King'amuzi: "SIM card never paired"

nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,771
5,315
Habarini wadau, Nina king'amuzi Cha Azamu toka Juzi naona kinaniandikia hivyo, nimeenda mpaka kwenye factory default bado tatizo Ni lile lile,

Kwa uchunguzi mdogo nimegundua dogo alichomeka flash kwenye port ya nyuma ili Hali king'amuzi kilikuwa kwenye matumizi,

Nimeenda kwenye system number card ya hicho king'amuzi haionekani Tena Kama zamani, badala ya yake imeandika "get info fail"

Naombeni msaada wenu,

NB nimewapigia Azamu customer service naona hatuelewani kiswahili!
 
Angalia kama card imechomekwa ktk uelekeo sahihi.kuna uwezekano imegeuzwa chini juu au juu chini au mbele nyuma au nyuma mbele.
 
Angalia kama card imechomekwa ktk uelekeo sahihi.kuna uwezekano imegeuzwa chini juu au juu chini au mbele nyuma au nyuma mbele.
Kadi imechomekwa sawa sawa mkuu
 
Piga *150*50*5# chagua, “Activate New Connection”. Ikigoma ipeleke kwa agent aliekuuzia.
 
Bonga nao kidhungu kama kiswahili hawakuelewi
 
Bonga nao kidhungu kama kiswahili hawakuelewi
Hahahahahaha hayaa bhana, sawa ngoja nijaribu hao wa kiingereza pengine tutaelewana! Nimecheka kweli aisee!
 
Imewahi kunitokea hiyo, hapo ishu ni smart card haijawekwa vizuri.. hebu chomoa weka tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom