King'amuzi cha Digitek

Zipo kaka kuna move channel, News channel, Sports and social entertainment.apo nilitaja local tv kwa kuwa ndo ziko sensitive kwa mazingira yetu


...Ziseme Sasa! Ama mpata tena tukuombe Uzitaje?? Kwa nini waTZ tunapenda sana Longo2? Mdau ameuliza kuhusu 'other African attractive channels' we umejibu kuwa Zipo, basi! Ungefanya jambo jema sana kama ungezitaja kabisa ili kuondoa ulazima wa mdau kulazimika kukutaka Umtajie!!!!:dizzy:
 
Ndugu, serikali imekurupuka sana na hii teknolojia.
Anachokisema mdau ni cha kweli, NO FREE LUNCH. Kwa sasa hao wanaouza visimbuzi vya Digitek wanakusanya wateja kwanza kwa kutoa huduma bure ukishanunua kifaa chao, lakini baadaye watageuka na kusema mlipie huduma hizo kama ilivyo kwa Easy Tv, Agape ama Startimes. Ni suala la muda tu. Anayesema mtalipia 6000/- mwanzoni mwa mwaka ujao yuko sahihi kabisa, huwezi kupata matangazo BURE. Vya bure vilishaondoka na mwalimu

Nashukuru sana mkuu, teknolojia hii naielewa vizuri tu - nilitaka kumchemsha jamaa kwa kuwa naona kama kampuni hii imekaa kaa kama ni jiont venture ya ITV na mshirika wake (I might be wrong though) wasije wakawa wajanja kwa kutuigia kwa gia ndogo kwanza huku wakituhuzia visimbuzi kwa bei ya kuruka hata kama vina option ya ku-record!

Ukijaribu kulinganisha bei zao na bei ya visimbuzi vingine vyenye specs na hardware zile zile kutoka far East utashangaa sana - bei ya Digitek hiko juu sana sijui kwa nini mkuu!!
 
hiki kidubwasha sio HD wala hakikaribii kuwa HD, ila kwa mtu atakaye migrate kutoka startimes kuhamia digitek ata notice tofauti ya ubora wa picha na sauti.
kwa kukiita HD wanaendeleza udanganyifu tu, hata sasa ukinunua wanakwambia utapata channel 20 ila chaajabu mi naona 15 ukiwauliza wanasema "tuliimaanisha zitakuwa 20 ivi karibuni ila kwa sasa kweli ni 15''

Mkulu
King'amuzi hicho ni HD kwani kina HDMI port, sasa wewe unavyosema "WANAKIITA HD" una maana gani??!!

Generally, HD quality depends on the Camera involved in the shooting.... unategemea picha za akina Charles Bronson zilizopigwa na kamera za 1947 unategemea zionekane kwa ubora wa HD?...haiwezekani.


Mengi ameweza kufanya kitu tofauti sana.
BTL subsidiary ya IPP imepewa jukumu la kusimamia king'amuzi kinachofahamika kama "DigiTek". Kampuni hii, ni ya kwanza yenye makao makuu hapa Tanzania.

Kwa tafsiri nyingine, Mengi ni mtanzania "mzanea" i.e NATIVE ( Mzanea >"mzawa" i.e "by birth") wa kwanza kuleta huduma ya aina hii.Makampuni mengine yote yametoka nje.

Tumuunge mkono mzanea mwenzetu, hasa tukimpima kwa kuzingatia ubora wa king'amuzi chenyewe vs washindani wake.

Take note.

Kwa ajili ya kumbukumbu:
SERA YA UZANEA ilizungumzwa vizuri sana... kipindi kile cha mageuzi ya kisiasa hapa nchini na Mh W. Mwakitwange(RIP). Kwa wale wenye interest na hiyo sera, wafuatilie....basically inahusu "EMPOWERMENT YA WATANZANIA HALISI". MTANZANIA HALISI NI YULE AMBAYE HISTORIA YA UKOO WAKE NI ZAIDI YA VIZAZI SABA
 
Annual subscription price Increase multichoice Dear Valued Subscriber Please be advised that MultiChoice Africa’s annual subscription price increase will become effective 1 April 2013. In determining a price increase MultiChoice takes into account many factors including, and amongst others, the impact on the subscriber, current inflation, satellite lease costs, programming costs and efficiencies effected within the company. Please see new DStv subscription pricing below: Premium Bouquet: $82.00 Compact Bouquet: $32.00 DStv continues to provide world-class home television entertainment, news and sports programming in line with the best digital pay television platforms worldwide. We are most grateful for your continued support and will continue to provide a service that is consistent, efficient, and accessible. Yours sincerely Carel Snyman botswana Chief Financial Officer multichoice_logo Unsubscribe © 2013 MultiChoice (PTY) LTD. All rights reserved. Privacy Policy | Multichoice Terms & Conditions | About DStv Online | Contact us
 
kama hakuna soka vizimwe tu nchi kwani ni maigizo tu.

Mkuu soka lipo..nunua kwanza uone ubora kabla ya kuanza kureject kitu ambacho haujakiexperience.take it from me Digitek kinaubora sana hauwezi kumlinhanisha na yule jamaa wa bamaga pale..Vikiria zile sifa 7 za iko kung'amuzi alafu linganisha na ivyo vingine.Jamani acheni ubishi tu tuunge mkono bidhaa zetu za tanzania,biashara ya Mtanzania na unahudumia na watanzania wenyewe let b proud jamani
 

King'amuzi hicho ni HD kwani kina HDMI port, sasa wewe unavyosema "WANAKIITA HD" una maana gani??!!
an HDMI port does not GENERATE HD content it just transmits content that is already in HD.

hiki kidubwasha kina tangazwa as if uki kinunua utaona HD content huu ni upotoshaji na uongo mkubwa.

Mengi ameweza kufanya kitu tofauti sana.
BTL subsidiary ya IPP imepewa jukumu la kusimamia king'amuzi kinachofahamika kama "DigiTek". Kampuni hii, ni ya kwanza yenye makao makuu hapa Tanzania.
kitu gani tofauti mengi alicho fanya?
na hii BTL ni ya kwanza kwa nini?
 
Utangazaji Wa HD unahitaji transmitter ZA HD. Tunafuatilia kutoa taarifa sahihi kwani Utangazaji Wa High Definition Kwa Tanzania bado hatu a taarifa hizi. Hata DSTV wana channel cha he sana ZA HD. Ila MPEG 4 inatoa picha nzuri sana kama mgandamizo ni mzuri.
 
Taarifa rasmi, ili kujibu maswali ya wengi hapa. Hakuna kituo chochote Cha Utangazaji Tanzania kinachotangaza kwa mfumo Wa High Definition. Content Service Provider wote hakuna anayetoa matangazo Kwa mfumo huo. Aidha, kiteknolojia haiwezekani Miltplex Operator akabadilisha signal kuipeleka HD.

Tuwasaidie Watanzania kwa kuelezea ubora kama ili yotolewa kuwa ni MPEG 4 nk ambayo ina quality nzuri zaidi.
 
Kampuni zote zilizopewa leseni kutoa huduma ya dijitali zote zina ofisi Tanzania Na ni moja ya Masharti ya leseni. Kama matangazo yetu yalivyoobesha huko nyuma wakati wa kutoa leseni wamiliki walitangazwa. Agape Associates walionesha ni consortium ya Watanzania asilimia 100, hii ni pamoja na kampuni Tanzu ya kuuza Kingamuzi chao Cha Ting. Badic Transmission kina shareholder watatu, wazawa wawili na mbia toka nje na wamegawana asilimia kwa mujibu wa makubaliano yao. Star Media Tanzania hali kadhalika kina wabia wawili, Serikali ya Tanzania kupitia TBC na kampuni ya Star Media International ya China. Kampuni yao Tanzu ya kuuza vingamuzi pamoja na channel za kulipia (leseni tofauti) Star Times.
 
Back
Top Bottom