunachanganya lugha(kiswanglish),sababu ni kuwa either hatujui kiswahili fasaha,au kiswahili kina mapungufu ya maneno na hivyo kukosa maana/tafsiri halisi/husika ya neno kutoka lugha 1(kiinglish) kwenda kiswahili.
Nnachotaka kukazia hapa ni kuwa waTz wengi kiswahili hatukijui,achilia mbali mapungufu ya lugha yenyewe. Tuache kulalama bila sababu endapo mtu anashindwa kuongea kiinglish,wala tusishangae kama mtu ataongea broken english,badala yake tumshangae mtu ambaye amekulia mjini na ana elimu nzuri tu lakini hajui kujieleza kwa kiswahili fasaha!
Jamani shida ya waTz wengi hata hicho kiswahili tu hatukijui...!!
 
Jana kuna mbunge wa Kisarawe alikuwa anaomba kura bungeni kupata uwakilishi kwenye SADC ilkuwa kichefuchefu maana mheshimiwa alidai ana masters ye economics lakini sijui presentation huwa anazitoaje na hii inaonyesha ni jinsi gani graduate wetu hawahui kiingereza lakini kujua lugha si kutenda vizuri.
 
Sijamwelewa kabisa huyu mtoa mada.

Vyuo vikuu vya Tanzania, kiingereza ni tatizo?

Kiingereza...kiingereza.... kiingereza..... Kiingereza ni nini bana?

Mbona hata vyuo vikuu vya China, Japan, Uholanzi, Ujerumani nk nk nk Kiingereza kwao ni tatizo?............
 
Back
Top Bottom